Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Nehemia ni aina ya watendaji wapendao sifa za kijinga na mshirika wa mafisadi na ndiyo maana JPM alimla kichwa.

Vilevile, huyo ni mmoja wa waliorejeshwa na Samia ili kumkomoa marehemu JPM 😄
Heee! hii mpya, unamkomoaje mtu aliyekufa?
 
Tuwache porojo, hilo shirika asili yake ni nyumba walizodhulumiwa watu, kinachowashangaza nini? Waliodhulumu wakajiweka kwenye majunba kama vile walijenga wao au baba zao na wao zqmu yao ya kulipa dhuluma imafika.

Waliotaifishwa hayo majumba wengine walikufa kwa shock. Wengine wakawa masikini hawana hata pakuishi.

Sasa ni zamu ya wenye asili ya majunba na viwanja hivyo kurudisha tena haki yao kwa njia aliyoiona Mwenyewe mgawaji mali inafaa.

Iwe Msechu au mwengine yeyote, zitqrudi tu kwa wenye haki nazo. Haki ya ntu haipotei duniani.
 
Hivi hii sera ya ubia ya NHC ilipelekwa kabisa kwenye baraza la mawaziri, wakailewa na kusema sawa.

Mtu ana mpango wa kwenda kuvunja majengo kadhaa kisa tu yapo prime areas na kuwatoa wapangaji sio tu hana hela ya kuendeleza yeye mwenyewe bali the immorality of it all is beyond me.

Kama hela kila kitu basi sasa hivi kusingekuwa na nyumba za ovyo Mikocheni, Msasani, Tetegeta, Kariakoo, Ilala na prime areas zingine za bongo.

Kila mwenye nyumba tokea miaka ya 80 isiyoendana na nyumba zinazojengwa leo maeneo hayo sasa hivi ingekuwa keshahama kitambo kwa kuuza.

Uwezi kunyanyasa watu kwa sababu eneo ni prime na serikali ina miliki nyumba kwa hivyo vunja tu.

Juzi raisi Samia katoka kwenye msiba uingereza eneo alilopanda basi maeneo ya ‘Marble Arch’ mbele kidogo tu ‘Oxford Street’ sidhani kama kuna prime area duniani kama hapo (labda Tokyo) na kuna council flats zilijengwa zamani. Safari yake ya mile mbili kufika msibani mpaka Westminster njia nzima ina sehemu kuna nyumba za serikali in short ‘west end’ yote ina maeneo yana council flats ambazo ingelikuwa ni matakwa ya matajiri tu wangeshanunua zote na kuzivunja. Lakini hata kwa nchi za mabeberu it’s immoral and inhumane uwezi fanya ivyo.

Na ndio sera inayofanya watu matajiri watafute maeneo mengine ya kuendeleza na kutengeneza future prime areas.

Ni hivi huyu Nehemia hana uwezo na nafasi anayopewa hapo NHC alianza Tibaijuka kumfunga speed governor alizuia huu mpango alipokuwa waziri, Lukuvi nae akamfunga tena speed governor kwenye kuwapandishia kodi wapangaji kwa asilimia 200% na kumtaka aache tena kupandisha kodi ovyo (hizo zilikuwa zama za J.K) na Magufuli ndio akamtibua kabisa kwa kutaka kuendelea serikali kumpatia dhamana ya mikopo ambayo inaishia kuhudumiwa na walipa kodi badala ya miradi anayojenga.

Huyo mtu hana uwezo wa kufanya miradi ya kibiashara inayohitaji mbinu anataka vitu rahisi tu kutekelezeka.

Hiyo sera inaenda waumiza watu kwa sababu ambazo hazina msingi wa kibiashara ya shirika la umma ata kidogo.
Mleta mada hauko sahihi, nahisi una maslahi binafsi.

Kuweka sawa hili, ngoja niandike machache kufafanua.

1. Hatuwezi kuwapangia nini cha kufanya NHC kwenye nyumba wanazozimiliki. Lolote watakaloliamua ni haki yao, kwa kuwa nyumba ni zao.

2. Hakuna upangaji wa kudumu au milele kwenye nyumba za NHC. Mpangaji yoyote anaweza kuondolewa mkataba wake ukiisha. Shirika litakupa notice ya miezi mitatu kabla ya mkataba wako kwisha kuwa uondoke, baada ya hapo utajua utakapokwenda, na shirika haliwajibiki.

3. Unapopangishwa ndani ya nyumba za NHC kisheria hupaswi kuendeleza, kukarabati au kuboresha chochote. Mambo hayo ni jukumu la shirika sio la kwako, na ikitokea umefanya hayo kwa nia njema kabisa hiyo itakuwa ni hisani (hupaswi kudai kufidiwa chochote) otherwise uwe na mapatano ya kisheria katika hilo na NHC. Na ikiwa sheria/mkataba utakiukwa ni vyema kukimbilia mahakamani kupinga.

4. Sehemu kubwa ya wapangaji wa asili kwenye nyumba za NHC (nyingi zikiwa Prime area) ni kama wanakaa bure, kodi wanayolipishwa ni ndogo mnoo kuliko kodi ya kupangishwa mitaa ya uswahili tena nyumba iliyochoka vibaya sana. Na kwa hali hiyo hakuna mpangaji wa NHC ambaye yuko tayari kutoka kwenye nyumba za NHC kirahisi.

5. NHC ilishabadilisha sera zake kutoka kwenye ujamaa (umaskini, huduma, hisani, umma) na kuingia kwenye ubebari (soko, ushindani, biashara, faida), hivyo ni lazima wawe na nyumba za kisasa na mwenye nguvu ya pesa ndio akae kwenye nyumba zake. Hayo yalifanyika ili NHC iweze kufufuka baada ya kuwa imeshakufa!

6. Pamoja na ufisadi mwingi, makando makando mengi ya Mchechu, lakini kiukweli ndio mtu aliyeweza kuinua upya NHC kuwa ya kisasa na kuweza kuwekeza kibebari. Yule jamaa ni mwizi kweli lakini ni mwamba haswaa.

7. Suala la NHC kuwekeza kwa ubia au kibebari haliwezi kuepukika kwa sasa, ndio dunia ya real estate ilipofikia. Japokuwa katika uwekezaji huo kuna upigaji wa kutisha, suluhisho sio kuzuia ubebari au ubia wa uwekezaji, suluhisho ni kuwa na uwazi na umakini katika uwekezaji huo.
 
Tatizo lako wewe unadhani mikataba ya NHC au public housing in general duniani ni kama ile inayoandikwa na wanasheria wa barabarani kwenye hivi vyumba tunavyopanga Magomeni.

Kwa taarifa tu kuna nyumba ata za NHC unaweza fanya extension kwa kibali chao (vinginevyo bila ya kibali wanavunja au kukutoa kwa kukiuka mkataba) na watu wengi tu wamefanya extensions.

Halafu mimi wala sizungumzi compensations hizo ni makeover tu za ndani kama kitchen updates and so forth. Hayo mambo unalipwa popote duniani unapoamishwa in addition to other costs kama za extension, amount of time uliyokaa kwenye nyumba and so forth.

Halafu kabla ya kumuamisha mtu unatakiwa kumpatia substitute property (hii sidhani) kama ipo kwenye mikataba ya NHC but that is customary kwenye public housing; uwezi kutoa watu tu kiholela that is inhumane.

Wewe ujawahi kupanga public housing popote duniani so stop kuongelea vitu kwa kuunga unga tu.
Sasa kama wajua yote haya na sheria zipo si uende mahakamani kama unahisi haki yako itadhulikiwa?
Fudia ndo nini wee ma.laya
Umeelewa ndio maana unakwepa kujibu.
 
Wewe kama ni mnyonge tafuta maeneo ya wanyonge sio ukae eneo ambalo linaweza kuwa productive kwa kisingizio cha unyonge..

Ujinga wa dizaini hii haukubaliki.kwenye Dunia ya Sasa.
Pumbav...wenye pesa wanaenda kuanzisha miji mipya ambayo ni ya kisasa......ndo maana ukienda katikati ya jiji la London utakuta majengo ya kale yenye miaka zaidi ya miatano, makazi ya kisasa yanajengwa pembezoni
 
Pumbav...wenye pesa wanaenda kuanzisha miji mipya ambayo ni ya kisasa......ndo maana ukienda katikati ya jiji la London utakuta majengo ya kale yenye miaka zaidi ya miatano, makazi ya kisasa yanajengwa pembezoni
NHC sio ya wenye pesa ni shirika la umma la kuleta faida sio kutumiwa vibaya na nyie mnaojiita wanyonge kufilisi shirika..

Serikali inaweza twaa eneo lolote la jamhuri inapoona linafaa kwa maslahi zaidi ya wengi hata ikibidi kuharibu maslahi yenu nyie wachache mnaojificha kwenye koti la unyonge..
 
Ndipo tulipofikia hapo yaani hawa watu, hawana utu wala huruma.

Ni tamaa kwenda mbele
Hizo ni dili za upigaji, watu wanataka kuvuta rushwa kubwakubwa kwa kuwakandamiza wanyonge. Hao matajiri wakatafute maeneo pembezoni wajenge hizo prime areas, siyo kukandamiza wanyonge.
 
Sio kwamba maeneo ya wazi, hayo ni machache na ni yao NHC.

Ila wana mpango wa kuvunja blocks na kutoa wapangaji na hawana hela ya wao kuendeleza. Baada ya hapo wanatafuta matajiri wajenge wao kama wabia tu.

Sasa kwanini utoe watu in the first place.
Nyie ndo wale mlisema hamjengi mtakaa City Centre ama?

Kwa Shirika hayo ni maamuzi ya manufaa zaidi..

Mmenunua hapo au ni wapangaji?
 
Zinataka kutofautishwa sehemu za mabwana na watwana !! Mchechu from North ??!!
Hilo shirika lilianzishwa kutoa unafuu wa makazi kwa wafanyakazi na watu wa kawaida wakazi wa mjini, lakini tunashanga limebadilika kuwa la kuwajengea matajiri nyumba na sasa wanataka kumilikisha matajiri maeneo wanayoita prime areas kwa kujificha kwenye kichaka cha ubia.​
 
Embu tuwaze tu kisayansi.
Kuna jengo la ghorofa mbili la kizamani (chakavu!)la NHC lipo Upanga ambalo lina wapangaji watatu, kwa mwezi linaipa NHC jumla ya kodi ya shilingi laki tatu tena kwa kushikana mashati!

Anatokea mwekezaji anataka hilo eneo ili kujenga jengo jipya la kisasa kwa ubia na NHC. Atavunja hilo jengo na ndani ya mwaka mmoja Atajenga jengo jipya lenye urefu wa ghorofa 15, ghorofa tano za juu atawapa NHC (ambazo zitapangishwa kwa wapangaji 20, kwa mwezi wapangaji hao kwa jumla watailipa NHC wastani wa shilingi 10milioni bila longolongo!).


Sasa utawashauri NHC wabakie na jengo lao la kizamani ili kuvuna laki tatu kwa mwezi, au waingie ubia ili kuvuna milioni 10 kwa mwezi?
 
Mikataba inasemaje?

Kama mna haki nendeni mahakamani..ni issue ndogo tu mbona
Hapo hakuna cha mikataba inasemaje, shirika linakusanya kodi kwa nini lisikarabati na kujenga nyumba badala ya kutaka kuwapa matajiri hizo nyumba kwa kisingizio cha kuingia ubia, yanajengwa mazingira ya upigaji na rushwa nono nono.​
 

Hiyo ni moja ya sheria amongst several others inazo regulate hilo shirika jinsi litakavyoendeshwa na right of occupancy za wapangaji.

Mimi sio mwanasheria wa wapangaji kusema nipitie zote ila kwa kuwa ni nchi ya kufanya copy and paste ya sheria; ukipitia zote hitimisho litakuwa ni hilo hilo sio sahihi kutoa watu kiholela holela.

Kuna angle nyingi huu mjadala ungeweza ongelewa financial appraisal ya hiyo miradi au uhalali wa sheria kuvunja nyumba na kuwatoa watu kama mbwa.

Binafsi sikuwa na shida na ya angle hizo; isopokuwa ethics za hiyo sera ni shida na za unyanyasaji hakuna serikali makini inayoheshimu watu wake au CSR demands za dunia ya leo inayoweza ruhusu ata private business kuvunja mikataba ya wapangaji na kubomoa nyumba bila ya kuelewa tenants wanaenda wapi.

Mimi sitakuwa muhanga wa hilo zoezi isipokuwa hiyo sio approach sahihi ya uwekezaji wa serikali ni watu waliokosa ubinifu na utu ndio wanapenda suluhisho za ivyo zenye kuwaumiza wengine.

As for me usiku mwema and thanks all for your input.
 
Hapo hakuna cha mikataba inasemaje, shirika linakusanya kodi kwa nini lisikarabati na kujenga nyumba badala ya kutaka kuwapa matajiri hizo nyumba kwa kisingizio cha kuingia ubia, yanajengwa mazingira ya upigaji na rushwa nono nono.​
Sasa km unataka kukwepa mikataba unakua unaukataa uhalisia na haya ni malalamiko baseless kabisa
We mtu anaweza kukupangia nyumba yako uifanyeje/uitumie vipi?

Cha kuazima hakistiri matako jmn mjenge..waliojenga Boko Bunju nk si kwamba UN Road AlMuntazir hawakupaona
 
Back
Top Bottom