NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

Rais Samia kupitia NEMC umeaamua kuuwa baishara za watu na kuuwa biashara za watu ni sawa na kuuwa watu kabisa!

Mh Rais wewe na wasaidizi wako mnakula raha kila siku na mko angani kila siku mnakula asali lakini sisi wananchi wengine burudani yetu ni muziki lakini mmeona tunafaidi sana ndio maana sasa mnaitumia NEMC kuhakikisha mnatupora hata hiki tulichobakiwa nacho!

Mh ukiwasikiliza baadhi ya wamiliki wa bar utagundua kabisa NEMC sasa hawana tofauti na TRA wanao funga biashara za watu…pia ni wazi kabisa hata wamiliki wenyewe hawajui kabisa hicho kipimo cha kelele badala yake wanashitukizwa na kuambiwa muziki umezidi kiwango hivyo wanafungiwa bar zao na biashara!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wanazifungua baadhi ya bar na kumbi kutokupiga muziki kabisa…kupitia EFM nimewasikia baadhi ya wamiliki wa bar wakieleza kwa uchungu jinsi ambavyo wameharibiwa biashara zao!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wamezifungia kabisa baadhi ya bar kupiga muziki kabisa ikiwemo Liquid bar ya Dar.

Hivi kweli bar gani itaendeshwa bila muziki nchi hii? Mama Samia hawafanya biashara mnataka wakale wapi? Wataishi vipi?

Hivi kwanini mnataka kuigeuza nchi hii ni ya kidini?

Jamani pesa za serikali mnazitumbua peke yenu na hakuna anayewafanya chochote sasa mnatuzuia hata sisi kuburudika na muzuki? Mnataka tukaishi wapi?
Kwani wanakunywa muziki?
Nani kawazuia kufunga sound proof?
 
Tena mheshimiwa Raisi amechelewa kupiga marufuku huu uchafu ,hivi kuna ubaya gani kupiga mziki kwa sauti ya kawaida ? Tunambomba mheshimiwa Raisi pia atupie jicho kwenye usafri wa mabasi ,yaani wanafungulia sauti hadi unajiuliza hivi niko klabu ya mbege ama?
 
Huna hoja.
Bar lazima waweke mziki wa juu?
Kama mnataka muziki wajuu jengeni bar nje ya mji pasipo makazi ya raia.

Wananchi pembezoni mwa bar wanateseka sana.
Katika hili niko na serikali
Shida wanatakankupiga mziki Kwa sauti kubwa kupita uwezo, waweke mziki sauti ya kawaida.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
NEMC washikilie hapo hapo imagine Kuna makanisa ilikuwa nyumba imegeuzwa eti kanisa Kwa eneo lililokuwa makazi wanaimba usiku mzima na ma speaker juu.
Sio hivyo tu unakuta baa inafungulia mziki wa bongo flavaour kwa sauti hadi watoto wanajikuta wanakuuliza baba hivi paka mate mate maana yake nini ?
 
Enzi ya Nyerere bendi zilipiga muziki open bar ...ni Bayankata majogooo mpaka Lyamba

Wapiwapi Chang'ombe Bar......burudani Ijumaaa Jumamosi Jpili

Ndekuleee Njatanjata Msondongoma Sikindeee Paselepaa KumbaKumba....VangaVanga ....Kamanyola....KimbungaJKT....
Kipindi kile kulikuwa hakuna magonjwa ya moyo !!
 
Huna hoja.
Bar lazima waweke mziki wa juu?
Kama mnataka muziki wajuu jengeni bar nje ya mji pasipo makazi ya raia.

Wananchi pembezoni mwa bar wanateseka sana.
Katika hili niko na serikali
Wakijenga nje ya mji watamuuzia nani huko porini? Au watauzia bundi na panya?
 
Rais Samia kupitia NEMC umeaamua kuuwa baishara za watu na kuuwa biashara za watu ni sawa na kuuwa watu kabisa!

Mh Rais wewe na wasaidizi wako mnakula raha kila siku na mko angani kila siku mnakula asali lakini sisi wananchi wengine burudani yetu ni muziki lakini mmeona tunafaidi sana ndio maana sasa mnaitumia NEMC kuhakikisha mnatupora hata hiki tulichobakiwa nacho!

Mh ukiwasikiliza baadhi ya wamiliki wa bar utagundua kabisa NEMC sasa hawana tofauti na TRA wanao funga biashara za watu…pia ni wazi kabisa hata wamiliki wenyewe hawajui kabisa hicho kipimo cha kelele badala yake wanashitukizwa na kuambiwa muziki umezidi kiwango hivyo wanafungiwa bar zao na biashara!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wanazifungua baadhi ya bar na kumbi kutokupiga muziki kabisa…kupitia EFM nimewasikia baadhi ya wamiliki wa bar wakieleza kwa uchungu jinsi ambavyo wameharibiwa biashara zao!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wamezifungia kabisa baadhi ya bar kupiga muziki kabisa ikiwemo Liquid bar ya Dar.

Hivi kweli bar gani itaendeshwa bila muziki nchi hii? Mama Samia hawafanya biashara mnataka wakale wapi? Wataishi vipi?

Hivi kwanini mnataka kuigeuza nchi hii ni ya kidini?

Jamani pesa za serikali mnazitumbua peke yenu na hakuna anayewafanya chochote sasa mnatuzuia hata sisi kuburudika na muzuki? Mnataka tukaishi wapi?
Kwani ndio Piere mwenyewe mzee wa mjengoni,au miliki wa jiko kwa Piere.Ila ulikumbuka kama kuna chuo mbali na makazi ya watu lakini😂.Ila na nyie mmezidi wakati mwingine starehe yenu,mateso na Karaha kwa wengine,Ila sasa hata NEMC akija kutoa darasa najua atasikilizwa sasa😂😂
 
Kwanini wanapoanza kuomba vibali hawatumii muda huo kuwapa masharti na maelekezo mpaka mtu anaanza kufanya biashara? Uzembe ni wao wenyewe.
 
Ndio maana mataifa yaliyoendelea waliamua kudesign Night Clubs ili kudhibiti kelele huku biashara ikiendelea.

Ninachokiona hapa ni wamiliki wa hizi biashara kukosa ubunifu. Hata nyimbo za kupiga zinatofautiana.

Kuna miziki kama Jazz ambayo sio miziki ya kelele unaweza kuweka hata sehemu ya wazi lakini isiwe kero.

Ila shida nyimbo wanazoweka ni za mikito na makelele ambayo ukifungulia na spika ya sauti ya juu basi utaona cha mtema kuni.
 
Rais Samia kupitia NEMC umeaamua kuuwa baishara za watu na kuuwa biashara za watu ni sawa na kuuwa watu kabisa!

Mh Rais wewe na wasaidizi wako mnakula raha kila siku na mko angani kila siku mnakula asali lakini sisi wananchi wengine burudani yetu ni muziki lakini mmeona tunafaidi sana ndio maana sasa mnaitumia NEMC kuhakikisha mnatupora hata hiki tulichobakiwa nacho!

Mh ukiwasikiliza baadhi ya wamiliki wa bar utagundua kabisa NEMC sasa hawana tofauti na TRA wanao funga biashara za watu…pia ni wazi kabisa hata wamiliki wenyewe hawajui kabisa hicho kipimo cha kelele badala yake wanashitukizwa na kuambiwa muziki umezidi kiwango hivyo wanafungiwa bar zao na biashara!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wanazifungua baadhi ya bar na kumbi kutokupiga muziki kabisa…kupitia EFM nimewasikia baadhi ya wamiliki wa bar wakieleza kwa uchungu jinsi ambavyo wameharibiwa biashara zao!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wamezifungia kabisa baadhi ya bar kupiga muziki kabisa ikiwemo Liquid bar ya Dar.

Hivi kweli bar gani itaendeshwa bila muziki nchi hii? Mama Samia hawafanya biashara mnataka wakale wapi? Wataishi vipi?

Hivi kwanini mnataka kuigeuza nchi hii ni ya kidini?

Jamani pesa za serikali mnazitumbua peke yenu na hakuna anayewafanya chochote sasa mnatuzuia hata sisi kuburudika na muzuki? Mnataka tukaishi wapi?
Tatizo la kwanza nchi haina au haifusti building code yenye zones, kuweka sehemu maalum, kwamba hili ni eneo la kibiashara unaweza kujenga bar, na hili ni eneo la makazi ya watu huwezi kujenga bar.

Kumekuwa hakuna muongozo kuongoza ukijenga bar unayotaka kupiga muziki wa sauti ya juu, unatakiwa kujenga vipi, kuweka vipi sound proof material ili usiwapigie kelele watu wa nje. Kama muongozo ulikuwapo, ulikuwa haufuatwi.Serikali imewaachia watu mpaka washazoea kujenga bar ovyo, kupiga muziki ovyo, halafu inataka kumaliza tatizo kwa tangazo la mara moja.
 
Bar kuwepo makazi ya watu hakuna ubaya, tatizo ni miziki.

Mbona Mbezi Makonde kuna Bar EB25 haina kelele, Triple 7
Labda hujanielewa sina shida bar kuwa katika makazi ya watu, kelele zao ziwe na stara. Ili makundi yote hapo niliyoyataja wasidhurike na hizo kelele zao. Kutoa mfano makazi ya watu, ili wao kelele iwe ya wastani. Kuna pub ni vidogo, ila zina kelele kubwa kila siku ya wiki.
 
Mkuu huko Uingereza hakuna Viwanja vya Ndege na kelele zake? Huko Uingereza hakuna Viwanja vya mpira na makelele yake?
Ndege zinaruhusiwa masaa yote ila inategemea
Kuanzia saa 5 usiku mpaka saa moja asubuhi hazitui na kuna saa 5:30 usiku mpaka saa 12 asubuhi

Naishi karibu sana na Heathrow au tuseme niko maeneo ya Airport kabisa ila kelele hisikii kabisa kwanza madirisha yanapunguza sana kelele

Kuhusu viwanja vya mpira hilo nalo huwezi kusikia hata nilipokuwa Wimbledon kusikia kelele ni zero

Na sokoni huwezi sikia eti mtu kaweka speakers [emoji344] au kwenye Bus waweke mziki hakuna kitu kama hicho

Yaani kwenye Train na mabasi wameweka onyo kabisa ukiongea na simu heshimu wenzako
Imagine kuongea na simu unaambiwa heshimu wenzio itakuwa kelele kabisa

Kuna tofauti kubwa sana huku na huko
Nyie naona bila kelele hamuwezi kuishi mkuu
Nikija likizo kuna machinga mmoja huwa ananikera kwa spika yake ya siku nzima yaani ni kila siku

Na watu wanaona sawa tu kama wanavyotawaliwa

Kweli kelele zipo lakini ni za mda kwa mfano Happy new year utasikia mafataki na ni mda wa siku kubadilika tu
Au Diwali ya wahindi huwa wanasherehekea kwa fataki ila ni mpaka saa 5 ya usiku tu na watu wanafuata sheria haswa hata jirani wanajua ikifika saa 5 unasikia kimya
 
Na sokoni huwezi sikia eti mtu kaweka speakers
emoji344.png
au kwenye Bus waweke mziki hakuna kitu kama hicho
Mbona nasikia omba omba huwa wanapiga magitaa mbele ya Maduka makubwa na kuporomosha Mziki wenye kuburudisha?
 
Back
Top Bottom