Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

Wenje ni bomu Hata Mbowe ni bomu. Bora useme Halima Mdee na Catherine.
 
By the way unakumbuka Msigwa alivyokuwa anabebeshwa picha ya Samia kama watoto kwenye sherehe?

Umenikumbusha kitu.. Kuna siku dogo aliiona ile picha akaniuliza kwa mshangao kwani kafa!?😂
 
Huu urejeaji wa mamuluki usikifanye chama kikateteleka na kuvuruga safa ya mashambulizi.
Tunafahamu wapo vijana na wanachama wenye msimamo thabiti ambao hawakufikiri kukihama chama licha ya kupita ktk magumu pindi hao mamuluki wakilanda landa huko walikokimbilia, sasa isije ikatokea vijana wetu wazalendo wakawekwa kando au kutengwa kisha nafasi au fursa za kugombea uongozi kupewa hawa mamuluki.
Huko kutaleta picha mbaya na ukatili.

Mamuluki waanze upya from the scratch haijarishi alishawahi kuwa kiongozi ndani ya chama au kuwa mbunge wa jimbo.
Chama kiendelee na mikakati yake. Kama kuna vijana waliahidiwa kupeperusha bendera, waachwe wapambanie nafasi zao.
 
Aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),na msemaji wa Serikali Gerson Msigwa, ametangaza rasmi kujiondoa ndani ya CCM na kurejea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akieleza kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na masuala ya haki za binadamu, utu na demokrasia nchini.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Msigwa amesema kuwa matukio ya hivi karibuni ya ukiukwaji wa haki yaliyoripotiwa kutokea Oktoba 29, 2025, yamemfanya kufanya tafakari ya kina kuhusu msimamo wake wa kisiasa.

“Nimefikia hatua ya kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya ubinadamu. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Msigwa amesema kuwa kwa dhamira yake binafsi, ameona ni vyema kujiondoa CCM na kurejea CHADEMA ili kuendelea kushiriki katika harakati za kupigania haki, utu na demokrasia ya kweli nchini.

Katika taarifa hiyo, pia amewaomba radhi Watanzania pamoja na wanachama wa CHADEMA ambao huenda waliumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wake wa awali alipokuwa ndani ya CCM.
“Naomba radhi kwa dhati kwa wale wote walioumizwa au kukatishwa tamaa. Tulikuwa pamoja katika safari ya kutafuta haki na demokrasia ya kweli,” alisema.

Aidha, Msigwa amesisitiza kuwa pamoja na mapungufu ya kibinadamu, dhamira humtaka mtu kusimama upande wa ukweli na haki wakati wote.


 
Sio huyo mkuu Mchungaji Peter Msigwa
 
Lakini mbona uchaguzi matokeo alikubaliana nao, hakuona zile kampeni zilikuwa za chama kimoja.
 
Yericko Nyerere huyu ni wa kupigwa mawe hadi afe.
Huyo Yeriko mnamkuza pasipo sababu yoyote. Jamaa hana impact yoyote kwenye siasa za Tanzania na hakuwa na impact yoyote CHADEMA. Ni kama wale wapiga debe wa stendi unaweza kudhani ni mwenye gari kumbe mwenye gari hata hamjui. Kumpiga mawe Yeriko ni kumuonea kwa sababu ufahamu wake ni mdogo kiasi cha kutojua kifo ni nini. N kama watoto wanofurahia ubwabwa kwao wakati wa mazishi
 
Mbowe ndiye yuko nyuma ya pazia la Chaumma, mgawanyiko uliotokea baada ya Mbowe kushindwa kwenye uchaguzi Mbowe alikuwa na uwezo wa kuuzuia lakini hakufanya hivyo kwa kinyongo hivyo huyu ni adui namba mbili wa Chadema baada ya CCM.
 
Hata wale kenge waliokimbilia chauma wanatamani kurudi, ni wanasiasa washenzi wasiokuwa na msimamo wakati mgumu, when the tough time is present, stickertivity never quit, lakini wapuuzi wale walikimbia. Wangebaki bila kukihama chama wangekuwa mashujaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…