Nikiona utetezi wa aina yeyote una "mnataka tukale wapi" nakuwa na wasiwasi nao. Sheria za mazingira si unazijua? Jitetee kwa kutumia sheria badala ya kutia huruma, badala ya kusema wanaua biashara zenu ambavyo ni accusation jiulize kama umezingatia sheria za NEMC na jitetee kisheria kama umekidhi vigezo vya kutoa huduma.
Kifungu fulani cha mwaka fulani kinataka bar iwe mita kadhaa nje ya makazi ya watu, na umetimiza.
Au ukiwa kwenye makazi ya watu upige mziki chini ya decibel ngapi, na umetimiza.
Mambo ya nitakula wapi nami naweza kuja kufungua dampo la kukodisha hapo pembeni ya bar yako likatoa harufu kali kisha niwalilie NEMC wasifunge maana nitakula wapi. Kuna sheria na huruma, inashangaza wabongo tunakimbilia huruma tunaacha sheria