NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

Breaking news:

Profesa Mkenda asema wanafunzi saba walibadilishiwa namba za mtihani
Profesa Mkenda asema wanafunzi saba walibadilishiwa namba za mtihani
Jumanne, Oktoba 25, 2022

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia, Profesa Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaamu jana,akitolea ufafanuzi tukio la mwanafunzi aliyemaliza darasa la saba katika shule ya awali na msingi ya Chalinze Modern Islamic, Iptisum Slim (wa kwanza kulia) ambaye alilalamika kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kwa namba isiyo yake. Picha na

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa ni kweli mwanafunzi wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary, Iptisum Slim pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasala saba.

Profesa Mkenda amebainisha hayo leo Jumanne Oktoba 25, 2022 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Uendeshaji Mitihani ya Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wataalamu wa maandishi kutoka Jeshi la Polisi (Forensic Bureau) umebainika jumla ya watahiniwa saba walibadilishiwa namba za mtihani katika kituo cha mtihani namba PS1408009 shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic” amesema Profesa Mkenda

Uchunguzi huo ulifanywa baada kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim wa kituo cha mtihani cha shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic akieleza kwamba, alibadilishiwa namba yake ya mtihani wakati akifanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) uliofanyika Oktoba 05 na 06/10/2022.

Profesa Mkenda amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo Serikali kupitia Baraza la Mitihani ilielekeza Kamati ya Uendeshaji Mitihani ya Mkoa wa Pwani kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko ya mtahiniwa na kuwasilisha taarifa Baraza la Mitihani.

Amesema kuwa uchunguzi uliofanyika pia umebaini kuwa mwanafunzi huyo pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasala saba.

“Mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim alifanya masomo matano kwa kutumia namba PS1408009/0040 na somo la sita (mwisho) kwa kutumia namba PS1408009/0039 na Watahiniwa wengine wanne pia walibadilishiwa namba katika somo la sita katika kituo hicho,” amesema.

Profesa Mkenda pia amesema Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary iliyoko mkoani Pwani imefungiwa kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana.

Vilevile, Profesa Mkenda ameagiza watumishi waliohusika na udanganyifu katika mtihani wa darasa la saba Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary kuchukuliwa hatua.

Pia, Profesa Mkenda ameiagiza Necta kumefanya marekebisho ya namba za mitihani za watahiniwa husika ili kila mtahiniwa aweze kutunukiwa matokeo yake halali.

“Nisisitize kuwa shule yoyote itakayobainika kufanya vitendo vya udanganyifu wa mitihani, itafungiwa na hata kufutwa kabisa kuendesha shughuli za elimu nchini,” anasema.


Source: Mwananchi

Mkuu nisaidie what is the point ya kumbadilishia huyu mtoto na wenzake namba? Nashindwa kuelewa
 
Afande mmoja,afisa usalama mmoja, wa walimu kadhaa walikuwepo hapo wanarinda hawa nao Kwa taarifa za chini chini nao walikula mgao je tunawaachaje?

Mh Waziri futa kazi hao waliokuwepo siku hiyo Ili liwe funzo Kwa wote
Naunga mkono hoja.
 
Maswala ya namba za wanafunzi afande anahusika vipi,yeye kazi yake ni kulinda mitihani tu
Ha ha ha! Afande kashikilia bunduki yake sawasawa ana-monitor pande zote nne za dira hata kinachoendelea huko ndani hana habari wala hayamhusu.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Afande mmoja,afisa usalama mmoja, wa walimu kadhaa walikuwepo hapo wanarinda hawa nao Kwa taarifa za chini chini nao walikula mgao je tunawaachaje?

Mh Waziri futa kazi hao waliokuwepo siku hiyo Ili liwe funzo Kwa wote
Mi naona wahusika wote wapewe kesi ya Jinai, shule isifungiwe, maana bado ina Wanafunzi wengi tu wasiokua na hatia, na Wana haki ya kupata elimu!
 
Afande mmoja, afisa usalama mmoja, wa walimu kadhaa walikuwepo hapo wanalinda hawa nao Kwa taarifa za chini chini nao walikula mgao je tunawaachaje?

Mhe. Waziri futa kazi hao waliokuwepo siku hiyo Ili liwe funzo Kwa wote.
Kuna watu huwa mnakurupuka kama Mkojo wa janaba. Afisa Usalama anaingia chumba cha mtihani? Anahusikaje na mpangilio wa Namba za Watahiniwa?
 
Elewa kuwa kuna aina tatu za wasimamizi

1. Msimamizi ( mwalimu) wa ndani ambaye ndiyo huhusika na kusimamia na kuwahudumia watahiniwa yaani wanafunzi wakati wa kufanya mtihani.

2. Msimamizi msaidizi
Huyu ni mkuu wa shule husika, hutoa ushirikiano wa document muhimu juu ya watahiniwa.

3. Msimamizi wa nje.
Huhusisha msimamizi mwenye wajibu wa kulinda eneo la kituo cha mtihani ili kusiwepo na ghasia yoyote inayoweza kuathiri ufanyikaji wa mtihani.
- msimamizi huyu ni askari yaani askari polisi au askari wa jeshi la akiba ( mgambo)

Mlinzi wa nje yaani askari hahusiki kwa namna yoyote ile na makosa ya ndani ya chuma cha mtihani.

- afisa usalama ( hasa DSO) hakai au kulinda kituo cha mtihani bali hupita tu kukagua na kuchunguza mazingira ya nje.
 
Mi naona wahusika wote wapewe kesi ya Jinai, shule isifungiwe, maana bado ina Wanafunzi wengi tu wasiokua na hatia, na Wana haki ya kupata elimu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Hapa imetumika methali ya samaki mmoja akioza wote wanaoza wakati siku hizi tunamwondoa aliyeoza wengine tunaanika juani mambo yanaendelea.
 
Huwa kuna tuzo ya Mwanamke jasiri nimesahau watoaji huyu msichana watetezi wa haki za binadamu ,vyama vya wanasheria nk wampe tuzo ya jasiri

Msichana kusimama single handedly kutafuta haki yake

Hakuna mijitu mibwege nchi hii kama hao wanaojitia watetezi wa haki za binadamu Tanzania. njaa tu unawasumbua.Mtoto kwa kuwa hakuwa na hela hakuna hata taasisi moja ya kutetea haki za jamii iliyojitokeza kumsaidia.Waliufyata sababu wanaona hamna maslahi ya hela.

Hata Chadema wanaojifanya watetezi wa wananchi hawakujitokeza walijifungia kwenye vyoo vya ofisi ya makao makuu ya Chadema Ufipa.Utafikiri hata hawakusikia malalamiko ya huyo mtoto

Huyo msichana apewe nisha ya ujasiri ita motivate wasichana wengine kuwa bold kwenye kudai haki zao ns kuwa na misimamo wanapoonewa au kutaka kuonewa

Niwapongeze waandishi wa habari wamefanya kazi kubwa sana

Unakuwa Kama shetani. CHADEMA ingeingia ungesema inatafuta kiki, imekaa kimya bado unaisema. Sijui lipi zuri kwako.
 
Wenzao wanafanya kila siku hayo ila husikii kufungiwa, wao wamejaribu tu fastaaaa
Kilichofanyika hakikubaliki na kufungia shule yote kufanya mitihani pia haikubaliki
 
Back
Top Bottom