Ngoja mtoto wako afike adolescent age (foolish age) ndio utaukumbuka umuhimu wa shule za Kayumba

Sawa
 
Umeana vzuri sana kuhusu watoto wa Isaachar...napenda sana kusoma masuala ya ujasusi
 
Hakuna atakayepingwa hapa. Kila mzazi anataka watoto wake WAPANCHI.
Iwe kayumba au private...ila kwenye dunia yangu nimewashuhudia WAKAYUMBA MJINI DAR WAKIPASUA MAISHA ZAIDI KULIKO PRIVATE..
Sielewe kwanini ila WANAWA DISSAPOINT wazazi wao mpaka unawasikitia
 
This is what am talking about here bro lakini wengi hawawezi kuelewa.
 
Sasa mkuu kama wewe ulipata mtoto wa kwanza ukiwa na miaka 15 na ulisoma kayumba. Huoni kuwa points zako zote huko mbele zinakua invalid
Ur very slow bro . Am so sorry to tell you this.
 
Hao watoto manaowasomesha english media na kuwaona kayumba hawana wanalofanya .....wote wanakutana kitaaa ,,,kwenye elimu Dunia ........
Hata mimi naona bora apate msingi wa medium ila sekondari aende kayumba tu hzo hela bora tuwekeze akimaliza ahule apate pakuanzia maana kuna shida ya ajira
 

Unapoongelea familia basi mawazo yangu Moja Kwa Moja huangalia jamii kama za wahamiaji au conservatives .

WaAsia wakiwa nnje ya Asia au mataifa mengine,Kuna spirit wanakuwanayo ,Kwani unapokuwa ugenini so jamii zao ndio nguvu yao na watoto wao tokea wadogo wanalelewa kuandaliwa kuendeleza wazazi walicho anzisha.,wahindi waarabu tunaona ,elimu kwao sio madarasa ,shule au academia Bali generational wealth kwani wako ktk kisiwa na jamii iliyowazunguka ni tofauti na Yao.
Waarabu wao wengi katika biashara na usafirishaji ,hawa watoto wanashinda gereji Kwa baba,mjomba au rafiki wa familia .
Wahindi biashara na uzalishaji,hawa watoto wanashinda dukani,gereji na watoto hufanywa mabosi kisimamia japo hawa uwezo ilikuwaanda kuwa mabosi baadae
Sasa turudi Kwa sisi wa utumishi wa umma , watoto wetu wanashiriki vipi ktk kuangalia maamuzi ya kifamilia practically.
Kifupi hakuna bond kati ya wazazi na watoto, pia hakuna utamaduni wa community sababu tuko nchini kwetu.,zaidi labda Mipira na Siasa ambazo SI community za kusaidiana Bali pastime.
Wewe kama mzazi wanao wanashiriki vipi ktk mambo Yako ya kupata rikzi hata kushinda nao ofisi ya serikali kama kina ridhiwani au wewe kulipa ada unaona ndio umemaliza.
Shule iwe kama icing on the cake kama tunakata generational wealth na watoto watusaidia baadae.
 
So whats your stand katika hilo la kusomesha umeandika mengi na umegusia vitu vingi ila hujatupa coclussion yako kwenye huo uzi iliopo kwenye fiscution..........
 
Cha msingi tutafute hela ili tupunguze malalamiko. Ukimsikiliza mleta mada vizuri ni kwamba kaenda kayumba kwasababu ya uchumi kuyumba. Na ninaona kama vile anachanganya elimu ya darasani na stadi za maisha. Cku zote kumbuka binadamu yupo kutokana na alichokikuta. Cc tumeprogramiwa mzee. Tuko kama tulivyowakuta watu wapo. So wewe nafikiri umeshindwa kusema wazazi tuwe karibu na watoto ili wajifunze stadi za maisha kutoka kwetu. Hayo yoote unayosema kama hakuna msukumo wa wazazi ni kazi bure. Kumbuka elimu inahtaji watoto wenye shauku ya kutimiza ndoto zao+ wazazi wenye moyo na waliojitolea kuwasaidia kuzifikia na walimu wenye bidii katika kuwasaidia. Mtoto wako ni copy yako na ukitaka mafanikio yako yaende vizazi na vizazi hakika kuwa na mwanao ajue how things work. Hapa ndipo wahind walipotuacha . Mi wanangu tangu wakiwa nursery ni privet mwanzo mwisho. Mkubwa ndio anamalizia chuo mwaka huu Winperg Canada. Na huyu jamaa kwa namna nilivyomseti yeye ndie anashughulikia mambo yote ya wadogo zake kuhusu elimu nk. Mdogo wake alimaliza six mwaka jana na jamaa ndie kamtafutia chuo uingereza mi nikuhakiki na kulipia tu. Sasa hiv wanagroup lao wako wanne. Wameelekezana kila mtu asomee nini ili waje kuanzisha kampuni yao. NInataka kusema nini. Watoto ni wewe sio shule. Shule wanaenda kuongeza kile ulichowafundisha kwa mapana zaid. Sorry kwa gazet
 
Usisahau kuna kurogwa pia mkuu
 
watanzania wote wana bet mkuu
Mkuu tunaishi na walimu wa shule hizi za kayumba. Tunawaona. Kifupi sana na kwa msisitizo inategemea na shule ipi ya kayumba unayompeleka mtoto. Si kila shule mkuu.
Na kwa dunia ya sasa ni heri mtoto akapata foundation nzuri kidogo mwanzoni kindergarten na primary huko juu kuanzia secondary atakuwa keshakuwa angalau kujua baya na zuri. Kuanzia kidumu ufagio toka chini ni risk sana kwa mtoto siku hizi.
Mimi naplan mtoto wangu asome English medium kindergarten then nimpeleke diamond au Olimpio Primary nikikosa angalau Maktaba, Bunge, Muhimbili, Mlimani basi lakini sio hizi takataka zingine
 
Two things
1)Kuhusu wana wa Isakari natamani ulete upya uzi wao tujifunze mengi.

2)Kuhusu Back to Kayumba, ningependa mazingira yaboreshwe kwanza. Kuna watoto wengi wamejifunza tabia ovu huko Kayumba. Imagine darasa la mjini lina wanafunzi 100+ ,hakuna muda wa kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja.

Vinginevyo shule za binafsi zinapendwa kwa sababu ya lugha na Siyo vinginevyo.
 
1. Ntakuja kuleta Uzi hapa kuhusu wana wa Isachar.

2. Upo sahihi. Kuhusu hilo la watoto wengi nitakuja na Uzi wa kuelezea FAIDA zake plus hasara za mtoto kusoma kwenye darasa lenye watoto wachache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…