NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

Mwenye akili anapewa karatasi yenye namba ya mjinga ili amfanyie mtihani.

Matokeo yakitoka hiyo namba ya mjinga insonekana kafaulu sana na anaenda sekondari

Namba ya mwenye akili anapewa mjinga chumba cha mtihani yakisahihishwa.buyo.mwenye akili matokeo yake yatakuwa mabaya hivyo matapeli

Lengo la hiyo shule lilikuwa kujifelisha huyo mwenye akili na kumfaulisha mjinga

Mzazi wa mtoto mjinga anakua amehonga au?
 
Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limethibitisha kuwa mwanafunzi wa darasa la 7 Iptisum Suleman Slim, alibadilishiwa namba ya mtihani na uchunguzi umepelekea kugundulika kwa wanafunzi wengine 7 kubadilishiwa namba zao za mitihani, na kuchukua hatua ya kuifungia shule ya Chalize Modern kuwa kituo cha mitihani ya baraza hilo.

Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof.Adolf Mkenda, amesema uchunguzi umebaini taarifa zilizotolewa na mwanafunzi huyo ni kweli.

ITV

=========

Uchunguzi uliofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani, umebaini kuwa mwanafunzi Iptisum Suleman Slim, wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primar alibadilishiwa namba yake akiwa chumba cha Mtihani.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema uchunguzi pia umebaini wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasa la saba.

Kutokana na kosa hilo, Profesa Mkenda pia amesema Serikali imeifungia shule hiyo kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana pamoja kuagiza watumishi waliohusika na udanganyifu kuchukuliwa hatua.

Pia soma:
solution ya watoto walio maliza shule hiyo ikoje?
Shule imefungiwa ili khali matokeo hayajatoka na wazazi wame spent lots of money kwa ada za watoto wao
 
Huyo binti Serikali impeleke shule za vipaji maalumu anaonyesha ana akili nyingi mno kuanzia darasani hadi uelewa mkubwa wa kisheria wa kudai haki zake

Mbeleni aweza ifaa nchi huyo Nadhani naeleweka kwa wenye uelewa
Ni udanganyifu, au ni hujuma ?
 
Afande mmoja, afisa usalama mmoja, wa walimu kadhaa walikuwepo hapo wanalinda hawa nao Kwa taarifa za chini chini nao walikula mgao je tunawaachaje?

Mhe. Waziri futa kazi hao waliokuwepo siku hiyo Ili liwe funzo Kwa wote.
Pole sana, TANZANIA Ni nchi yenye Sheria , hivyo hao Kama Ni kufukuzwa Sheria lazima zifuatwe
 
Hebu fikiria huyo mtoto angeonekana kafeli maisha yangemharibikia

Yaani viongozi wa kiislamu waingilie wamlazimishe mumiliki aondoke neno Islamic kwenye jina la shule anautia aibu uislamu na kuonea watoto waislamu wenye akili kama huyo msichana wa kiislamu waliyembadilishia namba

Kumekuwa na tuhuma kuwa Vyuo vikuu vinajaa wakristo wala nguruwe waislamu eti wengi wanafelishwa sekondari kumbe kwenye shule zenyewe za waislamu kuna Tatizo.Sasa huyo kilaza asiye na akili ambaye huyo aliyebadilishiwa namba isingegundulika angeenda sekondari na huyo mwenye akili angeonekana akili hana kafeli anabaki nyumbani

Sasa huyo bwege asiye na akili mbele ya safari huko iwe sekondari kidato cha nne au cha sita angetoboa kweli?

Akili hana form four tu angeweza pata division zero anaenda tu kuongeza idadi ya waislamu wapata division zero sekondari!! Na kuwajengea waislamu siasa kali hoja zisizokuwa na mashiko kuwa waislamu wanafelishwa sekondari.Kumbe vilaza walipelekwa tu na viongozi wa shule za kiislamu wenye majina ya kiislamu wasionna hofu ya Allah wamehongwa kupitisha watoto nusu kaputi kwa kudhulumu wale wenye jitihada na wanaomlingania Allah kama huyo msichana
Mwenye Shule amehusikaje na hiyo kadhia?

Majibu ya uchunguzi ,yameaacha Maswali mengi bila kujibiwa.

Tumeambiwa wahusika nipamoja na watumishi wa Serikali.
Japo nimemsikia waziri akisoma majibu ya uchunguzi huo , hajaenda mbali nakutueleza kama waliangalia kwa undani zaidi. je ni uzembe au kulikua na hujuma ndani yake?

Kumbuka hata huo uzembe unazaa hujuma lakini , kama haikuwepo Nia ya dhati kumhujumu mtu au taasisi, haiwezi kuitwa hujuma mojakwamoja.
Binafsi naona mimiliki anaonewa, hata kumfungia isiwe kituo Cha mtihani Bado ni uonevu.
 
Back
Top Bottom