Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Tuache udezo dezo, shirika litajiendesha vipi, nyumba zenyewe wanakaa wahindi, wanalipa pesa uchwara, shirika lazima lijiendeshe kama huwezi unahama unaenda kuishi keko, mtoni, zakiem, bungu, ikiwiriri masiha yaendelee. taasisi na mashirika lazima yaanza sasa kujiendesha kwa 100%.

Tumuache Lukosi afanye kazi yake habahatishi
 
National Housing hazikujengwa ili watu wakae maisha yao yote, na wajukuu wazirithi pia.
Ni kama transitional programme. kwa hiyo siyo sawa watu kudhani zile ni nyumba zao.
National Housing hazikujengwa ili watu wakae maisha yao yote, na wajukuu wazirithi pia.
Ni kama transitional programme. kwa hiyo siyo sawa watu kudhani zile ni nyumba zao.
La msingi hapa ni wanaitwa wapangaji kwenye hizo ngumba kujitambua na kitambua nafasi zao kama wapangaji na wala siyo wenye nyumba na hizo nyumba ni kwamba wanaishj mle kwa sababu mwenye nyumba naye ameridhia wakae huku wakilipa kodi ya pango hivyo ridhaa ya kuendelea kuwa mpangaji inatoka pande zote mbili yaani kwa mwenye nyumba na kwa mpangaji na inapofika kipindi mwenye nyumba anataka kuibadilisha nyumba yake ili aweze pia kunufaika na hiyo nyumba basi mpangaji hawezi kumnyima mwenye nyumba hiyo nafasi, miaka hiyo ya nyuma walikaa hao wapangaji wakijilipia kodi ndogo kwa sababu maisha yalikuwa rahisi pia na shirika nalo lilikuwa halijakaa ktk muundo kujiendesha kibiashara pengine ilipatikana pesa kidogo ya kutosha kuwalipa mishahara wafanyakazi wa NHC na hata kama isingetosha serikali iliyapatia haya mashirika ruzuku za kujikimu ili yaendelee kuwepo na yajiendeshe kwa hasara ni tofauti na wakati huu maisha yamebadilika shirika limekuwa na limehipanga kujiendesha kibiashara na serikali haiwapi tena ruzuku lakini pia tukumbuke kwamba shirika likipata faida siyo kwamba watafaidi tu wapangaji wa nyumba za shirika bali ni raia wote maana hili ni shirika la uma na pia serikali ikilipatia shirika ruzuku ni pesa ambayo inawaumiza uma ambao siyo wapangaji maana tunawasaidia walio wachache ambao ni wapangaji kumbe kinyume chake hii pesa ingekwenda kutekeleza miradi mingine ya maendeleao na shirika likipata faida serikali itapata gawio ambalo litawafaidisha watanzania wote. na tena tusisahau kwamba nchi inatakiwa iendelee ikiwa ni pamoja na kuweka majengo mazuei na ya kisasa sehemu zenye kustahili.hao wanaoishi humo ni muda wa kusogea tena nje ya mji kidogo ambako pia nyumba za kupanga zinapatikana za bei nafuu waziache hizi ambazo wapangaji wenye kulipa vizuri wanapatikana kirahisi maana watatulipa pesa nzuri na hatuwezi kuwajengea sehemu ambazo siyo prime tukitegemea kulipwa vizuri
 
Hizi ndio fikra za choyo kwanini asiende jenga hayo maeneo kuwaweka watanzania wengi zaidi kwenye nyumba hasa wafanyakazi wa serikali.

Miji inatanuka vipi kama serikali aitaki kuwekeza maeneo mengine.

Binafsi nina rafiki yangu kakulia Upanga nyumba ya serikali kajenga kwake Kinyerezi shughuli zake zipo huko alikuwa anasubiri shopping mall tu iishe ya mtoto mmoja wa Kigogo (sijui kama ishaisha) alisema ikiisha hiyo tu akienda mbali sana taifa kuangalia mpira. Kila kitu otherwise anachokitaka kipo Kinyerezi.

Tatizo la hawa watu ni kukariri awataki kutanua jiji kimkakati kwa kutengeneza miundombinu na kuweka huduma muhimu kama malls, shule na office space au business areas uone nje kidogo uone kama jiji alitanuki.

Wao wanachowaza ni kutengeneza easy money katika eneo la kilometre square kama nne au tano ya Dar nzima.

Hiyo kazi sio size yake miradi yote ya NHC Dar ipo ndani ya square meter 4/5 hizo tu za Dar, awaendi mbali.
 
labda maelekezo ya wakubwa na miradi ina mkono wa wakubwa, we sent some on mission so what do you expect, no wishes death nutmeg so unafanya atakayo bwana wa mataifa na majeshi ya duniani.
 
Hiyo ni sub-letting uwezi kumpangisha mtu nyumba ya kukodi hiyo automatic unanyanganywa mkataba.

Wala uwezi kumuachia mtu contract ambae hakuwa mkazi hapo automatic, ukiona mswahili kamuachia nyumba mdosi elewa kuna mtu ndani ya NHC ana facilitate huo mchezo. Vinginevyo contract unaweza waachia watu waliokulia humo ndani tu.
 
Ndiyo mfumo wa Ujamaa huo. Wakina Nyerere walitaifisha nyumba za watu binafsi walizojenga kwa jasho lao na mpaka leo hawajalipwa fidia wala kurudishiwa mali zao. Wengi waliamua kuhama nchi. Leo serikali imewageukia wale wale waliofaidika kwa mali zilizoporwa kwa wengine, mnalalamika. Malalamiko yaanze kwa pale watu binafsi walivyoporwa nyumba zao kwa sera za Ujamaa wa wakina Nyerere.
 
Toa hao Sasa usivunje majengo kwenye eneo linaloweza zalisha zaidi kisa nini?

Huna uwezo kapange kunakolingana na pesa zako.
 
labda maelekezo ya wakubwa na miradi ina mkono wa wakubwa, we sent some on mission so what do you expect, no wishes death nutmeg so unafanya atakayo bwana wa mataifa na majeshi ya duniani.
Hiki ata mimi naamini ndio kiini cha hii sera.

Hasa wakubwa wanaofanya property development siku hizi kama biashara yao na wanataka prime areas only.
 
Hiyo imeshaonekana ni fursa ya upigaji, hao watu kama wana pesa wakaanzishe miji mipya na siyo kuja na ujanja ujanja kupora maeneo ya wanyonge kwa kisingizio kwamba hawana uwezo wa kuyaendeleza.
Wewe kama ni mnyonge tafuta maeneo ya wanyonge sio ukae eneo ambalo linaweza kuwa productive kwa kisingizio cha unyonge..

Ujinga wa dizaini hii haukubaliki.kwenye Dunia ya Sasa.
 
Hiki ata mimi naamini ndio kiini cha hii sera.

Hasa wakubwa wanaofanya property development siku hizi kama biashara yao na wanataka prime areas only.
There you are mortage business pays kuliko watu wajuavyo. na huku kwenye infant state or emerging markets hakunaga depreciation ya ville, flactuation ya mortage prices. valuation ya housing in shoot kulingana na maoni binafsi, mtu anapewa billion 5 kwa nyumba ya bilion moja wanaachaje hii biashara.
 
Eti Kwa kisingizio Cha ujinga wa kuitwa wanyonge,stupid..

Tena sio tuu kupendeza bali kuingiza pesa za kuhudumia hao walalamishi wanaoitwa wanyonge..

Ni Bora mkadai kulipa fidia ya usumbufu it makes sense ila sio kupinga maendeleo Kwa kisingizio Cha unyonge..

Wamasai wamepisha maeneo kwa ajili ya maslahi mapana zaidi ya Nchi na sio blaa blaa za unyonge sijui mababubu.zenu kuzaliwa hapo and such shit.
 
Fuatilia mjadala toka mwanzo tunaongelea sera ya PPP ya NHC.

Hakuna aliesema NHC ni mali ya wakubwa.
Sera ina ubaya gani? Ipo hadi kwenye barabara ndio maana mtaanza kulipa till road kwenye baadhi ya barabara zinazojengwa kwa ushirika wa wabia..

In any way siwesi kukubaliana na huo Mtizamo wenu kwa kisingizio cha kupira ardhi ya wanyonge.
 
Hata huku wanakotaka.kuvunja sasa inawezeka sio kwingine inawezekana sio huko unakotaja pekee
 
That’s how people do things ila hawa sio ethical developers chini ya huyo bwana.

Wao wanataka vitu rahisi hakuna re-allocations wala fidia. Ni kupora tu ndio wanachojua kama ilivyo kwenye tozo.
Hakuna anaepora usipotoshe..kama hakuna fidia hilo ni swala jingine Mnaweza dai ila Sio kupinga redevelopment kwa kisingizio cha unyonge..

By the way Wale wa kimala mliowabomolea mliwapa fidia? Au hawakuwa wanyonge?
 
Na hakuna kuchekea chekeana na kudekezana kwenye maendeleo,ndio maana hayo mashirika yanakufa yaani Kodi zetu ziwe zinawabeba wengine huko mjini , pumbavu zao..

Weka private sector kuwe na nidhamu ya mali..
 
Bongo sidhani kama kuna mtu timamu anaweza nunua mortgage nyumba ya NHC.

Yaani nyumba ya 200+ million ulipe sijui 30% or whatever halafu ulipe mkopo wa kama million 160 at 18% for 30 years or whatever. Kama kuna mtu anafanya ivyo hayuko sawa.

Anyway let’s not turn this into a financial appraisal ya NHC investment. madeni yao yanayolipwa na Mwigulu kwa hela za walipa kodi badala return on investment ya miradi hayo sio matatizo yetu ni ya serikali.

Na kama wapo hao watu walionunua kwa mortage goodluck, ila nyumba nyingi walizotangaza wameuza kwa mortage in the past waliishia kupangisha tu.

Issue hapa ni kwenda kuonea watu and irresponsible government kwa raia wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…