BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
N
Naunga mkono maamuzi yote ya NEMC! Kelele ni tatizo kwenye makazi ya watuRais Samia kupitia NEMC umeaamua kuuwa baishara za watu na kuuwa biashara za watu ni sawa na kuuwa watu kabisa!
Mh Rais wewe na wasaidizi wako mnakula raha kila siku na mko angani kila siku mnakula asali lakini sisi wananchi wengine burudani yetu ni muziki lakini mmeona tunafaidi sana ndio maana sasa mnaitumia NEMC kuhakikisha mnatupora hata hiki tulichobakiwa nacho!
Mh ukiwasikiliza baadhi ya wamiliki wa bar utagundua kabisa NEMC sasa hawana tofauti na TRA wanao funga biashara za watu…pia ni wazi kabisa hata wamiliki wenyewe hawajui kabisa hicho kipimo cha kelele badala yake wanashitukizwa na kuambiwa muziki umezidi kiwango hivyo wanafungiwa bar zao na biashara!
NEMC wamekwenda mbele zaidi wanazifungua baadhi ya bar na kumbi kutokupiga muziki kabisa…kupitia EFM nimewasikia baadhi ya wamiliki wa bar wakieleza kwa uchungu jinsi ambavyo wameharibiwa biashara zao!
NEMC wamekwenda mbele zaidi wamezifungia kabisa baadhi ya bar kupiga muziki kabisa ikiwemo Liquid bar ya dar…
Hivi kweli bar gani itaendeshwa bila muziki nchi hii? Mama Samia hawafanya biashara mnataka wakale wapi? Wataishi vipi?
Hivi kwanini mnataka kuigeuza nchi hii ni ya kidini?
Jamani pesa za serikali mnazitumbua peke yenu na hakuna anayewafanya chochote sasa mnatuzuia hata sisi kuburudika na muzuki? Mnataka tukaishi wapi?