Nesi aliyempokea Lissu Hospitalini anadai kuwa Antony Mtaka alimtukana 'Fala wewe' na akamuweka mahabusu siku tatu wakati ni Mgonjwa

Nesi aliyempokea Lissu Hospitalini anadai kuwa Antony Mtaka alimtukana 'Fala wewe' na akamuweka mahabusu siku tatu wakati ni Mgonjwa

Unisamehe ila sijui kwa nini huwa unajiona una akili ukilinganisha na members wanavyokuchukulia.
 

Attachments

  • IMG_9600.jpeg
    IMG_9600.jpeg
    166.5 KB · Views: 1
CCM hatujawahi kuunga mkono Vitendo vinavyokiuka na kuvunja haki za binadamu. CCM na wana CCM tunapenda haki nakutaka kuona kila mtanzania akitendewa haki. Ndio maana hata mwenyekiti wetu na Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia ameendelea kusisitiza na kuvisihi vyombo vya dola kama vile jeshi la polisi kutenda haki kwa watu.

Kama usemayo ni kweli tuambie yafuatayo;

Je Walotaka kumuua Lissu ni kina nani?
Je uchunguzi umeshafanyika?
Je wamechukuliwa hatua gani?
 
Kama usemayo ni kweli tuambie yafuatayo;

Je Walotaka kumuua Lissu ni kina nani?
Je uchunguzi umeshafanyika?
Je wamechukuliwa hatua gani?
Waliotaka kumuua Lissu ni watu wasiojulikana na ndio maana waliendelea kutafutwa na upelelezi kuendelea ili wahusika wajulikane na kuchukuliwa hatua. Uchunguzi unaendelea maana jinai haifi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeendelea kuisikiliza video ya muuguzi aliyedai kuwa ni miongoni mwa wauguzi waliompokea Lissu hospitalini siku alipokimbiziwa hapo baada ya kushambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana 2017.

Ambapo katika mazungumzo hayo na Lissu muuguzi huyo ambaye anadai alishafukuzwa kazi kwa madai ya utoro kazini .anasema kuwa siku ya sheria Dunia mwaka 2022 aliingilia hotuba ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hasssan ili aweze kusikilizwa .ambapo hata hivyo muuguzi huyo anadai ya kuwa Rais aliamuru aende kwa wasaidizi wake ili wamchukue maelezo na wao watayawasilisha kwake.

Ambapo baada ya kuwa amekaa kwenye gari pale chini kwa ajili ya kusikilizwa ,anadai kuwa aliitwa mkuu wa mkoa wa Dodoma wa wakati huo Mheshimiwa Antony Mtaka ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Njombe,ambapo muuguzi huyo anadai ya kuwa baada ya Mheshimiwa Mtaka kuja alimtukana kwa kumwambia FALA WEWE. Ambapo muuguzi huyo anasema akasema yeye siyo fala na kwamba amefanya hivyo kwa kuwa amekuwa hasikilizwi. Anasema akamwambia Mheshimiwa Mtaka kuwa hata wewe utaondoka hapa yaani Dodoma.

Ameendelea kueleza kuwa alitoa maelezo kwa wasaidizi wa Mheshimiwa Rais ambapo anaamini pengine ni katika maelezo yake yale ndio maana Mheshimiwa Mtaka alipewa kama adhabu kwa kupelekwa mkoani Njombe. Ameendelea kusema kuwa Mheshimiwa Mtaka alimuweka central police kwa Amri kwa siku tatu wakati alikuwa anaumwa na kwa muda wote huo hakupewa dawa wala maji na kuendelea kupata maumivu makali sana Mwilini mwake yaliyotokana na kukosa dawa alizokuwa anazitumia kwa wakati huo.

Hoja yangu mimi ni kuwa hoja na tuhuma hii ni nzito sana ,kwa kuwa Mheshimiwa Mtaka amejijengea heshima kubwa sana hapa nchini juu ya utendaji wake ambao umejengwa katika taswira ya uchapa kazi.ambapo amekuwa akipongezwa na kusifiwa na viongozi wengi sana pamoja na wananchi mbalimbali nikiwepo mimi mwenyewe Mwashambwa Lucas mwanachama na kada kindaki ndaki wa CCM.

Kwa sababu inamchafua sana Mh Mtaka hasa kwa namna jina lake lilivyo kubwa miongoni mwa wakuu wa mikoa waliopo hapa nchini. Maana hata leo ukimwambia mtu akutajie wakuu wa mikoa walau watatu tu wachapa kazi ,basi jina la Mh Mtaka lazima litakuwepo. Sasa siamini kama Mheshimiwa Mtaka anaweza kuacha na kushindwa kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kwenda kumsikiliza mwananchi mwenye shida ili apatiwe majibu , na badala yake Mh Mtaka aende kumtukana huyo mwananchi kuwa ni FALA. Jambo ambalo naamini si sahihi kwa sababu hata fala anayo nafasi ya kusikilizwa katika ufala wake. Maana katika ufala wake kunaweza kukawa na maumivu katikati yake yanayohitaji msaada.

Najuwa kuwa kiongozi huwezi ukajibu kila kitu kinachotokea na kuendelea mitandaoni,najuwa siyo kila jambo linaloibuliwa mitandaoni linaweza kuwa la kweli. Lakini katika hili jambo zito la tuhuma tena ambalo lilitolewa maagizo na Mheshimiwa Rais natamani Mheshimiwa Mtaka angelitolea hata majibu kidogo tu hata kupitia mtandao wake wa kijamii kama vile kupitia twitter au njia yoyote ile. japo tamaa yangu siyo lazima kutimizwa au kupata majibu au kujibiwa.maana inategemea na mhusika atakavyojisikia na kulichukulia jambo hili. Maana hata kukaa kimya nako ni jibu na ni haki ya mtu na sehemu ya mbinu za kiuongozi na kuwa kama kiongozi siyo lazima uzungumze kila kitu na kutolea ufafanuzi kwa kila kitu.

Lakini pia suala la kupelekwa Njombe ningependa kusema kuwa ni jambo la kawaida katika utumishi wa umma au uongozi.maana hata Njombe ni sehemu ya Tanzania na ina watanzania wanaohitaji viongozi bora na wachapa kazi ili kuinua mkoa huo. na siyo kwamba ni mkoa wa kutumikia adhabu kwa wenye makosa na wala siyo Magereza ya viongozi waliotenda makosa sehemu nyingine za utumishi wao.. Kwa hiyo hoja ya kupelekwa Njombe siichukulii kama hoja ya msingi au adhabu bali naichukulia kama mabadiliko ya kawaida tu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Time will reveal the truth
 
Utakuwa humjui Anthony Mtaka, hawezi kupata muda wa kujibu vitu vidogo hivi!. Kwa tunaomjua Mtaka, tunajua Mtaka hawezi kumtukana mtu yeyote!.
Kwa kifupi, mtu kama huyu
View: https://youtu.be/Ed7c9aEw8-Y?si=RcVTCoB_eom6d54C ataanzia wapi kumtukana mtu?.

View: https://youtu.be/bKobi1sGjQ4?si=0Qh3vJg7hWbFQdqv

View: https://youtu.be/sOv_cJSC9As?si=_QRpMw_Rp1rh8C5h

View: https://youtu.be/-f10kAUh7ik?si=h-eJ70koa8_PUcQ9
P

Paschal nakuheshimu sana lakini hii hoja umeijibu KICHAWA CHAWA SANA huu siyo ubongo wako, huyo unaedhan hawezi tukana wengine tumefanya nae kazi wala hayupo hivyo na hata upigaji ni fundi mzuri sana, viongozi wote waliokuwa wameshirikishwa kwenye Verse ya kumuua Lissu hakuna aliyekuwa na akili zaidi ya kumfurahisha yule aliyetangulia kuzimu. Hivyo Paschal utakuja jiweka ktk wakati mgumu unapomchukulia mpigaji kama wapigaji wengine kuwa ni malaika
 
Nilichojifunza kuwa Njombe sio.. sehemu ya kuishi mtu na hadhi zako.. hii inatokana na Mtaka kutolewa Dodoma na kupeleka Njombe ilikuwa ni adhabu kwa kiongozi huyo
 
Acha dhihaka zako ndugu yangu. Kwani ni nani ambaye hatakufa hapa Duniani. Ni nani wa kuishi milele.
Wapi nimesema kuna mtu anaishi milele? Mimi nimetoa angalizo kuwa unapotenda maovu kwa watu ukumbuke kuwa kuna kifo. Ni mawazo yako finyu yaliyogubikwa na uchawa tu ndiyo yamekupa tafsiri potofu ya post yangu. Na usijione kwa ukada wako uchwara wa CCM basi unayo hati miliki ya fikra za watu wote walio kinyume na CCM yako. Ukitenda mabaya kumbuka kuna Jehannam
 
Nilichojifunza kuwa Njombe sio.. sehemu ya kuishi mtu na hadhi zako.. hii inatokana na Mtaka kutolewa Dodoma na kupeleka Njombe ilikuwa ni adhabu kwa kiongozi huyo
Nani kwakwambia kuwa alipelekwa Njombe kama adhabu? Kwani Njombe siyo Tanzania? Hakuna watanzania wanaoishi kule? Njombe hawalipi kodi?
 
Utakuwa humjui Anthony Mtaka, hawezi kupata muda wa kujibu vitu vidogo hivi!. Kwa tunaomjua Mtaka, tunajua Mtaka hawezi kumtukana mtu yeyote!.
Kwa kifupi, mtu kama huyu
View: https://youtu.be/Ed7c9aEw8-Y?si=RcVTCoB_eom6d54C ataanzia wapi kumtukana mtu?.

View: https://youtu.be/bKobi1sGjQ4?si=0Qh3vJg7hWbFQdqv

View: https://youtu.be/sOv_cJSC9As?si=_QRpMw_Rp1rh8C5h

View: https://youtu.be/-f10kAUh7ik?si=h-eJ70koa8_PUcQ9
P

Mkuu, mayala sijataka kusikiliza crp hizo ,lakini offkamera viongozi hawa wahovyo sana ,tafadhari tusubirie akipandishwa kizimbani
 
Back
Top Bottom