Nehemia Mchechu na Lawrence Mafuru warejea ulingoni, January Makamba awateua Wajumbe wa Bodi ya TANESCO

Nehemia Mchechu na Lawrence Mafuru warejea ulingoni, January Makamba awateua Wajumbe wa Bodi ya TANESCO

Huyu mchechu alivyokua D.G NHC alipiga madili ya Viwanja sana. Alikua ananunua viwanja kwa bei rahisi kupitia aliases then anaviuza kwa NHC kwa mabilioni, ama kweli safu nzima ya Mzee wa Msoga Itarudi yote. Yetu macho. Mama endelea kuupiga Mwingi.
Sio kweli alipokuwa D.G NHC alifanya kazi nzuri sana mpaka shirika likaanza kuludi katika hadhi yake ila siasa ikaingilia kati
 
Sio kweli alipokuwa D.G NHC alifanya kazi nzuri sana mpaka shirika likaanza kuludi katika hadhi yake ila siasa ikaingilia kati
Hadhi ya kujenga nyumba za wanyonge kuuza kwa bei ya millioni 400?

Kweli wewe ni genius.
 
Kama Dodoma kilikuwa kinashinda serikali kuamia Dodoma mpaka Magufuri alipoingia madarakani?kama unabisha mtafute mzee Mwinyi alisha kuwa Rais wa nchi hii, alisema Magufuri alifanya mambo makubwa yaliyowashinda yeye na wenzake kwa miaka 40,tena Magufuri kayafanya kwa miaka 5,tafuta You-torbe ukasikie mwenyewe
Hayakuwashinda bali hawakutaka kuhamua Dodoma.

Hata huyu Chifu Hangaya hataki jukaa Dodoma, anapenda upepo wa bahari.
 
Nchi ipo kwenye ‘catch 22’

Mama amenogewa na nafasi ya uraisi ila hana uwezo wa kuendesha nchi wala awezi mudu mikiki ya kubakia come 2025.

JK ana mbinu za kupindua meza ndani ya CCM hii ni situation mpya no one knows what to do.

JK anafahamu mbinu za kukamata madaraka which is good kumlinda mama asitishiwe nyau.

Tatizo lipo wapi kwa sababu mama hana dira JK anaamini deep down he was a good president and his measures were necessary for the nation prosperity.

So with good intentions JK anaamini mama atatimiza his unfinished business.

Yaani aoni ubaya wake, wakati JK finances zinampiga chenga sana. Yeye akiona miradi imeanzishwa hayo
kwake ni mafanikio bila ya kuelewa long term debt commitment za nchi na kama hiyo miradi imefanyiwa appropriate appraisal; ndio kama anavyolilia Bagamoyo port na gas Mtwara.

Sasa kwenye kichwa chake watu kama Nehemia walikuwa na akili sana akiona majengo waliojenga as far as JK is concerned with his limited finance understandings that is progress.

Ngoja sasa aende ofisi ya DMO wizara ya fedha wamuelezee gharama ya hiyo miradi na yeye kuiwekea guarantee wakati aijilipi kwa walipa kodi na madhara yake kwa national debt (we do know kwenye deni la taifa almost 10 trillioni ni deni la TANESCO na NHC).

Bado ujagusia matumizi mabaya ya cash cow za NHS Nehemia alivyokuwa anazitumia vibaya kuficha his bad investment kwenye cash flow kwa kuwatupia kodi za nyongeza wapangaji kwa madeni wasiohusika nayo ili kuongeza mapato ya kuhimili madeni ya bad investment alizofanya.

Hizi ndio sababu wengine tulionya mama kumtumia mtu kama JK anajichimbia shimo; kwa sababu huyo mtu aoni makosa yake.

JK naively believes he was the best president; na afanyi hivyo kwa nia mbaya it’s just psychology he actually believes he was doing the right thing.

Kuna watu inabidi wamrudishe huyu mtu kwenye dunia ya ukweli. He wasn’t a good president and he made more bad decisions than good ones; and it’s time he should step away for good. Huyu mtu ni tatizo kwa Tanzania.
Story ndefu ambayo haina ukweli wowote. Ni porojo tu na chuki za kisiasa zinakusumbua. Kama huwezi kuona mema ya Kikwete ambaye katika miaka kumi ya utawala wake uchumi ulikuwa unakuwa kwa asilimia 7,kila mwaka aliajiri na kupanndisha mishahara. Alijenga tasisi za umma. Alijenga mabarabara ya lami nchi nzima. Kama huwezi kuona mema yake,kwa sababu unazozijua wewe,ni vigumu mno kukuelewesha.
 
Mchechu huyu alie ingia NHC akawa billionea. Anafedha chafu huyo. Si mtu wa kumwamini. Kila afanyacho kwake ni deal za upigaji.
Heri Mafuru. Huyu anajituma si mpigaji kihivyo.
Lakini hivi hii nchi haina watu wengine, ni wale wale miaka yote?
Natamani jeshi lirudi enzi za kina Mwita Kyaro!!!
Watu hupenda kufanya kazi na wanaowafahamu
Hili nadhan ni dunia nzima
Mfn mdogo tu kwenye soka huko kwa wenzetu huchukua wale ambao walicheza klabun kwa mafanikio na kuwafanya tena makocha wa tim
 
Sina haja ya kuongelea kama Macho unayo
Amerusha chombo kwenda Mars au??

Kama sivyo hakuna alichofanya ambacho hakijawahi kufanywa, kama unabisha sema ambacho amefanya na hakijawahi kufanyika cha namna hiyo..
 
Kajenga Dodoma ambayo ilimshinda nyerere, kajenga Bwawa la kuzalisha umeme lililo shindikana tangu enzi za nyerere, kajenga Sgr tena kaanza na ela za ndani, Kikwete kitu ambacho kilimshinda Mpaka shirika lilikuwa limejifia,Kajenga masoko ya madini kila kanda pamoja na mitambo ya kuchenjua madini Kitu kilichozishinda serikali zilizopita,Kangalie stendi ya mbezi,angalia masoko ya kisasa yalivyojengwa kipindi cha Magufuri,hapo utujaenda kwenye miundombinu ya barabara na flyover,tena hiyo kazi kwa miaka 5 tu,ebu Wewe tueleze Kikwete kafanya nini kwa miaka kumi aliyokaa madarakani
Hapo hakuna kipya..

Mabwawa Nyerere pia alijenga, SGR ilianzia kwa JK na si yeye, ni kama tu vile Mkapa alivyoanzisha UDOM lakini ikajengwa na Kikwete. Flyover alianzisha Kikwete huyo Magufuli akiwa waziri, yeye kaja kukamilisha tu kama vile ambavyo Terminal Three na Daraja la Kigamboni alivyokuja kumalizia.

Nini kipya?? Nitajie vya kipekee sana ambavyo ni yeye binafsi tu ndio kaweza kufanya.
 
Kuhamia Dodoma nako ni jambo kubwa?

Magufuli amekuta Dodoma kuna ikulu, miundombinu na ofisi za serikali zikiwepo! Hakuikuta Dodoma jangwa bila kitu chochote!

Ameikuta Dodoma ina chuo kikuu ambapo ofisi za serikali zilianzia pale! Chuo alijenga yeye?

Acheni kuwapa watu sifa kupindukia na ndo mana Mungu akawaadhibu!
Hawa watu ni wapumbavu sana..wanaignore juhudi za viongozi waliopita waliojenga vitu vingi ili tu Jiwe aonekane..
 
Nakubaliana, sina cha kuongeza juu ya uzoefu wa wanabodi walioupata wakiwa viongozi ktk ubalozi, biashara kubwa, kampuni na idara nyeti za kuendesha masuala ya fedha na ujenzi.

Mfano mwanabodi Abubakar Bahkresa anatoka ktk viwanda binafsi, suala la umeme na uzalishaji viwandani anaelewa unyeti wa kuwa na umeme wa kuaminika na wa bei nafuu.

Balozi Mwanaidi Majaar, balozi mstaafu wa Tanzania ulaya na Marekani ya Kaskazini pia ni Mwanasheria mbobevu. Mwanaidi Sinare Majaar | Rex Attorneys | ICLG

Mchechu aliongoza NHC kwa kuonesha uthubutu uliokuwa UK mbele ya wakati kiasi akafanyiwa fitna. Nehemiah Mchechu

Lawrence Mafuru mtaalamu wa masuala ya fedha na mitaji, bila kusahau kuongoza taasisi nyeti. Hapa TANESCO watafaidika na uzoefu wake. FIMCO
😍
 
Hapo kuna kama majina manne makubwa yananitia mashaka sana na uadilifu wao kuanzia Mchechu,Mafuru,Maajar na Mzee Gachuma naona kama ni watu wa fursa zaidi,najua huyo mtoto wa Bakhressa hana njaa na hao wengine siwajui sana.
Hamna mwenye njaa hapo. Wengi walifanya kazi zao vizuri tu ila dictator alikuwa penda majungu sana
 
Hamna mwenye njaa hapo. Wengi walifanya kazi zao vizuri tu ila dictator alikuwa penda majungu sana
Unaweza kuwa na mapesa kedekede ukamiliki chochote unachotaka na bado ukawa mlafi.
Majungu yapo na wazandiki pia wapo,ni maoni yangu nawe unaweza kuamini tofauti.
 
Wewe ndio huna akili kabisa. Miaka kumi ya Kikwete uchumi wa Tanzania ulikuwa unakuwa kwa spidi ya asilimia 7! Aliajiri kila mwaka na kupanndisha mishahara. Barabara za lami nchi nzima na mahusiano yetu na nchi karibu zote duniani yalikuwa mazuri mno.
Mahusiano mazuri na nchi gani,ndo maana huyo jamaa kakuita hauna akili,Ugomvi na Rwanda,Malawi,Kenya na Uganda mpaka wakaunda COW,Kikwete ni failure anachoweza ni kuua viongozi tu hana anachoweza
 
Wenye nchi wameingia kilingeni baada ya walibatizwa kuwa 'washamba' kushindwa kwenda na kasi ya "Mapinduzi ya Nne ya Viwanda".

Viongozi 'washamba' waoga wa globalisation, multilateralism, changamoto za 4th Industrial Revolution hawafai kupewa madaraka ya kuongoza wizara, taasisi , kampuni za umma wala kampuni kubwa za binafsi.

Mfano kiongozi wa jiji la Dar es Salaam jiji la kibiashara kitovu cha kuvutia biashara za ndani ya nchi na kikanda mpaka Mashariki ya Congo, Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Burundi n.k kuogopa kulisafisha jiji letu liwe Dubai ya Afrika Mashariki kwa kuliboresha na kuwapanga upya machinga, huyo hatufai hapa Dar es Salaam. Na siyo DSm bali hata majiji mengine yote na miji nchini Tanzania yanahitaji kuongozwa na viongozi hao niliowasema wana uwezo wa kuleta mabadiliko chanya kwa kasi kubwa na kuachana na 'ushamba'.
Mkuu umewasema wapi,lakn unaweza kututajia.
Suala la machinga huwa linatatuliwa kisiasa sana, ndo maaba hakuna mpango wowite,subiri 2024 na 2025,utaniambia,sababu sasa wanaondolewa kakn hawajasema wanawapeleka wapi?
 
Hamna mwenye njaa hapo. Wengi walifanya kazi zao vizuri tu ila dictator alikuwa penda majungu sana
Ikiwa hawana njaa basi hawaitaji tena pesa? Hujui wemye pesa huwa ndio wanataka zaidi pesa
 
Back
Top Bottom