Amina68
JF-Expert Member
- Jul 16, 2021
- 298
- 547
Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limethibitisha kuwa mwanafunzi wa darasa la 7 Iptisum Suleman Slim, alibadilishiwa namba ya mtihani na uchunguzi umepelekea kugundulika kwa wanafunzi wengine 7 kubadilishiwa namba zao za mitihani, na kuchukua hatua ya kuifungia shule ya Chalize Modern kuwa kituo cha mitihani ya baraza hilo.
Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof.Adolf Mkenda, amesema uchunguzi umebaini taarifa zilizotolewa na mwanafunzi huyo ni kweli.
ITV
=========
Uchunguzi uliofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani, umebaini kuwa mwanafunzi Iptisum Suleman Slim, wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primar alibadilishiwa namba yake akiwa chumba cha Mtihani.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema uchunguzi pia umebaini wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasa la saba.
Kutokana na kosa hilo, Profesa Mkenda pia amesema Serikali imeifungia shule hiyo kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana pamoja kuagiza watumishi waliohusika na udanganyifu kuchukuliwa hatua.
Pia soma: