Hakuna shida. Sisi wananchi tunataka kuona umeme wa uhakika na wa bei nafuu unapatikana. Mwendo unaosuasua wa usambazaji umeme vijijini urudi kwenye kasi yake ya enzi za mwendazake tena bila upigaji.
Miradi mikubwa ya umeme isitetereke, ya Rufiji, Njombe na Makete. Umeme wa gesi utiliwe mkazo ili kuokoa jahazi wakati wa uhaba wa mvua unaoathiri mabwawa ya kuzalusha umeme wa maji.
Mimi sikuona shida ya Kalemani, alihitaji kukumbushwa tu kama alianza kupotoka. Makamba ni mpenda sifa na si mfuatiliaji kama alivyokua Kalemani. Yote kwa yote yetu tuwaombee wateule ili Mungu awaongoze wasimamie masilahi ya nchi na si masilahi ya watu wao na matumbo yao.