Neno "DEAR" linatumika vibaya au ni Ushamba wangu

Wewe ndiyo una tatizo.
Umezeeka kama mimi na English yetu ya shule za Nyerere.
Nadhani darling, My love na honey zina maana tofauti na dear ingawa dear inawahusu wote hao wengine.
Naamini wewe ni me.
mnaitana dear na marafiki zako?
 
Dear member ushamba wako tu unakusumbua
 
Una bahati hajatokea wa kukuambia “pole my love” na hamjawahi hata kuonana😂
 
Naamini wewe ni me.
mnaitana dear na marafiki zako?
Nimekuambia mimi na wewe tumezeeka.
Ukiona hivyo situmii neno dear zaidi ya kwenye friendly letter au nikimuandikia ndugu.
Binti yangu ananiita Lovely Dad au Lovely father kwenye mail. Mimi namuita dear daughter (au jina lake).
 
Uko sahihi kabisa sio kila mtu utamuita Dear

Mwanaume kwa mwanaume ni No hata kama ni mteja

Dogo fundi anakuita Dear, sio sawa labda wewe umuite Dear ktk hali ya kumbembeleza

Kifupi Dear inasehemu yake ya kutumika
 
Vibinti vya Kichina Alibaba huwa mazungumzo yao ni Dear. Kwa maana hiyo unayosema, ungevitongoza vyote!
 
Ni ushamba wako
 
Dear umeenda mbali sana
Dear ni neno la kawaidaa mno
Mimi ndio nimezoea aisee haswa kwa wadada wenzangu nitakuita love, mpnz, babe yaani hivyo tu dear
 
Kwenye upande wa barua ipo hivyo. Formal letter lazima ianze na dear.
Ila kibongobongo kwenye maongezi ya kawaida inaleta ukakasi.

Kwahiyo wewe mshkaji wako wa kiume akikuita dear utaona sawa? Kama ni sawa tufunge huu uzi kabisa
Kwani neno ''dear'' ni la kiswahili ili ilete ukakakasi? Na kwa nini kwenye barua tu ndiyo iwe sawa lakini kwenye kutamka kwa mdomo lilete ukakasi? Huoni unajigonga mwenyewe? Mimi naweza kuitwa ''dear'' na mtu yoyote. Nlikuwa nafanya kazi kampuni moja ya wazungu, inayoendeshwa na mtu na mkwewe, na ukifanya kazi nzuri, mkewe anakumbia ''thank you dear''. Mumewe hivyo hivyo. Hili la kusema mshikaji wa kiume akiniita dear kama naona ni sawa, wala halina mjadala kwa sababu nimeshaitwa mara nyingi tu. Naona ukakasi uko kwenye mawazo yako kwa sababu ulishaelewa vibaya maana ya neno ''dear'' tangu ukiwa mdogo hivyo ni vigumu kubadilidha sasa hivi.
 
Wewe ndiyo una tatizo.
Umezeeka kama mimi na English yetu ya shule za Nyerere.
Nadhani darling, My love na honey zina maana tofauti na dear ingawa dear inawahusu wote hao wengine.
Haya maneno ni maneno ya kiingereza kutoka utamaduni mwingine na wabongo wameiga na kuyaelewa vinginevyo kabisa. Angekuwa anajua utamaduni wa wazungu angejua kuwa hata wazazi wanaweza kuita watoto wao ''my sweetheart, ''my love'', ''honey''. Wanadhani yanatumika kwa wapenzi wenye uhusiano wa kingono tu. Ni ulimbukeni kama wabongo wengi wanadhani siku ya valentine ni siku ya wapenzi kufanya ngono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…