New Bilionea in town aliyebuni mfumo wa kununua umeme unaoingia moja kwa moja

Idea yake ashaiimpliment na kawanunulia XXL pale luku ikaingia na anakwambia haijalishi kokote atakapokuwa ilimradi umenunua luku inaingia.
Kama ameshawahi kuwanunulia XXL luku ikaingia moja kwa moja, aliwezaje? Maana hizi mambo mpaka upate codes kutoka kwa mwenye service ya kukuwezesha kufanya ivo. Na kama alipewa hizo codes, sioni sababu ya kuilalamikia Tanesco, bali alitakiwa awe na app na atoze % yake kwenye manunuzi ya umeme.
 
Kama ulikua kwenye akili yangu wazo lake liko complicated sana kwenye utekelezaji
 
Hujanielewa siku hizi watu wengi hawanunui mawazo wananunua kitu ambacho walau umetenkgeneza proto type, kuna mtu nimemwamvia hapo juu kuwa wazo la mpesa master card tulikuwa nalo toka mwaka 2012 tukajaribu wapa tigo na voda wakazinua, ikabidi nimtafute Kelvin Twisa. Alichoniambia ni kwamba siku hizi mawazo hayauzwi maana kila mtu ana mawazo, tutengeneze prototype ya wazo halafu nimtafute.
Kuna jamaa flani ana system ya kufanya malipo kwenye supermarkets kenya nikamchek tatizo likaja anataka ile kitu iwe chini ya kampuni yake wakati sisi tulikuwa na kampuni yetu, coders wakata ela nyingi tukafail hapo.
Sasa huyu siyo wazo bali anacho kitu tayari alichoshatengeneza. Inawezekana siyo kitu kipya labda kuna mtu mwingine ashataengneza ila inawezekana mechanism ya kufikia lengo zikawa tofauti.
Mfano kuna curved screen, miaka kadhaa nyuma nadani mitano apple alifile patent ya curve screen, ila mechanism ya implimentantion ya kitu alichofile ni tofauti na cha samsung ila mwisho wa siku ni curved screen.
 
Dogo anaweza pigwa na uhujumu uchumi kimchezo mchezo......
na hv ameanika ushahidi xxl
 

Twitter juzi alivyoreta mtumiaji kuweza kutuma Podcast kule Twitter kuna jamaa nyuma hapo eti alikuwa na Idea kama hiyo basi wale wanajiita ma-Founder wa Silicon Dar walipiga kelele sana kule Twitter kumbe haya mambo unakuta kampuni ina mpango mzima wa teknolojia zote kwamba hii tuta ifanya muda huu hii muda huu sasa wewe kichwa maji ukiwaza kwanini FB wasiweke kitu hiki unaona kama wewe ndio ewaza dunia nzima kumbe mambo yapo kwenye timeline tu.
 
Mkuu naona umeanza sasa kufikiri Critical sasa twende sambamba kwahiyo unataka dogo asaidiwe vipi na Tanesco? Kama upo dar au Arusha tembelea ivo vyuo vya ufundi uone final year student wanafanya nini izo project zipo inshu ni budget unategemea tanesco aingie cost kubwa bila kujiandaa ya kuweka hardware kwenye meter zote nchini ili tu watu wananunue umeme directly na uingie? Unataka akurupuke tu sio kisa dogo amekuja na unachoita innovation
 
Hajawaza ana implimentantion ya kitu hicho kama kuwaza mbona hata mimi nilishwaza mara kadhaa kwanini kusiwepo na hiyo huduma
 
Hakuna chuki bana hizo ni criticism za kawaida..
 
Huyo sio mbunifu.
Kwanini siyo mbunifu? Kaona waokijijini ni wakulima, kaona wanahangaika kutumia jembe la mkono akaamua kutengeneza trekta na muda huo wanamhoji wananchi walikuwa wanarekodisha linalima sasa kwanini useme siyo mbunifu? Ubunifu ni kutatua matatizo yaliyo kuzunguka.
 
Ukiwa na wazo Inatakiwa ujaribu hata kugoogle uone Kama Kuna mtu mwingine amefanya utagundua mawazo mengi watu walijaribu kufanya na walifail wapi.

Tatizo la vijana wengi wanaibuka na wazo hawalifanyii literature review alafu Wana taka support mambo hayaendi hivyo
 
Tofautisha ubunifu na "assembling". Huyo kijana ndio kafanya ubunifu.
Ka assemble nini sasa? mtu kachomelea katengeneza fram ya trakta, kafunga engine na kila kitu ni mbunifu
 
Tuna penda shortcut
 
Hapo utakuta tanesco badala wampe dogo nafasi wao wamewaagiza mafundi wao kutafuta maujanja anayotumia dogo wamalize kazi wenyewe 🀣
 
Hio project ipo complicated sana sio rahisi Kama watu wanavyofikiri

Sijakataa kwani hamna mtu alianza huku ana kimbia,hivi ni vipaji vyetu na hawa ni watu wetu lazima tuwasupport na tuchochee haya maswala haya ubunifu.


Mimi hawa madogo walienda Tanesco majibu waliopewa waliwakata maini kabisa wakawa hawana hamu hata ya kufanya hiyo projects yenyewe.

Dunia sasa hivi kila mtu anatengeneza na kusupport watu wake kwa ajili ya security ya mifumo yao,sasa wewe usipo support watu wako watakuwaje wabunifu.

Hizi teknolojia za wenzetu tunazo zitumia zinatuweka uchi,mbele ya nchi zilizo endelea,hivi hivi kwa udogo wetu kama tuki intergrate na kusupportiana mawazo yetu tutafika mbali.
 
Madogo kama hao ndio wanahangaika, wanakwenda ughaibuni, wanaanzisha vitu vyao huko, kwa michango ya wawekezaji wa nje, halafu wakitengeneza kitu kinatambuliwa dunia nzima ndiyo tunaanza kuwashobokea "dogo Mtanzania huyu".

Wakati yuko Bongo watu wanampiga danadana.

Marekani kwa mfano wanatafutwa watu wenye akili za innovation waanzishe startups.

Wakija Wamarekani wakamchukua huyo, utasikia watu wanalalamika brain drain, Wamarekani wanakuja kuchukua vipaji vyetu kwetu.

Wakati sisi wenyewe hatuvithamini.
 
Kitu ambacho aelewi kwenye teknologia, mfano gharama ya kutengeneza bidhaa inaweza ikawa kubwa sana hapa Tanzania, alafu ikawa ndogo ku-import ndo maana watu Wana prefer ku-import kwa sababu ya gharama ndogo
 
Hivi tabia ya kuja usiku wa manene walifundishwa na gamboshi gani?

Unareport tatizo asubuhi,yakijisikia yanakuja usiku mnene watu tumelala na wake zetu unasikia yanapiga hodi kwa fujo unaweza hisi umevamiwa.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Asante sana mkuu, leo kuna uzi huko nimeongea kuwa kiumbe cheusi kina roho mbaya sana duniani, watu wakanishambulia sana!! Lakini ukweli utabaki vile vile!!!
Matatizo ya ujinga na unasikini tusiyaunganishe na ngozi ya mtu.

Oprah Winfrey mtu mweusi lakini mbona kagawa magari kama pipi kwenye shiw yake,na mpaka kesho anaongoza kwenye chati za matajiri?

Mbona kuna watu weupe kibao wana roho mbaya na ni masikini?

Tuache kulundika matatizo yanayotokana na historia ndefu ya ujinga na umasikini kuwa ni matatizo yanayotokana na ngozi ya mtu.

Mbona watu weusi wengine tunasaidiana poa tu,tena tunasaidia watu hata si ndugu zetu? Kwa imani ya utu tu.

Kama weusi unaendana na roho mbaya na ubinafsi na ujinga, sisi wengine tumeepuka vipi kuwa hivyo wakati bado ni weusi kama weusi wengine tu?
 
100% upo sawa.πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…