NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

N
Naunga mkono maamuzi yote ya NEMC! Kelele ni tatizo kwenye makazi ya watu
 
Sio kweli kuwa maspika kanisani yanaruhusiwa kupaza sauti.
Wachungaji wameitwa na kupewa semina kuwa hawatakiwi kuwa na kelele za kuvuka kiwango.
Haya ni maandalizi ya kufuatiliwa na kuchukuliwa hatua.
Katila hili niko na serikali 100%
NEMC washikilie hapo hapo imagine Kuna makanisa ilikuwa nyumba imegeuzwa eti kanisa Kwa eneo lililokuwa makazi wanaimba usiku mzima na ma speaker juu.
 
Ngoja nami nifungue yangu, mchana namwambia DJ anaweka playlist ya nyimbo za RNB kwa sauti ya Wastani.

Jioni hadi saa 6 usiku ni nyimbo mchanganyiko amapiano, bongoflavour, Nyimbo za Kilingala n.k

Alafu kila siku naweka Ofa kwa Afisa wa Nemc kuja kupata Msosi pamoja na Vinywaji kwa Bill zangu. Nione kama itafungwa hiyo Bar 🤗🙌🏃🏃🏃
 
Unakomaa kutetea ulevi. Pombe haram, mziki haram Bar zifungwe tu sioni faida yake zaidi ya kuleta hasara na mmomonyoko wa maadili
 
Vipi adhana za msikitini na maspika ya walokole nazo NEMC wamezifungia, waache kukurupuka kusimamia utaratibu usiokuwepo.
 
Nasikia watu wakisema Tanzania ina mapori mengi sana, wafanyabiashara wa Bar kama hawawezi kudhibiti kelele za muziki na walevi wahamishie Bar zao huko maporini mbali na makazi ya watu.
Tatizo Mbega wanapenda pombe ila za bure,hizi Cornerpub zetu ziendelee kuuburudisha umma.
 
Inashangaza unalilia kelele, bar nyingi zimewekwa katikati ya makazi ya watu. Kuna magonjwa yasiyotaka mishtuko, kuna watu kwenye kelele hawalali. Kuna wanafunzi wanahitaji kujisomea.

Mbaya zaidi hizi bar wengine wamewekeana karibu, kwa maana hiyo wanashindana nani muziki wake utasikika zaidi. Wafikirie na watu wengine wanaoishi jirani. Wafanye utaratibu muziki uwe wa wastani usiokera wengine.
 
Vipi adhana za msikitini na maspika ya walokole nazo NEMC wamezifungia, waache kukurupuka kusimamia utaratibu usiokuwepo.
Adhana na Maspika ya Walokole na Kengele za Makanisani yaendelee kuwaburudisha wanadamu.
 
Vipi adhana za msikitini na maspika ya walokole nazo NEMC wamezifungia, waache kukurupuka kusimamia utaratibu usiokuwepo.
Cha kushangaza makanisa yanayopiga kelele ni mengi kuliko bar
 
Hilo ni jambo jema sana NEMC wanafanya, wakumbuke na kelele za stendi za magari, wahubiri kwenye magari na nyumba za kidini zinazojengwa kiholela pia.
Na zile kelele zinazojirudiarudia za vispika vya wamachinga bila kusahau kelele za magari na bodaboda......jiji limejaa makelele kila kona leo unaenda kufungia baa kweli? au ndo ile kutafuta kiki tuonekane na sisi tupo tunafanya kazi.
 

Tatizo la NEMC ni moja tu, RUSHWA …….MATATIZO YA KWELI NA HATARISHI YA MAZINGIRA kama maji ya maziwa na mito kuwa polluted na mercury , methane na gas au madini mengine hatari wanayajua , wenye viwanda hasa wachina ambao hawafuati hata sheria moja ya mazingira wanawajua…
LAKINI WANAAMUA KUCHAGUA MAMBO MADOGO MADOGO YA KUWAPA UMAARUFU ILI WAONEKANE WANAFANYA KAZI …..Tanzania ni nchi kubwa sana …..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…