New Bilionea in town aliyebuni mfumo wa kununua umeme unaoingia moja kwa moja

Ni Solution inayphitaji Smart meters (Luku) ambayo lazima iwe Online.
Na pia inahitaji Core Billing System ya kuwasiliana na Luku zote na ku update.
Similar to how Charges & Re charges works on mobile or fixed Networks.
Huyo dogo Muuza Chai tu ndio Maana Tanesco wamefukuzilia Mbali
 
Ndugu ufundi wa namna hiyo kila fundi baiskeli anaujua na kuuweza.
Kila fundi baiskeli anaweza chukua engine ya pikipiki akatengeneza frame, akaitengeneza iweze kushusha jembe ilimbe, izalishe umeme, upukuchue mahindi tena kwa kuendeshwa?
 
Exactly-Hizo ni internet of things applications ni kitu ambacho watu wengi hawaelewi

Mfano sahivi Kuna smart meter za maji, mtu hawezi kuja na kusema ni ubunifu
 
100% upo sawa.👏🏻👏🏻👏🏻
Watanzania tunapenda ready made. Yani mtu akihustle ukamsikia yuko nje mfano anacheza mpira utasikia yule baba yake mtanzania wakati akiwa hapa utasikia kile kipaji cha kawaida hata watoto wa mchangani wanaweza.
Hapa namwambia jamaa kuna mzee alitumia engine ya pikipiki katengeneza frame ya trekta akatengeneza jembe linashuka linalima inafua umeme inapukuchua mahindi. anasema eti hana ubunifu aliuna una tu na kila fundi baiskeli anaweza kufanya ivyo.
 
Mtanzania kumkubali Mtanzania mwenzake ni kazi,hapo ndio umewapelekea idea yako alafu ndio unakutana na wazee wanakuponda na utawasikia "kusoma tumesoma sisi nyinyi mnacheza tu siku hizi........".

Ndio nchi yetu hii sijui itabadilika lini.
 
Mtanzania kumkubali Mtanzania mwenzake ni kazi,hapo ndio umewapelekea idea yako alafu ndio unakutana na wazee wanakuponda na utawasikia "kusoma tumesoma sisi nyinyi mnacheza tu siku hizi........".

Ndio nchi yetu hii sijui itabadilika lini.
Aisee sasa nimeanza kuelewa kwanini watu wanaandaa mashindano ya Bongo Star Search na maigizo na wala siyo mashindano ya ubunifu
 
Ye kasema inatengemea na aina ya mita anaweza kia ttach aau akakifunga ndani.
Nadhani baadae itajulikana inafanyaje kazi
Andiko lako liko ki-layman sana bahati nzuri umeishakiri kuwa hujui.
Usipende kuongelea mambo magumu ambayo huna taaluma nayo.
 
Andiko lako liko ki-layman sana bahati nzuri umeishakiri kuwa hujui.
Usipende kuongelea mambo magumu ambayo huna taaluma nayo.
Nimeongea au nimetoa taarifa. Wewe kila unachotoa taarifa una details nayo? Mimi nimetoa taarifa kamanilivyoisikia na ndiyo maana sijaongelea mfumo wake na mechanism yake inavyofanya kazi maana hata yeye mwenyewe hajasema.
 

Mbona taasisi ipo mkuu. Inaitwa COSTECH maeneo ya Kijitonyama. Wapo pale wanakula mishahara na kuendesha gari za serikali. Hawana habari.
 
Kwahiyo unaamini media kubwa kama clouds inaweza tumika kupotosha? Unajua faini watakayopigwa clouds kwa kupotosha jamii?
 
Ingawa taarifa haijazama ndani kiufundi, lakini nampa 'bigup huyo mbunifu kwa kuthubutu. Kwani kisayansi tunasema kila tokeo la kiubunifu huachia 'gap' la kuendelela ubunifu zaidi. Hivyo hata hao waliotengeneza hizo mita wanatarajia some criticism kutoka nje ambazo zitaimarisha wazo lao la awali. Bigup propriator!
 
Kwahiyo unaamini media kubwa kama clouds inaweza tumika kupotosha? Unajua faini watakayopigwa clouds kwa kupotosha jamii?
TCRA inaingia kama upotoshaji una dhuru wananchi directly..

Ila huu ni uongo wa binafsi wa kujitafutia umaarufu
 
Mkuu

Kuna uongo mwingi somewhere...

Uzuri ni huyo bwana aje humu aulizwe maswali ajibu yeye kama yeye

Hapa tunasikia kwa third parties!
Aje kwani anashida na nyie? Aliokuwa na shida nao kawafata
 
Hakuna jinsi ya ku-modfy hizo luku?
 
Akili mavi hizi
 
Hate or get inspired.....mkuu mbona kama umepata wivu kwa uvumbuzi wa kijana
Naona huu Uzi umejaa ma-layman lukuki na mmojawapo ni wewe.
Jaribu kusoma comments za members wenye hoja nzito za kitaalamu kuhusu manunuzi ya umeme ktk mita za LUKU.
Umeambiwa kuwa hii technology ambayo dogo anasema kavumbua ipo siku nyingi na TANESCO wanajua hilo.
Kwamba dogo kafunga kifaa fulani ndani ya mita, huu ni uwongo mtupu!
Kwamba ni gharama sana ku-install system ya kuingiza umeme wa LUKU moja kwa moja ktk mita ya umeme.
Sasa kosa la TANESCO ni nini basi?
Watu wapovu yametamalaki, mara oooh, wivu, roho mbaya...!
Comments nyingi zinazohusu kuonewa kwa huyu dogo zinatoka kwa watu wasioelewa vizuri mfumo wa LUKU unavyofanya kazi.
 
Hicho kitu kipo kwenye baadhi ya mita za 3phase......na tanesco huwa wanaingiza huo umeme remotely for some cases......na hii ni kwa sababu hizo mita ni smart meters na zina mfumo wa moderm pamoja na chip......lakin hizi mita nyingine za kawaida hasa za majumbani haiwezekan.......kama dogo anasema kaweza ni uongo labda apite kwenye mita mojamoja aongeze baadhi ya vitu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…