Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Ndo hicho ninachokimaanisha, kuwanyanyasa wanyonge ili uwape fursa matajiri kwa sababu wao wanaweza kutoa rushwa.
 

Nehemia Mchechu ni wizi na JPM alimfahamu vema na kumfukuza kazi.​

Bi ushugi kashauriwa na JK kumrudisha kwenye nafasi ile ile.​

JPM akarudi leo kwa bahati mbaya huyu mama ataelekea wapi?​

 
Tunataka jiji lipendeze hasa maeneo prime.
Hatuwezi kuacha mabanda ya mkoloni yaendelee kuwepo ambayo 75% wanaishi watu wenye uraia zaidi ya mmoja.
Kwanini na wao wasijenge nyumba za kudumu wakaishi kama kina kikwete, magufuli, mkapa nk amba wana nyumba zao.
Watu wanaishi kiujanja ujanja tu hela wanaenda kujenga canada, dubai na marekani.
Hapana hapana
 
Tibaijuka ndio bomu kuliko chochote , labda kama hakukuwa na Maslahi yake , kule kurasini Mivinjeni Tibaijuka alisimamia dhuluma ya nyumba za wakazi wale kwa kuwalipa hela ndogo , kwa kisingizio cha kupanua Bandari , baada ya watu wale kuondolewa kwa mtutu wa bunduki , hakuna bandari iliyopanuka , bali eneo aliuziwa Oil com na Bakhresa .

Zaidi ya Nusu ya wakazi walioondolewa pale wamekufa kwa msongo wa mawazo huko walikohamia .
 
Nehemia ni aina ya watendaji wapendao sifa za kijinga na mshirika wa mafisadi na ndiyo maana JPM alimla kichwa.

Vilevile, huyo ni mmoja wa waliorejeshwa na Samia ili kumkomoa marehemu JPM [emoji1]
Kumkomoa jpm au marehemu(kama kweli anaweza kukomolewa)

Jpm alikuwa sawa na ibilisi akiona mpenda maendeleo anamuumiza ili aweke wasukuma wenzake
 

Nehemia Mchechu ni wizi na JPM alimfahamu vema na kumfukuza kazi.​

Bi ushugi kashauriwa na JK kumtudisha kwenye nafasi ile ile.​

JPM akarudi leo kwa bahati mbaya huyu mama atarlekea wapu?​

Yeah ni mtu ambae JK anamuamini sana.

Kurudi tu upya serikali imemkopea nyongeza kumalizia miradi ambayo JPM aligoma kutoa dhamana ya mkopo kwa sababu shirika lilishakopewa before kwa miradi hiyo hiyo ila imevuka budget probably due to poor financial management and overpricing za ufisadi.

Samia through JK wanaweza achia hiyo michezo.

Binafsi Makamba, Bashe na huyu Nehemia wachezee tu hizo hela za serikali wanavyotaka.

Ila kwenye upuuzi wao wahakikishe maamuzi yao au kwenye harakati zao za kutafuta sifa wasiumize watu wasio na hatia kama hii sera ya ubia. Wafanye huo bia lakini sio kwa kuwatoa wapangaji kwa mabavu na uonevu.

Watafute maeneo ya wazi wafanye wanavyotaka NHC no one cares what Nehemia does anymore ila upuuzi wake usigeuke stress kwa wengine kama huu mpango wa kuvunja blocks usio na kichwa wala miguu.
 
Kama watawafidia waondoke kwenye hayo maeneo ambayo ni prime

Ova
 
I can imagine hivi hawa watu awaelewi namna hayo mambo yanavyoenda vurugu maisha ya watu na psychological disturbance wanazowapelekea watu bila ya sababu.

Ovyo kweli ila hapo NHC huo mpango ulikuweko toka enzi za JK ni yeye huyo huyo ndio aliezuia na najua maeneo ya ‘Al Muntazir’ Nehemia ndio alikuwa akiyatamani sana.
 
Kama watawafidia waondoke kwenye hayo maeneo ambayo ni prime

Ova
Na kuwapa nyumba nyingine za kuhamia kwa rent zinazolingana well sawa tu.

Ila kumbuka kama ni maeneo ya mbali kuna watu inabidi waache kazi zao. Ni hivi nyumba nyingi za serikali uvunjwa kwa sababu sio safe tena au eneo husika lina uhalifu sana wanafanya regeneration ili kuvutia watu tofauti tofauti.
 
Hata maghorofa ya Jeshi njia panda ya Uwanja wa Taifa yako sokoni na wapangaji wameisha taarifiwa , sasa hivi ni kupora tu
 
NHC waache uhuni. Pale mtaa wa Samora Posta, ile parking opposite Salamander Tower, (GSM) kaipataje!?

Pale palivunjwa jengo na pakakaa muda mrefu wazi pakiwa pamezungushiwa uzio wa bati. Leo gsm kapageuza parking. Nini hasa lilikuwa dhumuni la kuvunja jengo lililokuwa pale!?

Leo gsm kapageuza parking. Je, ameuziwa!? Au amekodi!? Na kama amekodi, nini hasa lilikuwa lengo la kubomoa lile jengo!? Na kama kalinunua, ulifanyika mnada wa kuuza eneo lile!?
 
Hilo ni moja ya eneo ambalo washasema litajengwa kwa ubia na GSM huyo huyo ndio atashinda tender ya kuwa mmbia.

Na JK mwenyewe siku hizi pamoja na mwanawe Ridhiwani wameingia kwenye property development; you get the idea kwanini Nehemia anawafaa hapo.

Anyway sipo hapa kuongea umbea wa kunyofolewa kucha ila uonevu lazima ukemewe.
 
Kama waendeleza majengo wanataka kufanya biashara ,yapo majengo ya zamani ambayo watu walishauziwa wanaweza kuongea nao waingie ubia wa kuyaendeleza.

Mfano yale majengo ya railway mtaa wa ohio opposite ppf tower. Yale wafanyakazi walishauziwa. Ila ni ya zamani. Simple tu wanaweza kuingia mkataba na wakazi wa pale, wakapangiwa sehemu nyingine, zikavunjwa na kujengwa jengo zenye ghorofa nyingi tena za kisasa kisha wakazi wakapewa umiliki wa apartment na nyingine zikabaki kwa kampuni kwa malengo ya biashara.
 
Una point Ila bado hata hizo unazosema zijengwe bado watakaa watu wa hivyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…