Muziki wa Bar katika maeneo ya Makazi ni jambo hatari sana kwa taifa letu. Haiwezekani leseni za Bar sitolewe hovyo kana lilivyo sasa kwa kigezo cha mapato ya Halmashauri. Kuna watanzania wengi wabobezi wanafanya kazi za ushauri na kullipa kodi kuwa kuliko hayo makusanyo ya bar uchwala za maeneo ya makazi. Ni ushamba na uzamani kufikiri kuwa bar ndio zinazochania mapato ya halmahauri. Tunahitaji utulivu na ukimya kwenye maeneo ya makazi. Familia zina wagonjwa, wazee, watoto, wajawazito na hata vijana wanaotaka utulivu wa kufanya mambo tofauti na miziki, na shangwe za makundi ya kushaniglia mipira. Mipango miji wametenga maeneno ya starehe, watu waende huko wakapige makelele wapendavyo. Mimi naunga mkono ukomeshaji makelele katika maeneo ya makazi yakiwemo makelele ya bar, makanisa na hata misikiti.