Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Neema Village, Mzungu anayebadilisha maisha ya Wakina Mama Arusha, serikali yetu inakwama wapi?

Poleni na Majukumu,

Serikali yetu kwa sasa inapitia katika kipindi kigumu cha tatizo la ajira rasmi kwa vijana na watu wazima pia. Pamoja na Yote Serikali imekuwa ikisisitiza vijana wajiajiri bila kuwawezesha ni kwa namna gani vijana waweze kujiajiri.

Jijini Arusha mzungu mmoja aitwae Michael fortson yeye na mke wake wameanzisha kituo kiitwacho Neema Village ambapo mbali na kusaidia watoto yatima, wameamua kuwawezesha Wanawake Wajane, Waliotelekezwa(single mothers) na wale wasiokuwa na ajira au shughuli yoyote kwa kuwa patia yafuatayo :

MITAJI YA BIASHARA
mzungu huyo kwa kupitia taasisi aliyoianzisha yeye na mkewe bi Doris fortson huwapatia wanawake tajwa hapo juu mitaji ya biashara mbalimbali kulingana na uhitaji na uzoefu wao. Mfano mitaji ya mifugo ya kufuga kama vile kuku , biashara za sokoni nk.

MALIPO YA KILA MWEZI
Michael fortson hutoa kiasi cha pesa kila mwezi Kwa ajili ya Kujikimu kwa Wanawake wote tajwa hapo juu.

KODI YA NYUMBA NA VYOMBO VYA. NDANI
Wakina Mama wote ambao hawako kwenye nyumba zao huwezeshwa kwa kulipiwa kodi ya Miezi sita pamoja naKununuliwa vyombo vya ndani kama vile majiko ya gesi, majaba ya kuhifadhia maji, vitanda Magodoro na mashuka yake nk.

ELIMU /UFUNDI
Kuna wale wanawake wenye kupenda kujifunza kazi za ushonaji, ubunifu, ufugaji nk. Hupewa mafuzo yote hapo Neema Village bure na baada ya mafuzo hupewa vyeti pamoja na Kuwezeshwa kufanya kile walichokisomea au kujifunzia hapo kwenye kituo .

WAZAZI
Kuna wale wanawake waliotelekezwa na watoto wachanga Hospitalini na. Majumbani baada ya kujifungua ambao bado ni wazazi. Basi wanawake hao hupewa huduma zote muhimu katika kipindi chote cha uzazi ikiwa ni pamoja na chakula, maziwa ya unga ya watoto, pampers,lishe pamoja na nguo za watoto na gharama za kumpeleka mtoto kiliki.

Pamoja na mambo mengine mengi ambayo Neema Village imekuwa ikisaidia kwa wakinama wote wenye uhitaji mkoani Arusha pia imetoa huduma ya maji ya Kisima na masimtank kwenye viunga bure kwa wananchi wote wanao zunguka eneo hilo.

Lengo la Neema Village ni kupanua wigo zaidi na Kufikia walengwa tofauti tofauti.

Je serikali yetu imeshindwa kuwawezesha vijana wetu kwa namna yoyote ile? mfano wa large scale agriculture, kilimo chenye tija.
Kuwataftia masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi,

Kuomba misaada mbali mbali katika mataifa ya magharibi ikiwemo ajira za vijana na Masomo katika nchi hizo kuliko kila siku kukopa fedha ambazo hatujui zinaenda wapi.



View attachment 1986499
Wazungu lazma waingie peponi. Licha ya mabaya na machafu wanayoyafanya Duniani lakini wanajua saana kumfuraisha Mungu.

Mwafrika yeye roho mbaya tu.
 
Ni mawazo yako tu

Arusha kuna NGO nyingi sana zinazosaidia watu na wala hawapati chochote in return

Wenzetu wanautaratibu wa kutoa sadaka kwa wahitaji tofauti na sisi tunatoa sadaka kwa wachungaji
Benefit zipo tu nipo Chuga naandika sana hii miradi kwenye makampuni ya Utalii na NGOs....hii ni mbadala wa misaada ya makanisa...kila mtu anafaidika kwa nafasi yake
Some time huwa tunaruka mamtoni kufanya Fundraising
 
Hela za NSSF mijitu imejimilikisha hii ni mfano wa Roho mbaya na ukatili wa yenyewe kwa yenyewe....
 
Hela za NSSF mijitu imejimilikisha hii ni mfano wa Roho mbaya na ukatili wa yenyewe kwa yenyewe....
Ndo mana hii nchi ipo nyuma sana kutokana na ubinafsi Wa watu wachache.
Tuna safari ndefu kwa kweli
 
Hawajui ngozi nyeusi huyo watajazana wanawake wote hapo kwake walioolewa kwa kisingizio cha singo maza..........sababu moja tu ya ugumu wa maisha huku mtaani
Ugumu wa maisha unafanya mtu afanye asichokitarajia.
 
Wazungu lazma waingie peponi. Licha ya mabaya na machafu wanayoyafanya Duniani lakini wanajua saana kumfuraisha Mungu.

Mwafrika yeye roho mbaya tu.
Hahaha

Nimecheka sana mkuu[emoji23][emoji23][emoji38]
 
Tujiulize, yeye na wenzake wanafaidika nini hasa? Manake tusifurahie hii misaada in the name of misaada. In the end kuna namna anafaidika tu. Hakuna mtu mweupe mjinga mjinga.
Sio ujinga ni msaada...hivi waafrika mna matatizo gani?[emoji23][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Haijalishi anapata nini huyo mzungu, ila huduma anayoitoa kwa jamii yetu inatosha kumpongeza na kumtakia heri.

Tumeona baadhi ya watu wetu wakiwemo wafanya biashara wakubwa, viongozi wa serikali, viongozi wa dini hawajishughuliahi na wahitaji waliopo kwenye jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ndo neno la uzima[emoji122][emoji122]
 
Yaan hawaamini kama ni bure kutokana na roho za kiafrika zilivyo tunajijua[emoji848]
Kuna bibi mmoja mwezi uliopita alikuwa katika hali ngumu sana ya maisha, ameparalise upande mmoja wote, hana hata godoro na chakula anakula mlo mmoja kwa siku tena hakina hata mafuta Hakika nililia sana pale maana nilishindwa kujizuia mbele yale, baada ya. Pale nikaongea na mtu mmoja yupo nje ambae pia anamfahamu huyo bibi nikamuelezea.
Yan pale pale akaniambia nitafute mama wa kumuhudumia kama vile kumpikia na kumuogesha kila siku, akapata kigari cha miguu mitatu na chakula kila mwezi kinanunuliwa kwa gharama za huyo Mama niliyempigia simu. Yule bibi leo anafuraha sana maana ana uhakika wa kula kila siku.
Hakika Nimeona ukuu wa Mungu.
 
Back
Top Bottom