Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Sio ujinga ni msaada...hivi waafrika mna matatizo gani?[emoji23][emoji38][emoji38][emoji38]
No free lunch duniani witty, naamini unalijua hilo. Waafrika tuna matatizo ya kupenda "slope kitonga" hayo ndio matatizo yetu!!
 
No free lunch duniani witty, naamini unalijua hilo. Waafrika tuna matatizo ya kupenda "slope kitonga" hayo ndio matatizo yetu!!
Wewe unahisi wanataka nini kwetu zaidi ya msaada mkuu?
 
Kuna bibi mmoja mwezi uliopita alikuwa katika hali ngumu sana ya maisha, ameparalise upande mmoja wote, hana hata godoro na chakula anakula mlo mmoja kwa siku tena hakina hata mafuta Hakika nililia sana pale maana nilishindwa kujizuia mbele yale, baada ya. Pale nikaongea na mtu mmoja yupo nje ambae pia anamfahamu huyo bibi nikamuelezea.
Yan pale pale akaniambia nitafute mama wa kumuhudumia kama vile kumpikia na kumuogesha kila siku, akapata kigari cha miguu mitatu na chakula kila mwezi kinanunuliwa kwa gharama za huyo Mama niliyempigia simu. Yule bibi leo anafuraha sana maana ana uhakika wa kula kila siku.
Hakika Nimeona ukuu wa Mungu.
Duuuh ulifanya jambo jema sana

Mungu ambariki huyo mtu wa nje
 
Wewe unahisi wanataka nini kwetu zaidi ya msaada mkuu?
Kuna kitu wanataka, whites are ahead of us kwa kila kitu. Wao wahenyeke mikodi kibao kwao wakuleteeni bure tu? Uzuri na sisi tunapenda vya bure so tuendelee kupewa![emoji39]
 
Anazo kusanya huko kwao toka kwa wafadhili wake ni nyingi maradufu.
 
Masai wamefanywa kivutio cha watalii kama simba na tembo na sisi tinafumbia macho.Serikali huwa inasema wazi muws inajivunia wamasai kwa sababu ni kivutio cha watalii.Wazungu nao wanawatumia masai kupiga pesa.
Huu ujinga siupendi jspokuwa mimi sio masai.
Masai wanavunjiwa sana heshima na utu wao kama binadamu.
 
Haijalishi anapata nini huyo mzungu, ila huduma anayoitoa kwa jamii yetu inatosha kumpongeza na kumtakia heri.

Tumeona baadhi ya watu wetu wakiwemo wafanya biashara wakubwa, viongozi wa serikali, viongozi wa dini hawajishughuliahi na wahitaji waliopo kwenye jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili hio hio babu zenu wakauza ardhi kwa shanga na vioo na mashuka.Eti anasaidia, bado tunawaza kusaidiwa kama vile viwete.Duuu!!!
 
Poleni na Majukumu,

Serikali yetu kwa sasa inapitia katika kipindi kigumu cha tatizo la ajira rasmi kwa vijana na watu wazima pia. Pamoja na Yote Serikali imekuwa ikisisitiza vijana wajiajiri bila kuwawezesha ni kwa namna gani vijana waweze kujiajiri.

Jijini Arusha mzungu mmoja aitwae Michael fortson yeye na mke wake wameanzisha kituo kiitwacho Neema Village ambapo mbali na kusaidia watoto yatima, wameamua kuwawezesha Wanawake Wajane, Waliotelekezwa(single mothers) na wale wasiokuwa na ajira au shughuli yoyote kwa kuwa patia yafuatayo :

MITAJI YA BIASHARA
mzungu huyo kwa kupitia taasisi aliyoianzisha yeye na mkewe bi Doris fortson huwapatia wanawake tajwa hapo juu mitaji ya biashara mbalimbali kulingana na uhitaji na uzoefu wao. Mfano mitaji ya mifugo ya kufuga kama vile kuku , biashara za sokoni nk.

MALIPO YA KILA MWEZI
Michael fortson hutoa kiasi cha pesa kila mwezi Kwa ajili ya Kujikimu wao na watoto wao kwa Wanawake wote tajwa hapo juu.

KODI YA NYUMBA NA VYOMBO VYA. NDANI
Wakina Mama wote ambao hawako kwenye nyumba zao huwezeshwa kwa kulipiwa kodi ya Miezi sita pamoja naKununuliwa vyombo vya ndani kama vile majiko ya gesi, majaba ya kuhifadhia maji, vitanda Magodoro na mashuka yake nk.

ELIMU /UFUNDI
Kuna wale wanawake wenye kupenda kujifunza kazi za ushonaji, ubunifu, ufugaji nk. Hupewa mafuzo yote hapo Neema Village bure na baada ya mafuzo hupewa vyeti pamoja na Kuwezeshwa kufanya kile walichokisomea au kujifunzia hapo kwenye kituo .

WAZAZI
Kuna wale wanawake waliotelekezwa na watoto wachanga Hospitalini na. Majumbani baada ya kujifungua ambao bado ni wazazi. Basi wanawake hao hupewa huduma zote muhimu katika kipindi chote cha uzazi ikiwa ni pamoja na chakula, maziwa ya unga ya watoto, pampers,lishe pamoja na nguo za watoto na gharama za kumpeleka mtoto kiliki.

Pamoja na mambo mengine mengi ambayo Neema Village imekuwa ikisaidia kwa wakinama wote wenye uhitaji mkoani Arusha pia imetoa huduma ya kuchimba visima vya maji na kuweka masimtank kwenye viunga bure kwa wananchi wote wanao zunguka eneo hilo.

Lengo la Neema Village ni kupanua wigo zaidi na Kufikia walengwa tofauti tofauti.

Je serikali yetu imeshindwa kuwawezesha vijana wetu kwa namna yoyote ile? mfano wa large scale agriculture, kilimo chenye tija.
Kuwataftia masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi,mosoko nje ya nchi yangesaidia sana katika uchumi wetu maana yanaleta /yanaingiza pesa ndani ya nchi na hivyo kuongezeka Kwa mapato

Kufungua Ranch kila wilaya ambapo vijana wengi wangeajiriwa huko

Kuomba misaada mbali mbali katika mataifa ya magharibi ikiwemo ajira za vijana na Masomo katika nchi hizo kuliko kila siku kukopa fedha ambazo hatujui zinaenda wapi.



View attachment 1986499
Serikali haijashindwa popote ila kwanza tuzione kura zao na kadi za zao za CCM.
 
Wazungu nao Ni binadamu.
Jiulize wale wazungu waliokuja pwani ya afrika mashariki na kuzuia mababu zako wasichukuliwe na waarabu kwenda kuwa watumwa walifaidika na Nini?
Jiulize World vision,
JICA,
NORAD,
DOCTORS WITHOUT FRONTIERS,
CCBRT
SIDA wanafaidika na Nini?
CONCERN walitujengea shela ya msingi msaada miaka hiyo hadi leo ipo kijijini sna hawakufaidika na chochote
 
Concern ya mbongo ni kupiga tu. Yeye haangalii madhara ilmrad fedha anaingiza basi.

Utasikia huyu mzungu anapiga hela nyingi sana.
 
Back
Top Bottom