Neno langu kwa wasaliti wote wanaorejea CHADEMA: Karibuni nyumbani, ila....

Wasaliti wasirudi.
Baada ya kukosa ugali huko ndo anarudi.
Toka October 29 mpaka leo ni miezi mingapi imepita?
alipewa ahadi akawa anasubiri ikageuka hewa.ndo anaamka
Ujio wa peter msigwa umekuathiri vipi wewe kama mwanachama? Ameondoa wanachama? Amevunja chama? Au tatizo ni hisia binafsi?

Kama mtu ana uwezo wa kuongeza ushawishi, kuongeza nguvu kwenye kampeni zinazoendelea, connection, mali na kuisaidia CHADEMA kufika kwa wananchi wengi zaidi, shida iko wapi?

Peter Msigwa siyo mwanachama wa kawaida kisiasa. Anaweza akatusaidia mambo mengi ya kimkati yaliyofanyika kabla na baada ya uchaguzi, ameshaijua system ya CCM, ameshajua propaganda zao, mbinu zao za kisiasa na namna wanavyocheza game ya ushawishi. Hayo mambo hayaonekani kwenye Facebook au Twitter lakini ndani ya siasa ni silaha kubwa sana

Kama kweli lengo ni kukijenga chama na kushindana kisiasa basi tunatakiwa kuangalia mtu ana value gani kwenye mapambano ya sasa tusiwe na visasi na emotions kwa wakati kama huu na tukianza kubeza kila aliyewahi kukosea hatutapata tunachotaka kukisikia kutoka kwake
 
Wanarudi kwakasi tutawapokea ila wawe tayari kukiri usaliti wao hadharani na wapitie mafunzo ya kina ya itikadi ya chama na hawawezi kukimbia wakiwa watupa machela baharini na kutaka kukabidhiwa usukani mara baaada ya kurejea baada ya usaliti..Ikipendeza chama mapokezi yao yaendane na kupewa maneno haya na wayaridhie ili wakikiuka makubaliano iwe mlango wao wakutokea kurudi kwenye usaliti wao kwa chama na Watanzania
 
Mchungaji Msigwa kapokelewa na tawi lake huko IRINGA
 
Kama mnavyofuatilia siasa za nchi yetu hivi sasa, kuna wimbi kubwa la wanachama waliokihama chama na kukipigia kelele nyingi za kashfa wakiondoka, lakini sasa hivi wanarudi CHADEMA kwa kasi ya ajabu.

Kama m
Ni wanasiasa wachache sana ambao wako chama fulani purely for ideological reasons! Wanasiasa walio wengi wana political ambitions ambazo zinawafanya wawe wasaka fursa! Mifano ipo mingi sana.
 
Mapema leo hii, Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Mhe. Boniface Jacob, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mhe. Lema wakiteta jambo na Mchungaji Msigwa huko Dodoma mjini.
 
Kilichomrejesha Msigwa Chadema ni hali yake tu ya kujikuta ametelekezwa na maccm yaliyomshawishi kukimbia mapambano. Msigwa kwa sasa hana sifa ya kuitwa Kamanda.
Msigwa bora mara 100 Halima Mdee sio Msigwa
 
Yes Mdee sawa na mimi nakuunga mkono kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…