Neno 'Mhudumu' lasababisha kifo cha mmiliki wa baa

Mbona kule Mbeya Tena jirani na Njombe, "wapiga debe" wanaitwa maafisa usafirishaji na Wewe kama msafiri unakwenda mwenyewe pale stendi?

Tumia neno, Afisa Mauzo, badala ya muhudumu, Mkuu. Huyo anayekushawishi kununua bidhaa yake Tutampa jina la Afisa Ushawishi.😊
 
Kwa nini emergency room ya hospitali ya wilaya haiko active ?

Na kwa nini Wananchi ndio waamue pa kumpeleka badala ya emergency first responders ???

Tatizo la viongozi wetu na wasomi wetu ni kwamba mmeganda kwenye fikra za u third world wa kudumu.

Swali mnalolitafutia majawabu ni "tuna survive vipi na huu u third world, tunaishije na hii hali yetu." Badala ya "tunatokaje kwenye huu u-third world."

Jawabu la emergency room ya Wilaya kutokuwa "active" sio kuwakimbiza watu wote emergency room ya mkoa, ambayo iko moja tu. Ni kuwaadabisha kikazi, na ki criminal justice kama wakiua. Na sio kuwatwika wananchi jukumu la kukimbiza wagonjwa hospitali. Tunataka ambulances zisambazwe kila mahala. How ? Cut government spending on $200,000 luxury Land Cruisers to start with.

Umeelewa wewe msomi ???
 
Hata niwe nimekaa na wakwe zangu me nazingatia pesa tu, hakuna kiwango cha dharau cha kuniita mhudumu kisha nikasirike, me naipenda pesa babu. Sema tu landa kuna jambo tumefichwa kwenye hili tukio huenda walikuwa na ugomvi wao before.
Labda wote wawili walikuwa wanamendea/wanakula mmoja wa wahudumu wa bar hiyo na mteja akawa kagundua hilo na akawa kammaindi mwenye bar hivyo akawa kamwita "mhudumu" kama kumdhalilisha. Na yawezekana pia mwenye bar alikuwa kagundua kuwa yule mteja alikuwa akimla mhudumu ambaye pia ni chakula chake. Hivyo alipoitwa "mhudumu" akaona mbaya wake sasa kafika mbali na kuamua kupambana nae na matokeo yakawa ndiyo hayo.
 
ila hasiraa za hiviii hapana aiseee yani mtu mpaka unafika nyumbani na kurudi bado una hasiraa tuuu???
jamaa alidhamiria kuua
 
Kule kusini Kuna mambo ya kishirikina sana,,,kwa upande wangu huo ni ushirikina kwa 99.8%
Mungu tu atupiganie
[emoji1431][emoji1431]
 
Yaani mimi kuitwa mhudumu na mteja wa baa yangu mwenyewe ndiyo nikagombane nae na pengine nimpoteze huyo mteja kwenye biashara yangu?
Ukiona hivyo jamaa alimuita kwa lengo la kumdhalilisha. Sio kwa lengo la kupata huduma
 
Ni kwakuwa taarifa za wanaochomwa na kupona haziripotiwi ila wanaopona ni wengi kuliko wanaokufa
 
Mteja hakosei/mfalme...ni kutojua biashara na kujivika hadhi/uboss uchwara
Mteja hakosei yule anayeheshimu biashara yako. Mteja anadharau biashara yako na wewe mwenyewe bado unamuita mteja?

Usije ukadhani sijui customer service au customer care.

Kwa title ya huyo muuaji inaonyesha kabisa ana dharau wengine kwakua amewahi kushika mkwanja
 
Utoto.Ndio hasara ya kushika pesa kwenye umri mdogo wakati huna akili Wala Maadili ya kuheshimu pesa.

Mwenye pesa unakaa Bar Hadi ucku wa manane kufanya nini?
 
Jamaa aliyemuua mwenzie ni mfanyabiashara wa Madini.
 
Yes 99% correct, assumption yako iko sawa
 
Haaa haaa haaa, haya mkuu uko sawa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…