Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

Chadema itafanya kosa sana kwa kufikiri kuwa chama hicho ni cha wanachama pekee. Haijawahi na haitatokea.

Kila siku tunaona kampeni zikipitishwa cha tonetone nk, je hizi ni kwa wanachama pekee?

Kuna maelfu ya watu ndaji na nje ya nchi ambao, wanakiunga mkono kwa maduala mbalimbali, lakini sio wanachama. Hawa pia wanapaswa kusikilizwa.

Chadema itafanya kosa kama itaruhusu taasisi kukosa msimamo katika mambo muhimu. Mosi na kuu ya yote lazima kuwe na misingi ambayo kwayo hata akija au kutoka nani, itabaki ilivyo.

Haiwezekani leo mtu aseme ameamua kutoka CCM na kurejea CDM, eti kwa sababu ya matukio ya Oktoba 29. Kwa hiyo yasingekuwepo?

Kudai kuwa chama ni watu, huu ni.mtazamo potofu, ambao pia mnajikanganya wenyewe kwa kudai walioenda Chaumma, hawastahili kupokelewa! Huwezi kuwa na kila mtu katika chama chako, hata Yesu hakufanikiwa na hata leo wapo wasiokubaliana naye.
Mleta mada anasema, uwepo " utaratibu" wa kuwatimua ikiwa watabainika kufanya usaliti. Anasahau kilichotokea kwa COVid 19
Uko sahihi kwa kiasi kikubwa. Lakini i wish watu wote tusome historia ya nchi mbali mbali ya uongozi vs vyama tujifunze. Kwenye siasa ukijifanya kufuata principal sana hutoboi. Kna wakati inabidi ugeuke nyuma na kula matapishi yako ili tu kuwafanikiwa. Yes, umakini inatakiwa uwepo lakini tusiwe rigid sana na kujiapiza. Ukisoma harakati za siasaza Kenya tangu wakati wa Moi, na jinsi kila uchaguzi wanasiasa wanavyobadilisha timu ili tu kuendana na hali halisi ya wakati husika utajifunza mengi. Huyu Rig G anayemtupia mawe ya kufa mtu uto sasa hivi waligombea wote urais na makamu. Kenyatta na Ruto sasa hivi haziivi ila once upon... walikuwa timu moja.
 
Huyu anaweza kuwa hatari hata kuliko CCM. Nia yake ni kuona CHADEMA imezorota ili watu waseme bila Mbowe hakuna CHADEMA. Hata anapoona nyomi lamkutano sasa hivi anaumia sana. Ulishawahi kusikia anakemea kilichotokea 29/10? Kwangu mimi angekuwa ametokea na kukemea vikali na kusema Samia amevuka mpaka ningempa credit kubwa. Lakini hawezi kufanya hivyo kwa sababu ana deni la CCM. Alipewa fedha na akiwageuka wanaweza kumfanya kama mzee Kibao.
Alipewa b12 kumzuia Lissu asiwe mwenyekiti na akashindwa hivyi ni kweli ana deni kwa Samia.
 
Ila kwasasa ccm imedhoofika na kuparaganyika kabisa.. Kikichopo kwasasa ni makundi ya upigani sometimes yakisigina yenyewe kwa yenyewe
Mbona hiyo kawaida sana tangu enzi hizo. Ndiyo maana sisi kampeni zetu ni kuruhusiwa kwa mgombea binafsi. Hiyo ndiyo italeta mageuzi ya kweli katika nchi hii
 
Huu urejeaji wa mamuluki usikifanye chama kikateteleka na kuvuruga safa ya mashambulizi.
Tunafahamu wapo vijana na wanachama wenye msimamo thabiti ambao hawakufikiri kukihama chama licha ya kupita ktk magumu pindi hao mamuluki wakilanda landa huko walikokimbilia, sasa isije ikatokea vijana wetu wazalendo wakawekwa kando au kutengwa kisha nafasi au fursa za kugombea uongozi kupewa hawa mamuluki.
Huko kutaleta picha mbaya na ukatili.

Mamuluki waanze upya from the scratch haijarishi alishawahi kuwa kiongozi ndani ya chama au kuwa mbunge wa jimbo.
Chama kiendelee na mikakati yake. Kama kuna vijana waliahidiwa kupeperusha bendera, waachwe wapambanie nafasi zao.
Mawazo haya ni hatari na ndiyo maana wengine tunasita kuamini vyama. Hukitumikii chama ili upate madaraka, maana viongozi ni wachache na wanachama ni wengi. Uongozi ni dhamana tu. Mawazo haya ndiyo yaliyokiua chama cha mapinduzi, kikakosa mwelekeo hususan uongozi wa kupigiwa kura ulipokuwa ni ajira yenye marupurupu makubwa badala ya huduma.
 
Wewe ambaye sio msaliti, ukiwa mwanachadema una lipi la maana ulilolifanya ukiwa ndani ya chadema kuwazidi wakina Msigwa?
Unataka wote tuwe viongozi, ni mgawanyo wa majukumu, huwezi kumuona Heche au Katibu mkuu wa chama kila siku humu JF akianzisha uzi wa kukipambania chama kama Mshana Jr.

Anachofanya hapa JF ni kikubwa significant kwa chama kuliko machawa wanaosifia mauaji.
 
Unataka wote tuwe viongozi, hata anachofanya hapa JF ni kikubwa significant kwa chama kuliko machawa wanaosifia mauaji.
Sasa huoni kama unachanga hoja.. machawa na habari za kurudi chadema vina uhusiano gani
 
Kama mnavyofuatilia siasa za nchi yetu hivi sasa, kuna wimbi kubwa la wanachama waliokihama chama na kukipigia kelele nyingi za kashfa wakiondoka, lakini sasa hivi wanarudi CHADEMA kwa kasi ya ajabu.

Kama mwanachama na mdau wa mabadiliko ya dhati, naomba niwaambie hawa wanaorejea maneno machache ya ukweli mchungu bila kuwatafuna maneno.Kwanza kabisa.!

CHADEMA ni taasisi imara yenye misingi, na siyo duka la fursa za kisiasa au daraja la kupatia vyeo kwa haraka baada ya njaa kuwakamata huko mlikokuwa mmetorokea.

Tusisahau historia, kwani takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya makada waliokihama chama kati ya mwaka 2015 na 2025 kuelekea chama tawala walifanya hivyo kwa ahadi za vyeo au maslahi ya kiuchumi.

Leo hii, baada ya upepo wa kisiasa kubadilika na wengi wao kuachwa pembeni kwenye teuzi za serikali na ndani ya chama huko walikoenda, wanarudi CHADEMA kwa kasi.

Hatuwezi kugeuza chama kuwa dampo la kisiasa . Hakuna aliyerejea anayepaswa kupewa kipaumbele cha uongozi, kuteuliwa kugombea nafasi yoyote, au kupangiwa safu ya mbele kabla ya kukaa benchi na kuthibitisha uaminifu wake upya kwa muda mrefu.

Ili kuzuia usaliti mwingine wa kiitikadi, ni sharti wapitie mafunzo ya kina ya kiitikadi ili waelewe misingi ya chama ya Ulinganifu na Ustawi (Center-Right).Pili, kurejea CHADEMA kusichukuliwe kama jambo la kawaida la kisiasa;
Ni lazima wanaorejea wakiri hadharani usaliti wao na madhara makubwa waliyokiletea chama kwa kauli na vitendo vyao walipokuwa uhamishoni.

Wanachama waliovumilia dhoruba, wakitukanwa, wakifungwa magerezani, na kupoteza mali zao wakati wasaliti wakifurahia fursa katika vyama vya kidikteta, wanastahili kuombwa radhi ya dhati na ya wazi kabisa.

Waliorejea wanapaswa kuweka pembeni kiburi chao chote, washushe vitisho vyao, na wakubali kwa unyenyekevu mkubwa kuanza upya kama wanachama wa kawaida kabisa kuanzia ngazi ya msingi ya matawi.

Huwezi kuondoka ukiwa nahodha aliyetupa machela baharini, halafu ukarudi ukataka kupewa usukani wa meli mara moja!
Tatu, maneno matamu ya majukwaani, machozi ya mamba, na sifa za kishabiki hazitatosha hata kidogo kufuta majeraha makubwa ya usaliti; matendo ya kila siku ndiyo yatakayorudisha imani iliyopotea.

Historia ni mwalimu mzuri sana na inatupasa kukumbuka jinsi chama kilivyoyumba wakati wa vuguvugu la "Mamluki na Wasaliti" wa mwaka 2013/2014, na hata jinsi baadhi ya wabunge na madiwani walivyonunuliwa mchana kweupe mwaka 2017/2018 chini ya mkakati uliogharimu mamilioni ya kodi za wavuja jasho kwa kisingizio cha "kuunga mkono juhudi".

Kurudi kwa watu hawa bila kuchujwa kwa mifumo thabiti ya kiusalama (Intelligence ya Chama) ni kuwakaribisha maadui sebuleni huku tukijua wana njaa ya madaraka.

Kila anayerejea lazima aonyeshe utiifu wa asilimia mia moja kwa Katiba ya chama, miongozo, na maamuzi yote ya vikao halali vya chama.

Viongozi na mifumo ya usalama ya chama ipo macho sana sasa hivi, na jaribio lolote la kurejea kama mamluki au "pandikizi" litagundulika mapema na kushughulikiwa kwa kufukuzwa bila muhali, huruma, wala mjadala wa pili.

Mwisho kabisa wakuu, kurejea kwa waliokiacha chama kuwakumbushe wanachama watiifu umuhimu wa kulinda misingi, kushikamana, na kutovunjika moyo wakati wa dhiki kwani ukweli daima hushinda uongo na hila.

Mapokezi ya wanaorejea yaambatane na umakini mkubwa sana na tahadhari ya hali ya juu, huku macho ya kila mwanachama yakiwa wazi kulinda usalama, siri, na mikakati yote ya chama kuelekea chaguzi kuu zijazo.

CHADEMA ni salama na ni kimbilio kwa kila Mtanzania mwenye nia njema na ya kweli ya kuikomboa nchi, lakini ni moto mkali utakaomteketeza kila anayetaka kukichezea na kukitumia chama hiki kama kitega uchumi chake binafsi.View attachment 3593924
Mshana Leo umeuaaaa!!
Safi sana wakeleketwa wa chama
 
Uko sahihi kwa kiasi kikubwa. Lakini i wish watu wote tusome historia ya nchi mbali mbali ya uongozi vs vyama tujifunze. Kwenye siasa ukijifanya kufuata principal sana hutoboi. Kna wakati inabidi ugeuke nyuma na kula matapishi yako ili tu kuwafanikiwa. Yes, umakini inatakiwa uwepo lakini tusiwe rigid sana na kujiapiza. Ukisoma harakati za siasaza Kenya tangu wakati wa Moi, na jinsi kila uchaguzi wanasiasa wanavyobadilisha timu ili tu kuendana na hali halisi ya wakati husika utajifunza mengi. Huyu Rig G anayemtupia mawe ya kufa mtu uto sasa hivi waligombea wote urais na makamu. Kenyatta na Ruto sasa hivi haziivi ila once upon... walikuwa timu moja.
Tatizo vijana wanaweka hisia kwenye mambo yasiyohitaji hisia ndio maana wanaishia kuvunjika moyo.
 
Kama mnavyofuatilia siasa za nchi yetu hivi sasa, kuna wimbi kubwa la wanachama waliokihama chama na kukipigia kelele nyingi za kashfa wakiondoka, lakini sasa hivi wanarudi CHADEMA kwa kasi ya ajabu.

Kama mwanachama na mdau wa mabadiliko ya dhati, naomba niwaambie hawa wanaorejea maneno machache ya ukweli mchungu bila kuwatafuna maneno.Kwanza kabisa.!

CHADEMA ni taasisi imara yenye misingi, na siyo duka la fursa za kisiasa au daraja la kupatia vyeo kwa haraka baada ya njaa kuwakamata huko mlikokuwa mmetorokea.

Tusisahau historia, kwani takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya makada waliokihama chama kati ya mwaka 2015 na 2025 kuelekea chama tawala walifanya hivyo kwa ahadi za vyeo au maslahi ya kiuchumi.

Leo hii, baada ya upepo wa kisiasa kubadilika na wengi wao kuachwa pembeni kwenye teuzi za serikali na ndani ya chama huko walikoenda, wanarudi CHADEMA kwa kasi.

Hatuwezi kugeuza chama kuwa dampo la kisiasa . Hakuna aliyerejea anayepaswa kupewa kipaumbele cha uongozi, kuteuliwa kugombea nafasi yoyote, au kupangiwa safu ya mbele kabla ya kukaa benchi na kuthibitisha uaminifu wake upya kwa muda mrefu.

Ili kuzuia usaliti mwingine wa kiitikadi, ni sharti wapitie mafunzo ya kina ya kiitikadi ili waelewe misingi ya chama ya Ulinganifu na Ustawi (Center-Right).Pili, kurejea CHADEMA kusichukuliwe kama jambo la kawaida la kisiasa;
Ni lazima wanaorejea wakiri hadharani usaliti wao na madhara makubwa waliyokiletea chama kwa kauli na vitendo vyao walipokuwa uhamishoni.

Wanachama waliovumilia dhoruba, wakitukanwa, wakifungwa magerezani, na kupoteza mali zao wakati wasaliti wakifurahia fursa katika vyama vya kidikteta, wanastahili kuombwa radhi ya dhati na ya wazi kabisa.

Waliorejea wanapaswa kuweka pembeni kiburi chao chote, washushe vitisho vyao, na wakubali kwa unyenyekevu mkubwa kuanza upya kama wanachama wa kawaida kabisa kuanzia ngazi ya msingi ya matawi.

Huwezi kuondoka ukiwa nahodha aliyetupa machela baharini, halafu ukarudi ukataka kupewa usukani wa meli mara moja!
Tatu, maneno matamu ya majukwaani, machozi ya mamba, na sifa za kishabiki hazitatosha hata kidogo kufuta majeraha makubwa ya usaliti; matendo ya kila siku ndiyo yatakayorudisha imani iliyopotea.

Historia ni mwalimu mzuri sana na inatupasa kukumbuka jinsi chama kilivyoyumba wakati wa vuguvugu la "Mamluki na Wasaliti" wa mwaka 2013/2014, na hata jinsi baadhi ya wabunge na madiwani walivyonunuliwa mchana kweupe mwaka 2017/2018 chini ya mkakati uliogharimu mamilioni ya kodi za wavuja jasho kwa kisingizio cha "kuunga mkono juhudi".

Kurudi kwa watu hawa bila kuchujwa kwa mifumo thabiti ya kiusalama (Intelligence ya Chama) ni kuwakaribisha maadui sebuleni huku tukijua wana njaa ya madaraka.

Kila anayerejea lazima aonyeshe utiifu wa asilimia mia moja kwa Katiba ya chama, miongozo, na maamuzi yote ya vikao halali vya chama.

Viongozi na mifumo ya usalama ya chama ipo macho sana sasa hivi, na jaribio lolote la kurejea kama mamluki au "pandikizi" litagundulika mapema na kushughulikiwa kwa kufukuzwa bila muhali, huruma, wala mjadala wa pili.

Mwisho kabisa wakuu, kurejea kwa waliokiacha chama kuwakumbushe wanachama watiifu umuhimu wa kulinda misingi, kushikamana, na kutovunjika moyo wakati wa dhiki kwani ukweli daima hushinda uongo na hila.

Mapokezi ya wanaorejea yaambatane na umakini mkubwa sana na tahadhari ya hali ya juu, huku macho ya kila mwanachama yakiwa wazi kulinda usalama, siri, na mikakati yote ya chama kuelekea chaguzi kuu zijazo.

CHADEMA ni salama na ni kimbilio kwa kila Mtanzania mwenye nia njema na ya kweli ya kuikomboa nchi, lakini ni moto mkali utakaomteketeza kila anayetaka kukichezea na kukitumia chama hiki kama kitega uchumi chake binafsi.View attachment 3593924
Kwa mbwembwe na kashfa zake huyu mchungaji wakati anaondoka, wengi tukajiuliza maadili ya uchungaji wake kayaacha wapi huyu...?

Lakini tukajua tu kuwa kama ni pesa, basi kapewa furushi kubwa kwelikweli mpaka limemong'onyoa akili na ufahamu wake, likamtia kiburi na majivuno yaliyoanza kumsukumia kwenye mauti ya kuharibu kila alichokijenga kwa muda mrefu sana kwa jasho na damu akiwa CHADEMA...

Amerudi sawa. Lakini kuirejesha heshima na credibility aliyojijengea akiwa CHADEMA, itachukua muda mrefu sana unless otherwise...

Hata hivyo, binafsi, namuombea kwa Mungu Yehova amsamehe na kumpa nafasi ya pili tena...

All in all Mch Peter Msigwa aliondoka kwa mbwembwe na maneno mengi yenye karaha na kashfa akasahau kabisa methali za maonyo za wahenga wetu..

"Usitukane wakunga uzazi ungalipo"
au

"Uziwazomee mamba wakati hujauvuka mto"​

Ni wachache sana waliondoka CHADEMA kimya kimya wakitunza heshima na utu wao na ule wenzao waliowaacha...

Mfano mmoja ni aliyewahi kuwa katibu mkuu Dr Vincent Mashinji

Huyu jamaa alijiondokea kimya kimya. Inawezekana ni kwa sbb alifikia kupewa cheo cha madaraka ya uDC? uDED? (I am not sure, naweza kukumbushwa)
 
Mchungaji sijui alipatwa na kitu gani?
Alikuwa ni mjenzi mzuri wa hoja!
Sijui wakamwahidi nini mboga mboga. 😊
downloadfile.png
 
Hii ni mada huru inayohitaji hoja jadidi na hoja kinzani.. Si lazima niwe sahihi kwa asilimia 100 lakini siwezi kupungua 90

Hapa hatubishani tu bali tubabishana kwa hoja zenye kufundisha, kujenga na kufikirisha huku nyingine zikitoa Way forward kwenye mnyumbuliko wake!
Hiki ndicho kile yule wa jana alisema"wenye" akili wanataka, tunaacha kujadili msmbo muhimu na kujikita kujadili watu!

Taifa lina mazonge mengi, yanayogusa maisha yetu sote, badala ya kuyaangalia hayo, tunatolewa kwenye mstari na mtu aliyefuata" taratibu zote" kurejea kwrnye chama.

Nsshauri tuache hawa, watapita, Tanzania itasalia magofu kama sio mahandaki na sisi tutabaki na stori kama za kibibi Gagula.
Angalia Tanzania inavyorejea nyuma kwa kasi katika kila kitu, tuwaache hawa na chama chao.
 
Back
Top Bottom