Hivi hii sera ya ubia ya NHC ilipelekwa kabisa kwenye baraza la mawaziri, wakailewa na kusema sawa.
Mtu ana mpango wa kwenda kuvunja majengo kadhaa kisa tu yapo prime areas na kuwatoa wapangaji sio tu hana hela ya kuendeleza yeye mwenyewe bali the immorality of it all is beyond me.
Kama hela kila kitu basi sasa hivi kusingekuwa na nyumba za ovyo Mikocheni, Msasani, Tetegeta, Kariakoo, Ilala na prime areas zingine za bongo.
Kila mwenye nyumba tokea miaka ya 80 isiyoendana na nyumba zinazojengwa leo maeneo hayo sasa hivi ingekuwa keshahama kitambo kwa kuuza.
Uwezi kunyanyasa watu kwa sababu eneo ni prime na serikali ina miliki nyumba kwa hivyo vunja tu.
Juzi raisi Samia katoka kwenye msiba uingereza eneo alilopanda basi maeneo ya ‘Marble Arch’ mbele kidogo tu ‘Oxford Street’ sidhani kama kuna prime area duniani kama hapo (labda Tokyo) na kuna council flats zilijengwa zamani. Safari yake ya mile mbili kufika msibani mpaka Westminster njia nzima ina sehemu kuna nyumba za serikali in short ‘west end’ yote ina maeneo yana council flats ambazo ingelikuwa ni matakwa ya matajiri tu wangeshanunua zote na kuzivunja. Lakini hata kwa nchi za mabeberu it’s immoral and inhumane uwezi fanya ivyo.
Na ndio sera inayofanya watu matajiri watafute maeneo mengine ya kuendeleza na kutengeneza future prime areas.
Ni hivi huyu Nehemia hana uwezo na nafasi anayopewa hapo NHC alianza Tibaijuka kumfunga speed governor alizuia huu mpango alipokuwa waziri, Lukuvi nae akamfunga tena speed governor kwenye kuwapandishia kodi wapangaji kwa asilimia 200% na kumtaka aache tena kupandisha kodi ovyo (hizo zilikuwa zama za J.K) na Magufuli ndio akamtibua kabisa kwa kutaka kuendelea serikali kumpatia dhamana ya mikopo ambayo inaishia kuhudumiwa na walipa kodi badala ya miradi anayojenga.
Huyo mtu hana uwezo wa kufanya miradi ya kibiashara inayohitaji mbinu anataka vitu rahisi tu kutekelezeka.
Hiyo sera inaenda waumiza watu kwa sababu ambazo hazina msingi wa kibiashara ya shirika la umma ata kidogo.
Mleta mada hauko sahihi, nahisi una maslahi binafsi.
Kuweka sawa hili, ngoja niandike machache kufafanua.
1. Hatuwezi kuwapangia nini cha kufanya NHC kwenye nyumba wanazozimiliki. Lolote watakaloliamua ni haki yao, kwa kuwa nyumba ni zao.
2. Hakuna upangaji wa kudumu au milele kwenye nyumba za NHC. Mpangaji yoyote anaweza kuondolewa mkataba wake ukiisha. Shirika litakupa notice ya miezi mitatu kabla ya mkataba wako kwisha kuwa uondoke, baada ya hapo utajua utakapokwenda, na shirika haliwajibiki.
3. Unapopangishwa ndani ya nyumba za NHC kisheria hupaswi kuendeleza, kukarabati au kuboresha chochote. Mambo hayo ni jukumu la shirika sio la kwako, na ikitokea umefanya hayo kwa nia njema kabisa hiyo itakuwa ni hisani (hupaswi kudai kufidiwa chochote) otherwise uwe na mapatano ya kisheria katika hilo na NHC. Na ikiwa sheria/mkataba utakiukwa ni vyema kukimbilia mahakamani kupinga.
4. Sehemu kubwa ya wapangaji wa asili kwenye nyumba za NHC (nyingi zikiwa Prime area) ni kama wanakaa bure, kodi wanayolipishwa ni ndogo mnoo kuliko kodi ya kupangishwa mitaa ya uswahili tena nyumba iliyochoka vibaya sana. Na kwa hali hiyo hakuna mpangaji wa NHC ambaye yuko tayari kutoka kwenye nyumba za NHC kirahisi.
5. NHC ilishabadilisha sera zake kutoka kwenye ujamaa (umaskini, huduma, hisani, umma) na kuingia kwenye ubebari (soko, ushindani, biashara, faida), hivyo ni lazima wawe na nyumba za kisasa na mwenye nguvu ya pesa ndio akae kwenye nyumba zake. Hayo yalifanyika ili NHC iweze kufufuka baada ya kuwa imeshakufa!
6. Pamoja na ufisadi mwingi, makando makando mengi ya Mchechu, lakini kiukweli ndio mtu aliyeweza kuinua upya NHC kuwa ya kisasa na kuweza kuwekeza kibebari. Yule jamaa ni mwizi kweli lakini ni mwamba haswaa.
7. Suala la NHC kuwekeza kwa ubia au kibebari haliwezi kuepukika kwa sasa, ndio dunia ya real estate ilipofikia. Japokuwa katika uwekezaji huo kuna upigaji wa kutisha, suluhisho sio kuzuia ubebari au ubia wa uwekezaji, suluhisho ni kuwa na uwazi na umakini katika uwekezaji huo.