Neno HAKI limeanza kutawala midomoni mwa watawala, alianza Rais Samia, kafuata IGP na leo nimemsikia Kinana

“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

Yoote haya yatasemwa tuu! Tiba inabakia kuwa KATIBA KATIBA Mpya.
Ndio Haki walihokibaliana pale walika mama Rais na Mwamba FAM.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umeambiwa relax naona umechoka, soma katiba inavyotenganisha haki na wajibu.

SEHEMU YA TATU: HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa

12.Usawa wa Binadamu.
13.Usawa mbele ya sheria.

Haki ya Kuishi
14.Haki ya kuwa hai.
15.Haki ya uhuru wa mtu binafsi.
16.Haki ya faragha na ya usalama wa mtu. 17.Uhuru wa mtu kwenda atakako.

Haki ya Uhuru wa Mawazo
18.Uhuru wa maoni.
19.Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo. 20.Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine. 21.Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
Haki ya Kufanya Kazi
22.Haki ya kufanya kazi.
23.Haki ya kumiliki mali.
24.Haki ya kupata ujira wa haki.

Wajibu wa Jamii
25.Wajibu wa kushiriki kazini.
26.Wajibu wa kutii sheria za nchi.
27.Wajibu wa Kulinda mali ya Umma.
28.Wajibu kwa Ulinzi wa taifa.
Hiyo ni katiba iliyotengenezwa na binadamu.

Pius Msekwa na wenzake 20.

Katiba haitoi Haki inatoa wajibu ndio sababu watu 20 waliwapangia watu milioni 60 namna ya kuishi!
Ndio inatoa haki kwa kutafsiri hizo sheria, kwani aliyeivunja sheria amemnyima mwenzie haki yake, kama haki ingekuwa inatoka kwa Mungu pekee, basi Biblia na Quran ndio vingekuwa Katiba zetu.
Unadhani kwanini Rais akiapa atashika ama Biblia au Quran?

Nakuhakikishia mahakama haina jukumu la kutoa haki.

Hata mahakama ya kanisa katoliki haitoi haki.
 
“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

Haki Huinua Taifa
 
Kama duniani hakuna haki wale wanaoenda mahakamani huenda kutafuta nini? usiniambie tena wajibu!.

Au unataka mtu akinyimwa haki yake (kuvunjiwa sheria na mwingine) aende kanisani au msikitini kupiga magoti?
Mahakamani wanaenda kupata tafsiri ya sheria zilizotungwa na bunge la wanadamu.

Mahakama haitoi haki na siyo jukumu lake!
 
Mkuu 'Tindo',
Nimesoma yanayodaiwa kusemwa na IGP Sirro hapo mwanzo wa mada, juu ya HAKI, nikatikisa kichwa kabisa!

Mtu asiyejuwa yaliyotokea chini ya uongozi wa huyu mtu wa jeshi la polisi, akisoma matamshi hayo, atasifu sana jinsi jeshi letu lilivyo na uongozi imara.
Lakini sote tupo hapa. Ni nani asiyejuwa namna ya jeshi letu la polisi lilivyogeuzwa kuwa chombo cha kukandamiza wananchi! Leo ukisikia maneno matamu hayo ndiyo yakufanye kusahau kila kitu?
Huu ni mfano tu wa huyo mmoja, Sirro. Hao wengine na wao hawana tofauti yoyote naye.

Naunga mkono hoja yako ya kugundua hizo lugha za ghiliba.
 
Mzee Kinana ni msanii sana. Anataka kuichota hadhira ya CHADEMA.

Mnakumbuka mwaka 2010 mzee Kinana alikuwa anatoa machozi kuwaombea kura na kula wana CCM?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
“Kitu kikubwa tulichojadiliana ni kuwa, Tanzania ni yetu sote na tunapaswa kufanya kazi pamoja, kuijenga, lakini hili linawezekana tu iwapo tutajenga uaminifu na kudai HAKI, pamoja na kuheshimiana”. Rais Samia Suluhu.

“Tumekubaliana kuwa, njia nzuri ya kuwa na maridhiano ni wakati kuna HAKI. Tumepitia madhila mengi, hakuna haja ya kuyarudisha mara kwa mara, badala yake tunapaswa kusonga mbele na kuwa na siasa safi na kuiunga mkono serikali”.- Freeman Mbowe.

“Mimi ndio mkuu wa jeshi la polisi leo nyie ni polisi kesho sio polisi lazima muwaheshimu watu na mtende HAKI kuna makosa mengine ya trafiki mweleweshe mtanzania mwenzako sio lazima kila kosa umuweke mahabusu”. - IGP Sirro.

“Kila mtu awe na HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa na HAKI ya kutoa mawazo. Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo na hakuna mwenye hati miliki ya mawazo. Tukiweza kuimarisha HAKI ndani ya CCM tutakuwa tumeimarisha hadi nje kwenye maeneo mengine " Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM (Bara), Abdulrahman Kinana.

Kama kweli CCM mna nia ya kusimamia haki basi tuleteeni katiba yetu mpya, ni haki yetu si ndiyo?
 
Ni maigizo kama maigizo mengine
They don't mean what they say....

Msiwe wepesi kuamini yatokayo midomoni mwa watawala
Leo mnaamini maneno ya kinywa cha mtesi ciro [emoji849]
Wote wanafanya posturing
 
Hiyo ni katiba iliyotengenezwa na binadamu.

Pius Msekwa na wenzake 20.

Katiba haitoi Haki inatoa wajibu ndio sababu watu 20 waliwapangia watu milioni 60 namna ya kuishi!

Unadhani kwanini Rais akiapa atashika ama Biblia au Quran?

Nakuhakikishia mahakama haina jukumu la kutoa haki.

Hata mahakama ya kanisa katoliki haitoi haki.
Rais anaapa kwa kutumia biblia au quran lakini akishaingia madarakani anatumia Katiba ya nchi kuongoza, hiyo ndio inatoa muelekeo wa nchi na wale wanaoongozwa ili waongozwe kwa usawa na hapo ndipo haki inapopatikana.
 
Kumbe unaelewa.

Biblia na Quruan ndio zimebeba Haki

Katiba ni mama wa sheria za kutawala!
 
Mahakamani wanaenda kupata tafsiri ya sheria zilizotungwa na bunge la wanadamu.

Mahakama haitoi haki na siyo jukumu lake!
Kwahiyo mahakama ikisha tafsiri sheria Mungu anakuja kutoa haki.
 
Haki haihitaji Mungu aje atoe bali iko tayari kwa walio wake.

Hakimu anakutafsiria wajibu wako kwa mujibu wa sheria

Kwa mfano DPP alipotaka kumtoa Mbowe gerezani alipeleka kifungu cha sheria kwa Jaji ili kitafsiriwe na Mbowe aachiliwe, na ndivyo ilivyofanyika

Lakini Mbowe anaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa lile lile.

Ila mbele ya Mungu wa mbinguni kama Mbowe hakuwa na NIA ya kutenda ugaidi basi ameishaipata Haki yake tangu akiwa gerezani!
 
Dah! Aliko Mwendazake anashangaa sana hata hawa.

0112397A-EA44-45E7-8CAB-3C6FB6E3CDA4.jpeg
 
Back
Top Bottom