NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

Taratibu naiona biashara ya night clubs ikirud kwa kasi... hizi bar na lounge ziliua sn biashara ya night clubs
 
Starehe zako isiwe kero kwa watu wengine! Unapokwenda bar unakwenda kupata kinywaji iwe kikali au baridi, muziki ni ziada. Na muziki siyo kelele bali burudani.

Ndani ya bar kuna watu pamoja na kupata kinywaji pia wanazungumza na kuongea. Ili mazungumzo au maongezi yawe na tija inabidi waelewane na siyo wapigizane kelele.

Bar nyingi ziko karibu na makazi ya watu ambao pia wanahitaji kupumzika na kulala na siyo kipigiwa kelele za bar hivyo wanastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa

Napongeza NEMC kwa hatua ilizoanza kuzichukua! Kwanza wamechelewa sana kuanza kutekeleza hatua za kuwafungia wote ambao biashara zao zinasababisha kelele mitaani.
 
Haya ndio matokeo ya nchi kutokupanga ardhi.

Eneo la makazi ya watu, Kuna Bar, mashine za kusaga, misikiti na makanisa.
 
Wapuz sana watu kama hawa

Utakuta nyumba iko kwenye mzkazi

Alafu ni bar basi hayo makelele sasa

Mpaka majirani wanapata kero

Hapo usiku watoto wenyewe kulala

Shida

Ova
Naomba NEMC waendelee kukaza hivo hivo hii kitu ni kero sana imagine umechoka unatafta usingizi ukiupata kelele zinaanza ukichangia na hizi stress unakesha.
 
Naomba NEMC waendelee kukaza hivo hivo hii kitu ni kero sana imagine umechoka unatafta usingizi ukiupata kelele zinaanza ukichangia na hizi stress unakesha.
Mleta mada anasema eti wanaiua sanaa
Ningependa jua sanaa gani hiyo

Ova
 
Unakomaa kutetea ulevi. Pombe haram, mziki haram Bar zifungwe tu sioni faida yake zaidi ya kuleta hasara na mmomonyoko wa maadili
Na yale makelele ya makanisani na msikitini pia yapigwe marufuku
 
MEMC wanaua Biashara na local economy kwasababu ya kumfurahisha Mzanzibari mmoja, Pombe ni asili yetu Tanganyika sio Nchi ya Kiislamu kama Zanzibar.

Karibia MEMC watatulazimisha kuvaa kanzu.
 
Sisi pia tuna allergy na mabango ya kizushi tunayolazimishwa kuyasoma kila siku stress na pressure zinatupanda.
Unaweza ukafumba macho au ukaangalia pembeni lakini sauti kubwa hakuna namna ya kutoisikia πŸ˜… zipo Bar zingine usiku kucha ni mziki mzito na ukipita Asubuhi pale mtaani itabidi upandishe suruali maana mikojo imejaa barabarani utadhani mvua ilinyesha usiku πŸ˜‚πŸ˜‚ Hatar sana !!
 
Wapi umeona vispika vya wamachinga vikawashwa usiku?. Mziki wa bar unaweza leta madhara kwa mtu mwenye presha, hasa ile mikito yake na sound effects wanazoweka maDJ
Kumbe makelele ya hivyo vispika hayakukeli mzee, mixer maspika ya matangazo, mahubiri na adhana........mbona mimi huwa nikikatiza maeneo kama kariakoo hizo kelele za vispika huwa zinanitia wenge kinyama, nakuwa natamani niondoke haraka maeneo hayo. Hao NEMC waache double standard kwenye ku-enforce sheria, vinginevyo watasababisha malalamiko kama haya.​
 
Adhana ni muito wa ibada. Hata wewe inakuhusu adhana na ungeifurahia kama ungejua tafsiri ya maneno yanayotamkwa. Karibu kwenye uislam
Kaka siamini imani hiyo kwagu ni makelele tu,hata wewe ikipigwa kengele za kanisani zitakupigia kelele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…