NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

... kwenye ule uzi mwingine nili-comment "... English inajenga confidence sana ..."
Hao wengine sita mbona walikaa kimya? Au wao walikuwa wanafundishwa kwa Kiswahili?

Hoja yangu ipo hapo, matendo hayatengenezwi kwa Lugha.
 
Hao walimu waliohusika kwenye ujinga huo wamelaaniwa na watapata laana kubwa hapa duniani na akhera. Hawawezi kucheza na maisha ya watoto kwa sababu za kipuuzi wanazozijua wao wenyewe.
Hebu fikiria huyo mtoto angeonekana kafeli maisha yangemharibikia

Yaani viongozi wa kiislamu waingilie wamlazimishe mumiliki aondoke neno Islamic kwenye jina la shule anautia aibu uislamu na kuonea watoto waislamu wenye akili kama huyo msichana wa kiislamu waliyembadilishia namba

Kumekuwa na tuhuma kuwa Vyuo vikuu vinajaa wakristo wala nguruwe waislamu eti wengi wanafelishwa sekondari kumbe kwenye shule zenyewe za waislamu kuna Tatizo.Sasa huyo kilaza asiye na akili ambaye huyo aliyebadilishiwa namba isingegundulika angeenda sekondari na huyo mwenye akili angeonekana akili hana kafeli anabaki nyumbani

Sasa huyo bwege asiye na akili mbele ya safari huko iwe sekondari kidato cha nne au cha sita angetoboa kweli?

Akili hana form four tu angeweza pata division zero anaenda tu kuongeza idadi ya waislamu wapata division zero sekondari!! Na kuwajengea waislamu siasa kali hoja zisizokuwa na mashiko kuwa waislamu wanafelishwa sekondari.Kumbe vilaza walipelekwa tu na viongozi wa shule za kiislamu wenye majina ya kiislamu wasionna hofu ya Allah wamehongwa kupitisha watoto nusu kaputi kwa kudhulumu wale wenye jitihada na wanaomlingania Allah kama huyo msichana
 
Hao wengine sita mbona walikaa kimya? Au wao walikuwa wanafundishwa kwa Kiswahili?

Hoja yangu ipo hapo, matendo hayatengenezwi kwa Lugha.
... hawakuwa na significant evidence kwamba wanadhulumiwa! Kugundua hutendewi haki ni jambo moja; na kutetea haki yako unapogundua unadhulumiwa ni jambo jingine.
 
... hawakuwa na significant evidence kwamba wanadhulumiwa! Kugundua hutendewi haki ni jambo moja; na kutetea haki yako unapogundua unadhulumiwa ni jambo jingine.
Iwe ni "Vivid evidence" au "Significant evidence" wote hao waliitwa kwa Mwalimu na kuambiwa wakae kimya. Kwamba na wao walibadilishiwa namba walijua.

Kwa ivo kupigania haki kumbe siyo lazima uwe na uwezo kama wa Martin Luther King Jr wa kusema "I have a Dream".
Kumbe hata kusema "Nina ndoto" nako kunaweza kumfanya mtu kuwa mwanamapinduzi.
 
Aiseeee!! Hii nayo inabidi ifanyiwe uchunguzi wa kina,inaweza ikawa ni tatizo kubwa,wajaribu kuangalia Matokeo ya nyuma kwa huyo aliyebadilishiwa namba!!
 
Breaking news:

Profesa Mkenda asema wanafunzi saba walibadilishiwa namba za mtihani
Profesa Mkenda asema wanafunzi saba walibadilishiwa namba za mtihani
Jumanne, Oktoba 25, 2022

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia, Profesa Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaamu jana,akitolea ufafanuzi tukio la mwanafunzi aliyemaliza darasa la saba katika shule ya awali na msingi ya Chalinze Modern Islamic, Iptisum Slim (wa kwanza kulia) ambaye alilalamika kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kwa namba isiyo yake. Picha na

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa ni kweli mwanafunzi wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary, Iptisum Slim pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasala saba.

Profesa Mkenda amebainisha hayo leo Jumanne Oktoba 25, 2022 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Uendeshaji Mitihani ya Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wataalamu wa maandishi kutoka Jeshi la Polisi (Forensic Bureau) umebainika jumla ya watahiniwa saba walibadilishiwa namba za mtihani katika kituo cha mtihani namba PS1408009 shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic” amesema Profesa Mkenda

Uchunguzi huo ulifanywa baada kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim wa kituo cha mtihani cha shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic akieleza kwamba, alibadilishiwa namba yake ya mtihani wakati akifanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) uliofanyika Oktoba 05 na 06/10/2022.

Profesa Mkenda amesema kuwa baada ya kupata taarifa hiyo Serikali kupitia Baraza la Mitihani ilielekeza Kamati ya Uendeshaji Mitihani ya Mkoa wa Pwani kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko ya mtahiniwa na kuwasilisha taarifa Baraza la Mitihani.

Amesema kuwa uchunguzi uliofanyika pia umebaini kuwa mwanafunzi huyo pamoja na wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasala saba.

“Mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim alifanya masomo matano kwa kutumia namba PS1408009/0040 na somo la sita (mwisho) kwa kutumia namba PS1408009/0039 na Watahiniwa wengine wanne pia walibadilishiwa namba katika somo la sita katika kituo hicho,” amesema.

Profesa Mkenda pia amesema Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary iliyoko mkoani Pwani imefungiwa kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana.

Vilevile, Profesa Mkenda ameagiza watumishi waliohusika na udanganyifu katika mtihani wa darasa la saba Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primary kuchukuliwa hatua.

Pia, Profesa Mkenda ameiagiza Necta kumefanya marekebisho ya namba za mitihani za watahiniwa husika ili kila mtahiniwa aweze kutunukiwa matokeo yake halali.

“Nisisitize kuwa shule yoyote itakayobainika kufanya vitendo vya udanganyifu wa mitihani, itafungiwa na hata kufutwa kabisa kuendesha shughuli za elimu nchini,” anasema.

Source: Mwananchi
 
Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limethibitisha kuwa mwanafunzi wa darasa la 7 Iptisum Suleman Slim, alibadilishiwa namba ya mtihani na uchunguzi umepelekea kugundulika kwa wanafunzi wengine 7 kubadilishiwa namba zao za mitihani, na kuchukua hatua ya kuifungia shule ya Chalize Modern kuwa kituo cha mitihani ya baraza hilo.

Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof.Adolf Mkenda, amesema uchunguzi umebaini taarifa zilizotolewa na mwanafunzi huyo ni kweli.

ITV

=========

Uchunguzi uliofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani, umebaini kuwa mwanafunzi Iptisum Suleman Slim, wa Shule ya Chalinze Modern Islamic Pre and Primar alibadilishiwa namba yake akiwa chumba cha Mtihani.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema uchunguzi pia umebaini wanafunzi wengine sita walibadilishiwa namba ya mtihani katika mtihani wa taifa wa darasa la saba.

Kutokana na kosa hilo, Profesa Mkenda pia amesema Serikali imeifungia shule hiyo kuwa kituo cha mtihani kwa muda usiojulikana pamoja kuagiza watumishi waliohusika na udanganyifu kuchukuliwa hatua.

Pia soma:
Shule hizi zinazoendeleza ujinga , wizi na kughushi ndizo zinadumaza elimu nchini.
Hizi si shule bai vituo vya ujinga.
 
Hebu fikiria huyo mtoto angeonekana kafeli maisha yangemharibikia

Yaani viongozi wa kiislamu waingilie wamlazimishe mumiliki aondoke neno Islamic kwenye jina la shule anautia aibu uislamu na kuonea watoto waislamu wenye akili kama huyo msichana wa kiislamu waliyembadilishia namba

Kumekuwa na tuhuma kuwa Vyuo vikuu vinajaa wakristo wala nguruwe waislamu eti wengi wanafelishwa sekondari kumbe kwenye shule zenyewe za waislamu kuna Tatizo.Sasa huyo kilaza asiye na akili ambaye huyo aliyebadilishiwa namba isingegundulika angeenda sekondari na huyo mwenye akili angeonekana akili hana kafeli anabaki nyumbani

Sasa huyo bwege asiye na akili mbele ya safari huko iwe sekondari kidato cha nne au cha sita angetoboa kweli?

Akili hana form four tu angeweza pata division zero anaenda tu kuongeza idadi ya waislamu wapata division zero sekondari!! Na kuwajengea waislamu siasa kali hoja zisizokuwa na mashiko kuwa waislamu wanafelishwa sekondari.Kumbe vilaza walipelekwa tu na viongozi wa shule za kiislamu wenye majina ya kiislamu wasionna hofu ya Allah wamehongwa kupitisha watoto nusu kaputi kwa kudhulumu wale wenye jitihada na wanaomlingania Allah kama huyo msichana
Huyu mkuu wa shule ameaibisha sana Uislamu.
 
Aiseee yaani wasimamizi wanataka kuharibu future ya binti kwa sababu ya vipande 30 vya shekeli?
 
Wavaa kobazi wanasikitisha sana. Mkapa aliwapa chuo wamegeuza kituo cha unajimu. Wamekalia kukariri kitabu cha waarabu.
 
Naomba majina ya hao wasimamizi wa mtihani siku hiyo
Invigilator mkuu nani
Swala kubwa ni system mbovu iliyopo! Pia hao wasimamizi ni bomu tupu. Na ndio maana nchinA wenye uelewa wanafunzi wanatahiniwa kila muhula mtihani ya mwisho ni points tu zinampitisha na hakuna kufeli!

Hao wanaobadilisha namba si wachukuliwe hatua Kwa Nini Shule ifungiwe??
 
Back
Top Bottom