Nehemia Mchechu na Lawrence Mafuru warejea ulingoni, January Makamba awateua Wajumbe wa Bodi ya TANESCO

😍
 
Sasa watu kama wamekaa wakakubaliana wahamishe Hela kutokea Serikalini kupeleka huko,cha msingi uliza ameacha shirika katika hali gani.
 
Jakaya alifika pazuri wapi? Pa kuiba hela za umma? Wewe una akili kweli?
Utawala wa Kikwete ulikuwa na mapungufu yake LAKINI utawala wa Magufuli ulikuwa hovyo kupindukia. Ndiyo utawala ulioiondoa Tanzania kuweza kuingia kwenye uchumi wa gas.

Kama tungepata kiongozi mwenye uelewa mzuri, Tanzania sahizi usingekuwa hapa ilipo leo.
 
Hivi wajumbe wa bodi wanalipwa mshahara kila mwezi au hua inakuaje?
Wanalipwa pale wanapofanya kikao Cha bodi....ndo maana huwa wanafanya vikao kibao ili wajipe mihela kibao...maana nahisi hata posho ya kikao huwa wanapanga wenyewe
 
Hizo trillions ziko wapi na ww umekuwa swept na habari za vijiweni!!
Kamuulize Prof Assad au kamfate kiongozi wa malaika anajua alikozipeleka..

Hivi uwanja wa ndege wa Chato ulikuwamo kwenye bajeti yoyote ya hii nchi iliyopitishwa bungeni??
 
Mkuu, shida moja ya JF ni kwamba unaweza kujadiliana na mtu yeyote kwenye jambo lolote hata ambalo hana ufahamu nalo kwa undani, hiki ndio nachokiona kwako.

Sasa ili kuhitimisha haya majadiliano naomba nikubaliane na mtazamo wako kwenye kila kitu.

Ahsante.
 
Hadi Mwanaidi Maajar, Mafuru, Mchechu, Gachuma, haki ya Mungu, Mungu tusaidie, team ya ulaji hii, team JK katika bodi ya Tanesco, na wasiwasi hali inaweza kuwa mbaya mbaya sanaaa mbeleni kwenye nishati, tumekwisha, Mh. Rais Samia, kuwa macho sana, hawa wajumbe imani haipo kabisa..
 
Kamuulize Prof Assad au kamfate kiongozi wa malaika anajua alikozipeleka..

Hivi uwanja wa ndege wa Chato ulikuwamo kwenye bajeti yoyote ya hii nchi iliyopitishwa bungeni??
Habari za uwanja wa ndege Chatto kamuuliza Kagame...
 
Miluzi imekuwa mingi mpaka tumeshindwa kuelewana, swali langu je upepo wa hela mtaani utakuwaje?
 
Watu hupenda kufanya kazi na wanaowafahamu
Hili nadhan ni dunia nzima
Mfn mdogo tu kwenye soka huko kwa wenzetu huchukua wale ambao walicheza klabun kwa mafanikio na kuwafanya tena makocha wa tim
Duuuh! Hii kali, ungozi wa nchi unafananishwa na timu ya mpira kweli watanzania tumechoka. Haya mazoea ya kufanya na watu unao wafahamu ndo yalimwangusha Kikwete.
Kikwete ni moja ya viongozi wazuri sana. Ni mtu ambae hakurupuki. Lakini kilichomwangusha, japo yeye alifanya kwa nia njema ni kuweka watu anao fahamiana nao madarakani. Kweli walimuharibia. Japo Kikwete alikuwa na maono mazuri na nia njema kwa Tanzania.
Alimuweka Makamba katibu Mkuu CCM, Huyu mzee alikuwa anakula rushwa katika uchaguzi acha tu. Kuna mkubwa fulani Kikwete alimteua namfahamu, yeye alikuwa anaongea wazi kuwa Kikwete ni mshikaji wake, wametoka mbali, huyu jamaa alikuwa hawajibiki kabisa. Yeye ilikuwa ni mademu tu na kutafuta pesa kwa matajiri wakubwa.
Tunachotaka ni utendaji, hata huo mpira wanaangalia mtu kama ni mchapakazi mzuri. Ni sawa na chuo kikuu, uchukua wanafunzi wanao maliza hapo hapo chuoni kubaki kufundisha. Lakini wanaobakishwa lazima wawe na daraja la juu, na wenyekujituma. Si kujuana tu.
 
Hapo kuna kama majina manne makubwa yananitia mashaka sana na uadilifu wao kuanzia Mchechu,Mafuru,Maajar na Mzee Gachuma naona kama ni watu wa fursa zaidi,najua huyo mtoto wa Bakhressa hana njaa na hao wengine siwajui sana.
Huyu mtoto wa Bakhresa kawekwa kimukakati,Makamba atakapoanza kugombea urais awe na uhakiki was sehemu atachota pesa.
Kama alivyofanya JK kwa akina Chenge,Karamagi,Rostam nk.
 
Sibishani na mbumbumbu,Jk huyu alishindwa kufufua miundombinu ya reli,aje ajenge Sgr?miaka 25 train haikuwai kufika kilimanjaro,imefikishwa na Magufuri,alafu unasema alikuwa na akili za kujenga Sgr, wakati kuendeleza aliyoachiwa yalimushinda,kila siku ilikuwa ni kuzurula Nchi za watu, baada ya kujenga Nchi yake, ndio mtindo alioanza nao mama yenu
 
Unafikiri MOU ya Kenya, Uganda na Rwanda ilianzia wapi.. Watoto wadogo nyie hamna mnachojua
 
Huyu mtoto wa Bakhresa kawekwa kimukakati,Makamba atakopaanza kugombea urais awe na uhakiki was sehemu atachota pesa.
Kama alivyofanya JK kwa akina Chenge,Karamagi,Rostam no.
Ndio maana yake..anatengeneza timu ya kampeni kwenye ofisi ya umma...mbaya sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…