Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Angeanzisha mswahili angefuatiliwa hela katoa wapi.

Hukohuko Arusha Kuna shule iliyokua inatoa elimu kwa vijana wasio na uwezo wa kulipa ada, matokeo yake walipata bill ya TRA ya kufa mtu. Hivi Ile shule ilishafunguliwa?
Ipo inaitwa St jude, ipo chini ya wazungu elimu bure mpaka chuo kikuu mzazi hanunui hata pencil.
 
Hivi hiyo ngozi unaiangalia kwenye tv au huwa inawafuatilia in deep?..

Anakupenda kwa kiasi gani mpaka akulelee wewe na mwanao kwa maziwa ya kiwandani huku mkeo anasomeshwa ufundi na kulipwa nyumba plus mshahara every end of the month?.
Acha mawazo potofu, kwako unaona haiwezekani lakini wengine wameweza.
 
Tujiulize, yeye na wenzake wanafaidika nini hasa? Manake tusifurahie hii misaada in the name of misaada. In the end kuna namna anafaidika tu. Hakuna mtu mweupe mjinga mjinga.
 
Angeanzisha mswahili angefuatiliwa hela katoa wapi.

Hukohuko Arusha Kuna shule iliyokua inatoa elimu kwa vijana wasio na uwezo wa kulipa ada, matokeo yake walipata bill ya TRA ya kufa mtu. Hivi Ile shule ilishafunguliwa?
Zile zilikuwa roho ya korosho ya katili Kayafa,alitaka ile shule iwe Chato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujiulize, yeye na wenzake wanafaidika nini hasa? Manake tusifurahie hii misaada in the name of misaada. In the end kuna namna anafaidika tu. Hakuna mtu mweupe mjinga mjinga.
Wewe ulitaka asifaidike sio? Au ulitaka awe katika hali gani ili uridhike,? Wabongo Muwe na shukrani
 
Tujiulize, yeye na wenzake wanafaidika nini hasa? Manake tusifurahie hii misaada in the name of misaada. In the end kuna namna anafaidika tu. Hakuna mtu mweupe mjinga mjinga.
Wazungu nao Ni binadamu.
Jiulize wale wazungu waliokuja pwani ya afrika mashariki na kuzuia mababu zako wasichukuliwe na waarabu kwenda kuwa watumwa walifaidika na Nini?
Jiulize World vision,
JICA,
NORAD,
DOCTORS WITHOUT FRONTIERS,
CCBRT
SIDA wanafaidika na Nini?
 
Wewe ulitaka asifaidike sio? Au ulitaka awe katika hali gani ili uridhike,? Wabongo Muwe na shukrani
Hujasema ni benefits zipi anapata ili ku balance story yako!
 
Haijalishi anapata nini huyo mzungu, ila huduma anayoitoa kwa jamii yetu inatosha kumpongeza na kumtakia heri.

Tumeona baadhi ya watu wetu wakiwemo wafanya biashara wakubwa, viongozi wa serikali, viongozi wa dini hawajishughuliahi na wahitaji waliopo kwenye jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu anajitolea kutoa misaada ambapo hata serikali yetu imeshindwa kufanya lakini bado watu wanauliza huyo muhusika anafaidika na nini hapo
 
Mwizi Hana akili ya kuwekeza. Unakuta waziri Fulani amepiga mabilioni sana sana atakachowekeza Ni kujenga nyumba za kupangisha Mbweni na Mbezi beach, kununua shamba Kibaha misugusugu na kuweka ng'ombe na mbuzi. Zingine kumnunulia wife harrier, nyumba ndogo Nissan dualis. Hawana akili ya kuwekeza hata kiwanda Cha maji.
Bure kabisa
Kwahiyo kujenga nyumba za kupangisha, kununua shamba kuweka mifugo sio uwekezaji?
 
Kwahiyo kujenga nyumba za kupangisha, kununua shamba kuweka mifugo sio uwekezaji?
Unatoa ajira ngapi?
Fungua hata kiwanda Cha unga au Cha maji.
Mtu anagawa pesa mabilioni kwenye misandarusi wakati nchi haina viwanda vya mafuta ya kula, maji ya kuchota tu na kuweka kwenye chupa anashindwa kutengeneza.
Kujenga nyumba ya kupanga Ni kuwekeza sawa lkn hakuinui pato la taifa tofauti na kiwanda kinacho ajiri vijana Mia au hata ishirini.
 
Back
Top Bottom