Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Tibaijuka ndio bomu kuliko chochote , labda kama hakukuwa na Maslahi yake , kule kurasini Mivinjeni Tibaijuka alisimamia dhuluma ya nyumba za wakazi wale kwa kuwalipa hela ndogo , kwa kisingizio cha kupanua Bandari , baada ya watu wale kuondolewa kwa mtutu wa bunduki , hakuna bandari iliyopanuka , bali eneo aliuziwa Oil com na Bakhresa .

Zaidi ya Nusu ya wakazi walioondolewa pale wamekufa kwa msongo wa mawazo huko walikohamia .
Wewe ukapona?
 
Kama waendeleza majengo wanataka kufanya biashara ,yapo majengo ya zamani ambayo watu walishauziwa wanaweza kuongea nao waingie ubia wa kuyaendeleza.

Mfano yale majengo ya railway mtaa wa ohio opposite ppf tower. Yale wafanyakazi walishauziwa. Ila ni ya zamani. Simple tu wanaweza kuingia mkataba na wakazi wa pale, wakapangiwa sehemu nyingine, zikavunjwa na kujengwa jengo zenye ghorofa nyingi tena za kisasa kisha wakazi wakapewa umiliki wa apartment na nyingine zikabaki kwa kampuni kwa malengo ya biashara.
That’s how people do things ila hawa sio ethical developers chini ya huyo bwana.

Wao wanataka vitu rahisi hakuna re-allocations wala fidia. Ni kupora tu ndio wanachojua kama ilivyo kwenye tozo.
 
Mm naunga mkono wa kuvunja nyumba maeneo ambayo ni prime areas.....
Mfano kinondoni shamba.....ile ni prime area palitakiwa pavunjwe watu wafidiwe haiwezekani eneo ambalo ni prime likaachwa squatter

Ova
Upo sawa kwenye hili, Ila hapo kwenye kufidiwa ndio utata unapokujaga. Hata hivyo serikali kulipa watu waondoke maeneo yote prime ni ngumu na ndio maana kesi kila siku haziishi.

Hata magomeni yote ile ilipaswa ivunjwe, Ila pesa ya kufidia watu ipo wapi?
 
Hilo ni moja ya eneo ambalo washasema litajengwa kwa ubia na GSM huyo huyo ndio atashinda tender ya kuwa mmbia.

Na JK mwenyewe siku hizi pamoja na mwanawe Ridhiwani wameingia kwenye property development; you get the idea kwanini Nehemia anawafaa hapo.

Anyway sipo hapa kuongea umbea wa kunyofolewa kucha ila uonevu lazima ukemewe.
Sasa naelewa kwa nini Ridhiwani kawekwa pale wizara ya Ardhi.

Na kwa kiasi fulani yale maneno kuwa JK ndiye Rais wa ukweli wa hii nchi, sasa nayaamini. Jamaa karudi muhula wa tatu kuendelea pale alipoishia.
 
Kwani hizo nyumbani mali ya nani?

Kama ni za serikali sasa utaizuiaje serikali kufanya inavyoona ni bora zaidi?

Acha kuleta mifano ya wakoloni wa kiingereza. Mbona Wachina wamevunja mijengo ya Zamani Shanghai na kujenga vitu vya ukweli na vya kisasa?.

Hakuna kuogopa mabadiliko chanya!
Mabadiliko chanya!? Wangejenga kwanza kwenye open spaces walizonazo mfano pale Billcanas ilipovunjwa, unajua mwaka wa ngapi huu pako wazi!?
 
Kwani hizo nyumbani mali ya nani?

Kama ni za serikali sasa utaizuiaje serikali kufanya inavyoona ni bora zaidi?

Acha kuleta mifano ya wakoloni wa kiingereza. Mbona Wachina wamevunja mijengo ya Zamani Shanghai na kujenga vitu vya ukweli na vya kisasa?.

Hakuna kuogopa mabadiliko chanya!
Fuatilia vizuri sera ya China hakuna alieondolewa bila ya kupewa nyumba kwanza na kupewa fidia maeneo waliyotoa wakulima.

Serikali ni administration tu sio wenye nchi na nchi inaongozwa na katiba na sheria zake.

Acha dhana potofu ya kuamini serikali ina uhalali wa kujiamulia tu kisa huku kwetu wanafanya ivyo bila ya kuwa challenged mahakamani mara nyingi.
 
Go Jeremiah it time African wamiliki nchi zao. The so called prime areas kwenye nchii hii zinakaliwa na wageni, doesn't reflect uafrica wetu
Kwamba pakishajengwa hayo majengo ya kisasa, hao wenyeji watapata uwezo wa kukaa hizo prime area na sio wageni tena!? Bila shaka unaota, ukiamka utakutana na reality. Naomba tu usifie usingizini.
 
Tunataka jiji lipendeze hasa maeneo prime.
Hatuwezi kuacha mabanda ya mkoloni yaendelee kuwepo ambayo 75% wanaishi watu wenye uraia zaidi ya mmoja.
Kwanini na wao wasijenge nyumba za kudumu wakaishi kama kina kikwete, magufuli, mkapa nk amba wana nyumba zao.
Watu wanaishi kiujanja ujanja tu hela wanaenda kujenga canada, dubai na marekani.
Hapana hapana
Hao unawasema akina Mkapa, Jk na wenzao walizawadiana (kununua kwa bei ya kutupa) zile nyumba za serikali tena kwenye prime areas. Kama wangekuwa na uchungu na hii nchi, wangeziuza kwa bei ya soko(ushindani) japo nchi ifaidike.
 
Tibaijuka ndio bomu kuliko chochote , labda kama hakukuwa na Maslahi yake , kule kurasini Mivinjeni Tibaijuka alisimamia dhuluma ya nyumba za wakazi wale kwa kuwalipa hela ndogo , kwa kisingizio cha kupanua Bandari , baada ya watu wale kuondolewa kwa mtutu wa bunduki , hakuna bandari iliyopanuka , bali eneo aliuziwa Oil com na Bakhresa .

Zaidi ya Nusu ya wakazi walioondolewa pale wamekufa kwa msongo wa mawazo huko walikohamia .
Hawa wendawazimu hawana uwezo wa kuona aibu. Wabaya sana.
 
Kumkomoa jpm au marehemu(kama kweli anaweza kukomolewa)

Jpm alikuwa sawa na ibilisi akiona mpenda maendeleo anamuumiza ili aweke wasukuma wenzake
Honestly, JPM ana mabaya yake mengi, ila ni wazi alikuwa na nia ya dhati kuona nchi inaendela na hakupenda kabisa wahuni kujipatia fedha kiujanja ujanja.
 
Ushawahi ata kuusoma mkataba wa NHC au washirika la nyumba yoyote duniani kuhusu contract terminations au rules za kuachiana mikataba and the logic behind it?

Halafu issue sio watu kuishi maisha yao yote hapo, swala ni cheap business strategy.

Ukishawatoa hao watu unawapeleka wapi? Umeshaona shirika la serikali linavunja jengo lake bila ya kuwalipa watu fidia ya decorations wali ifanya na kuwatafutia wapangaji makazi mapya kwanza sambasamba na kodi zinazoendana kabla ya kuwatoa.

Hata Magomeni quarters kulikuwa na utaratibu sahihi na hizo kodi walizoweka ingekuwa bado JPM yu hai sidhani kama angeafiki.
Ushasema jengo lake. Sasa fidia ya nini?
Decorations haziruhusiwi. zinazoruhusiwa ni zile ambazo hazitabadili structure ya jengo.
NHC wapangaji wake hawafuati sheria, haiwezi kupata faida lazima private sector iingie.
Tuache mabo yasiyo na tija, ili mradi wabia wawe wamewekewa masharti yenye tija kwa kila pande.
 
Anajidanganya mwenyewe huyo. Kapuku wa ubungo maziwa atapata wapi jeuri ya kwenda kuishi kwenye hayo majengo mapya.!?
Haya majengo ya Sasa chakavu wapangaji wazawa weusi wanauza haki ya upangaji kila siku kwa millioni 10 mpaka 20 na kurudi uswahilini kodi hawaimudu, ni Mchechu huyu huyu ndio alipandisha kodi kwa kiwango kikubwa.
Watabaki Wahindi tu kwenye NHC waswahili wote wataomba poo.
 
Ushasema jengo lake. Sasa fidia ya nini?
Decorations haziruhusiwi. zinazoruhusiwa ni zile ambazo hazitabadili structure ya jengo.
NHC wapangaji wake hawafuati sheria, haiwezi kupata faida lazima private sector iingie.
Tuache mabo yasiyo na tija, ili mradi wabia wawe wamewekewa masharti yenye tija kwa kila pande.
Tatizo lako wewe unadhani mikataba ya NHC au public housing in general duniani ni kama ile inayoandikwa na wanasheria wa barabarani kwenye hivi vyumba tunavyopanga Magomeni.

Kwa taarifa tu kuna nyumba ata za NHC unaweza fanya extension kwa kibali chao (vinginevyo bila ya kibali wanavunja au kukutoa kwa kukiuka mkataba) na watu wengi tu wamefanya extensions.

Halafu mimi wala sizungumzi compensations hizo ni makeover tu za ndani kama kitchen updates and so forth. Hayo mambo unalipwa popote duniani unapoamishwa in addition to other costs kama za extension, amount of time uliyokaa kwenye nyumba and so forth.

Halafu kabla ya kumuamisha mtu unatakiwa kumpatia substitute property (hii sidhani) kama ipo kwenye mikataba ya NHC but that is customary kwenye public housing; uwezi kutoa watu tu kiholela that is inhumane.

Wewe ujawahi kupanga public housing popote duniani so stop kuongelea vitu kwa kuunga unga tu.
 
Back
Top Bottom