NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
Hivi kwa mtoto ambae combination haijabalance, Three ya 25 (naamini anaweza asichaguliwe advance shule za serikali), Private school wanaweza kumpokea?
 
Hapana ni First born wa shemeji yangu..
Kuhusu Mimi kwenye ukoo wetu hususani baba zangu wotee...ukoo wa mama wotee..
Pia kwenye tumbo letu katika watoto wa Tano mama alio wazaa hakuna AMBAE amewai ku fail kielimu na wote Wana degree na wote Wana Maisha yao.......last born wetu ndio kamaliza udsm hapo last year so kuhusu elimu hio sekta tupo vizuri
Kwaio Mimi automatically siwezi kuzaa mtoto kilaza 😊😊
Kwahiyo mkuu unatoka ukoo wa wasomi hongera Sana.
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 29, 2024.

Matokeo hayo yametolewa rasmi leo, Alhamisi, Januari 23, 2025, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohammed.

Wanafunzi pamoja na wazazi sasa wanaweza kuyaona matokeo hayo kupitia tovuti rasmi ya NECTA.

Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024/2025

Hongera kwa waliofanikiwa, na kwa wale ambao hawakufikia malengo, bado kuna nafasi ya kujifunza na kufanikiwa zaidi!

===================================================

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote.

Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa fursa ya kurudia mitihani ya kidato cha nne mwaka huu 2025.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed, akitangaza matokeo ya kidato cha nne leo Alhamisi Januari 23, 2025 amesema wanafunzi hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani ya kidato cha nne kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

Aidha, Baraza la Mitihani limetangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi kwenye mitihani.

Dk Said Mohammed amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili.

“Maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,”
Shule za kata zinachosha, ndio maana wanafunzi wanaandika matusi. Serikali izimulike hizi shule kwa jicho la tatu. Hizi shule zimekuwa makaburi ya kuzikia elimu ta watoto wa wakulima.
 
Shule za kata zinafelisha watoto, imagine unakuta shule ina zero 100. Serikali iifanyie kazi hili swala
 
Wazo la kuanzisha Shule za kata ni zuri sanaa, na mimi ni moja ya zao hilo. Shida iliyopo ni kwamba zinatumika ku-accomodate wanafunzi wengi ambao hawajui wanafuata nini shuleni. Jaribu kufuatilia suala hili fungua matokeo ya shule nyingi za kata, utagundua wanafunzi wengi sanaa waliopata Div IV na Div 0 ni wale waliosoma Masomo ya Arts tuu. Lakini ukichunguza Div I hadi Div III , zilizo nyingi zinatoka kwenye masomo ya Sayansi au masomo ya Biashara
Shule za kata zinachosha, ndio maana wanafunzi wanaandika matusi. Serikali izimulike hizi shule kwa jicho la tatu. Hizi shule zimekuwa makaburi ya kuzikia elimu ta watoto wa wakulima
 
Shule za kata zinachosha, ndio maana wanafunzi wanaandika matusi. Serikali izimulike hizi shule kwa jicho la tatu. Hizi shule zimekuwa makaburi ya kuzikia elimu ta watoto wa wakulima.
Tafsiri yake wale wanaochukua masomo ya Sayansi au masomo ya biashara huwa wengi wao wanajitambua nini wamefuata shuleni. Si kwamba kwenye masomo ya Sanaa hawapo, la haha wapo ila ni kwa idadi ndogo sanaa. Na hao wanasoma hayo masomo ya Sayansi au Biashara unakuta ni wale waliotazamia kuingia shule za ufundi, mkoa au wilaya.
 
Hapana ni First born wa shemeji yangu..
Kuhusu Mimi kwenye ukoo wetu hususani baba zangu wotee...ukoo wa mama wotee..
Pia kwenye tumbo letu katika watoto wa Tano mama alio wazaa hakuna AMBAE amewai ku fail kielimu na wote Wana degree na wote Wana Maisha yao.......last born wetu ndio kamaliza udsm hapo last year so kuhusu elimu hio sekta tupo vizuri
Kwaio Mimi automatically siwezi kuzaa mtoto kilaza 😊😊
Babangu alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Ilboru walioshiriki saidia fundi kwenye kuujenga uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha mwaka 1976. Babangu mdogo naye kasoma Ilboru. Hizi akili zangu nyingi ni za kurithi.
 
Back
Top Bottom