Ngoja mtoto wako afike adolescent age (foolish age) ndio utaukumbuka umuhimu wa shule za Kayumba

Umeongea ukweli mchungu sana
Kijana wangu nimehangaishana nae mpk alipofikia si haba.
Ila kazi niliyojua itakua yake na alipewa offer ya ajira alipomaliza masomo headquater kakataa.
Ni likampuni kuubwa duniani kiasi hata hapo bongo wana branch yao.
Alinikata maini mpk basi.
Kazi anayofanya sasa!
Namwangalia napata wazimu ila poa tu atajua nilichokua naongea badae.

Kakataa
Je, Mwanao Hali yake hiyo imesababishwa na kusome English Medium?
Kuna any connection?
Kwamba watoto wakisoma Kayumba hiyo age ya Balehe haiwasumbui ?
 
Biblia inasema Mungu aliwapenda sana wana Isachar ( sio Isaka ni ISACHAR: Huyu Isachar alikuwa ni kati ya watoto 12 wa Yakobo. Sasa huyu Isachar alikuwa na watoto wa kiume 200 ndio hao ambao ninawazungumzia.

Biblia inasema Mungu alipendezwa sana na wana wa Isachar.

Sababu kuu iliyo mfanya Mungu apendezwe na wana Isachar utaikuta kwenye kitabu cha 1 Chronicles 12:32.

They knew what Israel had to do and at what time and how to do it.

Kwa ufupi hawa wana wa Isachar walikuwa ni majasusi.

JASUSI ni mtu anae jua kitu gani kinatakiwa kufanywa na wakati gani na kwa namna gani.

JASUSI anajua yote hayo sio kwa kupitia uchawi bali ni kupitia sanaa ya kutafuta na kuku sanya taarifa (the art of intelligence gathering) kuchakata taarifa (the art of intelligence processing) kuandika ripoti ya kitaalamu kupitia taarifa zilizo kusanywa na kuchakatwa ( the art of intelligence report) na kuifanyia kazi ripoti hiyo (the art of intelligence execution) .

Kikubwa zaidi ni kujua wakati gani muafaka wa ku -execute hizo taarifa.

Wana wa Isachar walikuwa ndio the brain behind King David's victory in all wars and battles which he fought.

Kwa wasio jua, His Majesty King David, the King of the United Kingdoms of Israel and Judah, ndio mfalme ambae hajawahi kushindwa vita yoyote ile katika utawala wake. Huduma ya ujasusi kutoka kwa wana wa Isachar ilikuwa ni sababu kuu mfalme Daud alishinda vita zake zote.

Mfalme Daudi alikuwa na intelligence madhubuti sana. (Nenda kasome kitabu " Rise and Kill First: The secret history of Israel's Targetted Assasinations " kilicho andikwa na Investigative Journalist na JASUSI wa kiyahudi aitwae Ronen Bergman ili uweze kujua wana wa Isachar ni watu wa namna gani katika dunia ya sasa)

The reason why King David acted strangely during Absalom Rebellion was because of the advice he was given by the children of Isachar. At the end of the day King David secured the victory without even putting a fight. All this ni kwa sababu ya kuzungukwa na wabobezi wa ujasusi.

Binafsi tangu nifahamu kuhusu siri hii ya wana wa Isachar nimekuwa nikiitumia hadi kwenye vitu vya kawaida kabisa kwenye maisha yangu.

Hata michepuko wangu huwa nawafanyia ujasusi kabla ya kuwapa " zawadi" ya kuwa nao kimapenzi. Kila mwanamke ana file na dawati lake. Mfano " Fatuma's desk" ( Dawati la Fatuma: dawati maalumu la ku dili na masuala yote yanayo muhusu Fatuma. Humo kuna mafaili yenye taarifa zote kuhusu Fatuma plus what when and how to act when dealing with Fatuma). The same to my children. Kila mtoto ana dawati lake.

BACK to my topic . Wazazi wengi wa miaka hii ya elfu 2 ambao ndio kina sisi tulio zaliwa miaka ya themanini katikati na mwishoni ( themanini mwanzoni na 70 mwishoni) plus miaka ya tisini mwanzoni, kwenye mindset zetu hatunaga image ya mtoto ambae yupo kwenye adolescent age ( teen age / foolish age) When it comes to children, wengi wetu huwaga tuna picha ya yule mtoto wa mwaka 0 mpaka 9 au 12 n.a. 13 hapo. Mtoto ambae bado ni mtiifu kwa almost kila kitu. Mtoto anaeweza kudhibitiwa hata kwa fimbo etc.

Wengi wetu huwaga hatujiandai kisaikojia kukabiliana na changamoto za mtoto alie balehe. Huwaga tunadhani mtoto ataendelea kuwa " Mtoto " hivyo hivyo maisha yake yote..

Utamsikia mtu anasema " namlipia mamilioni mtoto wangu shule hii ya English Medium kwa sababu hapa wanafaulisha vizuri. So nataka afaulu vizuri hapa then aende O level then A level then Chuo the apate kazi yake nzuri"

Mawazo kama hayo [emoji115] anasema Robert Kiyosaki kwenye kitabu " Poor Dad Rich Dad " yalikuwa valid kuanzia mwaka 1985 kushuka chini and not after that. Sasa hivi dunia imebadilika ( kumbuka hiyo ilikuwa mwaka 97 mzee ) Sasa hivi ni 2023 dunia imebadilika zaidi. Mfumo wa maisha ya dunia ya sasa umebadilika juu chini kama ulivyo badilika pale Eden baada ya Adam na Hawa Kula tunda la mti ule ulio katazwa...

Wakati wewe mzazi unahangaika kulipa mamilioni ili mtoto wako awe injinia, mwanasheria au daktari kumbe mwenzako anawaza kufanya kitu tofauti kabisa na wewe. Anataka kuwa kama Mzize, Zuchu au Gigy Money

Ndo maana nasema no matter how much money u put on ur children when they are young, when they grow up they will branch out.

Kwa wewe mzazi ambae una watoto wadogo ambao ni watiifu kwako at this moment fanya yote unayo fanya lakini jua kwamba wakifika adolescent age wata branch out. Watakuwa tofauti kabisa na unavyo tarajia..

Mimi namshukuru Mungu nimeujua huu ukweli tangu nikiwa mdogo kwa sababu Nimepata watoto nikiwa mtoto.

Nimesex ( kikubwa kubwa achilia zile za utotoni za kufanya kinguo nguo au kichupi chupi) kwa mara ya kwanza tareje 18 November 2000 nikiwa kidato cha pili najiandaa kuingia form three. I was 15 years old and she was 15 years old too. Tuliendelea na kamchezo Ketu mpaka demu akapata ujauzito nikapata mtoto wa kwanza wa kike nikiwa nna miaka.16 ( 2001) ( kumbuka jambo hili ni kinyume kabisa na maadili ya familia yetu Nimetoka kwenye familia inayo swali)

Mwaka 2003 nikiwa nna miaka 18 nikapata mtoto mwingine wa kike kwa mwanamke mwingine.

Hawa wote walisoma Kayumba.

Mwaka 2007 nikapata mtoto mwingine wa kike kwa mwanamke mwingine. Huyu alinikuta tayari nna vihela hela nikampeleka English Medium kuanzia la kwanza hadi la saba. N.a. private school kuanzia form one hadi form four.

2015 n.a. 17 nikapata watoto wawili wa kiume kwa mwanamke mmoja.

Huyu wa 2001 now yupo chuo mwaka wa mwisho ( she is very smart and very disciplined. )

Huyu wa 2003 yupo Chuo mwaka wa kwanza. She is very smart and very disciplined ( wote hawa wamesoma kayumba kuanzia la kwanza hadi form six )

Huyu wa 2007 yupo form four. Amesoma private kuanzia chekechea hadi form four. She is very smart darasani but kuhusu discipline nisiseme uongo. Ana leta uzungu mwingi. ( anajionaga kama.yupo na kina Ticha Thomas muda wote ) Kwake yeye uzungu ndio ujanja. I was so much dis appointed with her nilipomuuliza anataka kuja kuwa nani akaniambia she want to be a soldier. Duh yani Mimi nahangaika kulipa mamilioni ya hela halafu unakuja kuniambia unataka kuwa mwanajeshi? Hiyo hela si bora ningeenda kutoa single kwa .master Jay nikakusomesha Kayumba? ( ningejua ange kuja kuwa na wazo kama.hili aisee Kayumba ingemfaa sana kuanzia std 1 . Ila nashukuru Mungu huyu dogo amenisanua)

Hawa wawili niliwarudisha Kayumba mmoja akiwa la tatu na mwenzake akiwa la kwanza now mmoja yupo la nne na mwenzake la pili ( I am so much pleased na namna walivyo na discipline )

Namshukuru Mungu nimestuka mapema.

Mimi Nina afadhali, kuna jamaa zangu ambao wamekuwa dis appointed big time.

1. Kuna huyu brother ( was born in early 80s) a very smart dude . Darasani alikuwa anafanya vizuri sana. Mtoto wake wa kwanza wa kiume kamlipia private kuanzia chekechea hadi form four. He was paying almost 4 million per year ( hiyo ada 2 ukijumlisha na makorokoro mengine inafika almost 7 million)( hiyo chekechea na Primary)
Secondary kampeleka Alpha. Dogo kamaliza form four kapata one Kali. Ila kagoma kwenda form six. Anataka kwenda chuo. Now anasoma CBE. Kozi anayo isoma sasa? Procurement ina nafuu.

Baba mtu amechanganyikiwa amekuwa dis appointed watoto wake wengine wote kawarudisha Kayumba ( mmoja class 5, mwingine glass 2) na.mwingine form 3. Hataki tena kusikia habari za kulipa mamilioni kusomesha mtoto.

Huyu ana ahueni kuna dada mmoja mlokole best yangu, ni single mother , kamsomesha mtoto wake wa kiume shule za private kuanzia chekechea hadi form four . Dogo kapata one form form four ila anataka kusoma chuo. Kozi anayoitaka sasa!!! Anataka driving.

Mama kamshauri Mwanae hadi kachoka kaita wachungaji na walimu wamshauri ila dogo msimamo wake uko palepale.

Mwisho wa siku kanitafuta nimpe ushauri Mwanae asome chuo gani nikashauri asome Veta akisha pata leseni ya udereva aende pale NIT asome Defensive Driving plus other driving courses. ( nilishauri hivi ili at least mama mtu apate faraja aone mwanae anasoma kitu cha kueleweka) Now dogo yupo Veta, mama.mtu anasema mtoto wake amerogwa...

Kama.uwezo wako ni mdogo usijibane kumsomesha mtoto wako English Medium kwa matarajio kwamba eti atakuja kuwa vile unavyo tarajia wewe nope. English Medium waachie wenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao kwao hiyo milioni 7 kwa mwaka sio pesa ya mawazo.

Wewe mwenye pesa ya mawazo bora umsomeshe Kayumba mwanao halafu pesa itumike kufanya mambo mengine ya maana.

Zile zama za eti kulala chini ili mtoto asome hazipo tena.Gone are those days!!
Usije kuishia kumpa mwanao radhi bure. Wewe unataka awe injinia kama Hersi kumbe mwenzako anataka kuwa kama Konde Boy.

Ni Mimi Likud wa JF..

Rais wa,
BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN

motto : MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN CAMPAIGN

There has to be another option kwa ajili ya watoto wa kileo kama unavyosema kupeleka kayumba is not the only option
Bado hujaelezea kayumba inafanyaje ili kumshape mtoto
The only benefit naona hapo ni kusave pesa tu sioni maajabu mengine
Issue ya discipline nikuulize watoto wote wa kayumba wana discipline na wa english medium hawana?
What is your reasoning bado sijakusoma
Tunaongelea mabadiliko ya watoto katika teenage stage hio ni stage ambayo malezi yenyewe huanza bad enough wazazi tunasukumia shule zitulelee watoto hatutaki kuwalea wenyewe ndio hii hoja yako inakuja
Hamna sababu ya kayumba au english medium ina justify kuharibika kwa watoto
Malezi ya wazazi ndio sababu
 
Kayumba ni shule za wale wasio kua na plan B, wenye abject povert,....... wanao toboa maisha kupitia elimu wengi hutokea shule za magari ya njano, kijiji chetu tulio maliza darasa la saba tulikua 105, tulio weza kufika dar es salam na kuendekea na elimu ya juu tuko wa wili tu, kijiji kizima kina tutetegemea sisi mwaka uliofuatia hamna alio toboa, mwenzangu alisoma dip in electronics, mimi ndo nilio toboa zaidi.........

Wengi ni boda boda, wakulima, vibarua, mama wanyumbani, wengine walisha kufa n.k.......elimu ya kayumba is harzadius au massacre kwa future za watoto wa kitanzania, mpaka pale ccm itakapo kua na utashi wa kuboresha elimu ya nchi hi, mimi sitakuja kumpeleka mwanangu shule hizo hiyo ni 'ecademic suicide'.

There has to be another option kwa ajili ya watoto wa kileo kama unavyosema kupeleka kayumba is not the only option
Bado hujaelezea kayumba inafanyaje ili kumshape mtoto
The only benefit naona hapo ni kusave pesa tu sioni maajabu mengine
Issue ya discipline nikuulize watoto wote wa kayumba wana discipline na wa english medium hawana?
What is your reasoning bado sijakusoma
Tunaongelea mabadiliko ya watoto katika teenage stage hio ni stage ambayo malezi yenyewe huanza bad enough wazazi tunasukumia shule zitulelee watoto hatutaki kuwalea wenyewe ndio hii hoja yako inakuja
Hamna sababu ya kayumba au english medium ina justify kuharibika kwa watoto
Malezi ya wazazi ndio sababu
 
Je, Mwanao Hali yake hiyo imesababishwa na kusome English Medium?
Kuna any connection?
Kwamba watoto wakisoma Kayumba hiyo age ya Balehe haiwasumbui ?
Kasoma english medium mda wote,
Mamaake alikataa asiende kayumba anajutia mpk leo.
Mtoto alifaulu vizuri tu akapangiwa seminari nzuri tu mama kakataa.
Tukapeleka private ni hela baada ya hela.
Kamaliza nikambeba mazima
Aje tupambane.
Connection kapata mahali pazuri tu.
Katosa.
Nikamuacha apambane na hali yake na Malengo yake
 
Kayumba mtoto anajua vitu vingi kuhusu maisha ,,,kufagia uwanja ,kupanda maua ,kufanya usafi chooni na darasani ,usafi kuanzia kiatu mpaka mavazi ....maana yote hayo anayafanya mwenyewe Tena Kwa fimbo ....kuelekezwa kidogo na kujitafutia kingiii .......na haya ndio maisha halisi ya Duniani ...

Kutana sasa na Hao st Mary's sijui nin ,uzungu mwingi tu [emoji23]...mtoto WA kike anajua U nooo ,bikozi ,ze boyifurendi.....kupika haijui ,kufua hajui ,usafi hajui ,hata kufagia uwanja hawezi ....anakuwa boyaaaa boyaaaa ti zobaaaa shittyt kabisa

Hio ni kazi ya mzazi kumfundisha mtoto sio walimu
Wazazi kumpeleka mtoto shule,kumlisha,kumvesha kumpa mahitaji muhimu haitoshi,waleeni watoto wenu msiwaachie walimu wafanye hio kazi mtavuna mabua
Wazazi acheni uvivu kwa kujificha kwenye kivuli cha ubusy
Watoto wanaharibikiwa sio private schools au kayumba sababu ni wazazi wenyewe
 
Bado unasomesha watoto wako huku unawaza white collar jobs,bado una safari sana...
English medium zitaendelea kuwa suluhisho ya kizazi hiki Cha competition,sio mtoto analetewa mnyarwanda tu wa hapo Kigali anashindwa kujielezea😥
 
Wanafaulisha kisiasa ila wako empty kichwani asikudanganyi mtu, shule za kayumba zinazo jitahidi ni zile kwenye majiji makubwa kama Dar arusha mwanza moro dodoma tena sio zote.
Sio zote lakini nyingi kwasasa ziko vizuri tofauti na zamani.

Jamaa kashauri vizuri kama uwezo wako ni mdogo usihangaike na private schools. Tafuta kayumba yenye unafuu iliyo karibu nawe mpeleke mwanao.

Labda eneo lako shule shule ziwe hazieleweki kabisa.

Lakini kama uwezo upo, mpeleke private ni bora zaidi.
 
Kayumba ni shule za wale wasio kua na plan B, wenye abject povert,....... wanao toboa maisha kupitia elimu wengi hutokea shule za magari ya njano, kijiji chetu tulio maliza darasa la saba tulikua 105, tulio weza kufika dar es salam na kuendekea na elimu ya juu tuko wa wili tu, kijiji kizima kina tutetegemea sisi mwaka uliofuatia hamna alio toboa, mwenzangu alisoma dip in electronics, mimi ndo nilio toboa zaidi.........

Wengi ni boda boda, wakulima, vibarua, mama wanyumbani, wengine walisha kufa n.k.......elimu ya kayumba is harzadius au massacre kwa future za watoto wa kitanzania, mpaka pale ccm itakapo kua na utashi wa kuboresha elimu ya nchi hi, mimi sitakuja kumpeleka mwanangu shule hizo hiyo ni 'ecademic suicide'.
Sahihi kabisa mkuu
 
Yeye kasema anataka kuwa dereva hataki tena kusoma

Kuna kitu kipo nyuma ya yeye kutaka kuwa dereva
Nikiwa mdogo nilipenda sana kuwa miss,hii ilichangiwa na mama alipenda niwe miss,kila siku jioni nilikuwa nafanya catwalk na viatu virefuuu[emoji3][emoji3][emoji3].Nakumbuka mzee alikuwa anamind sana haya mambo ya mama nikimaliza zoezi la catwalk alikuwa ananiita ananiambia mimi sikupangii unataka kuwa nani baadae lakini jua tu kuna uzee,kuna baadhi ya kazi zina limit ya age jitahidi upate kazi ambayo haitoathiriwa na age yako
Alikuwa ananipa mfano ukitaka kuwa dancer ujue ukifika 40’s viungo vinauma itakuwa mwisho wako
Nakumbuka mimi na kaka zangu alikuwa anatuambia haya mambo mara kwa mara na toka tukiwa wadogo tuliweza kujua tunataka kuwa nani na hivyo ndivyo tumekuja kuwa.Kidogo walichokosea kwenye skills and talents hawakutufatilia sana tumezipush wenyewe kiubishi
My point is sauti ya mzazi inatakiwa kuwa kubwa kuliko sauti nyingine yoyote kwa mtoto.Ninaposema sauti iwe kubwa sio kumfokea,ila sauti ya wazazi iishi ndani ya watoto,how?that’s the puzzle ya mzazi kutegua huo mtego
Tena kwa watoto wa sasa hivi kuna sauti nyingi sana sababu ya technology etc
Mzazi ukipoteza sauti yako kwa mwanao jiandae kustaajabishwa na maamuzi yake.
Huyu mtoto badae atajiuliza kwanini alichagua udereva tu while angeweza kuongeza na ujuzi mwingine pia.Mimi nawalaumu wazazi wake wala wasishangazwe sana na maamuzi yake
 
Mkuu umeongea ukweli. Na Kuna Ile hadhi zao wanapokuwa wanauzia maua unasikia mwanangu anasoma shule fulani Yani Ile shule ada zao za kirafiki sana, wanajazana upepo
Halafu dogo alivyoanza la kwanza ndani ya mwezi wakasema ana akili sana tunamrusha la pili. Mama mtu anafurahi anakuambia angeenda ulipotaka angekua wapi

So dogo yupo la 2 private mdogo wake ndiyo hao middle class.

Baba yao chekechea nilisoma kwa Mwalimu Mjaluo, msingi kayumba na tution za kubaki ukifika muda wa kuondoka. O na a level kayumba
 
Kuna mtoto, kwao pesa zipo, anapelekwa shule za gharama. Mtoto yupo darasa la nne anafungwa viatu kamba, anafungwa vifungo vya shati. Mtoto wa kike anafuliwa Pichu mpaka darasa la sita. Kwa ujumla wanakuwaga wapumbavu kichwani.
 
Hio ni kazi ya mzazi kumfundisha mtoto sio walimu
Wazazi kumpeleka mtoto shule,kumlisha,kumvesha kumpa mahitaji muhimu haitoshi,waleeni watoto wenu msiwaachie walimu wafanye hio kazi mtavuna mabua
Wazazi acheni uvivu kwa kujificha kwenye kivuli cha ubusy
Watoto wanaharibikiwa sio private schools au kayumba sababu ni wazazi wenyewe
Mzazi atafundisha mtoto wapi wakati muda mwingi Yupo Kazin na mtoto Yuko Shulen ,na hata likizo mtoto anakuwa nyumbani mzazi kazin ,Ni muda mchache mnoo ambao mzazi anakuwa na mtoto kuliko shuleni kuwa na mtoto ....piga hesabu mwaka unasiku 365 lakin katika hizo siku unakuta siku nyingi mtoto katumia kuwa na walimu Shulen ...mzazi siku chache ....

Sasa hizo siku alizotumia kuwa na mwalimu kama walimu hawamfunzi na kumkanya vzuri anakuwa mayai mayai hizo st Mary's sijui medium zinafanya mtoto anapooza kimaisha ya Duniani ...huko anafuliwa ,anapikiwa ,ananyoshewa nguo ,anafungiwa tai ,usafi hadi kiti anachokaa anapangusiwa ,bustani ya Shule hajui hata maua yanapandwa vipi ,yaani mtoto anakuwa boss....

Kayumba mtoto anakuwa strong kuanzia hatua ya Kwanza anayoingia Shule ,asubuhi tu anaingia Shulen anajua usafi unahitajika ,kufagia shuleni uwanja ,chooni ,darasani ,usafi wake yeye mwenyewe shati ,viati soksi mwalimu tu anapita kukagua ukiwa hovyo ni fimbo ,,tai utajua kufunga tu automatic ,,,maua utaleta wewe na utapanda shuleni ,utamwagilia maji ....utajua kuelekezwa kidogo na kujiongeza kutafuta ...maana usipofanya hivo Ni fimbo tu .....shuleni atafundishwa adabu ,kusalimia ,....aiseee hiki kitu hauwezi kukiona english medium maana huko mwanafunzu ndio boss[emoji23],,,wakati kayumba mwalimu ndio boss so anahakikisha watoto wako msatari mnyoofu ....

Medium mtoto anaweza mvimbia mwalimu hata asimsalimie na walimu wenzake wakamsupport mwanafunzi maana mwanafunzi Ni boss ndio anapesa ,kayumba unaingia stafu ofsin Kwa adabu na dua zote na heshimu maana ukifanya utovu WA nidhamu utakula fimbo mpaka Akili itakukaa sawa ......mtoto anakomaa toka shuleni mpaka nyumbani .....

Kayumba inakufundisha the real meaning of current life tusifichane bana ,,,,hizo medium zinawafanya watoto kuwa goigoii...
 
Biblia inasema Mungu aliwapenda sana wana Isachar ( sio Isaka ni ISACHAR: Huyu Isachar alikuwa ni kati ya watoto 12 wa Yakobo. Sasa huyu Isachar alikuwa na watoto wa kiume 200 ndio hao ambao ninawazungumzia.

Biblia inasema Mungu alipendezwa sana na wana wa Isachar.

Sababu kuu iliyo mfanya Mungu apendezwe na wana Isachar utaikuta kwenye kitabu cha 1 Chronicles 12:32.

They knew what Israel had to do and at what time and how to do it.

Kwa ufupi hawa wana wa Isachar walikuwa ni majasusi.

JASUSI ni mtu anae jua kitu gani kinatakiwa kufanywa na wakati gani na kwa namna gani.

JASUSI anajua yote hayo sio kwa kupitia uchawi bali ni kupitia sanaa ya kutafuta na kuku sanya taarifa (the art of intelligence gathering) kuchakata taarifa (the art of intelligence processing) kuandika ripoti ya kitaalamu kupitia taarifa zilizo kusanywa na kuchakatwa ( the art of intelligence report) na kuifanyia kazi ripoti hiyo (the art of intelligence execution) .

Kikubwa zaidi ni kujua wakati gani muafaka wa ku -execute hizo taarifa.

Wana wa Isachar walikuwa ndio the brain behind King David's victory in all wars and battles which he fought.

Kwa wasio jua, His Majesty King David, the King of the United Kingdoms of Israel and Judah, ndio mfalme ambae hajawahi kushindwa vita yoyote ile katika utawala wake. Huduma ya ujasusi kutoka kwa wana wa Isachar ilikuwa ni sababu kuu mfalme Daud alishinda vita zake zote.

Mfalme Daudi alikuwa na intelligence madhubuti sana. (Nenda kasome kitabu " Rise and Kill First: The secret history of Israel's Targetted Assasinations " kilicho andikwa na Investigative Journalist na JASUSI wa kiyahudi aitwae Ronen Bergman ili uweze kujua wana wa Isachar ni watu wa namna gani katika dunia ya sasa)

The reason why King David acted strangely during Absalom Rebellion was because of the advice he was given by the children of Isachar. At the end of the day King David secured the victory without even putting a fight. All this ni kwa sababu ya kuzungukwa na wabobezi wa ujasusi.

Binafsi tangu nifahamu kuhusu siri hii ya wana wa Isachar nimekuwa nikiitumia hadi kwenye vitu vya kawaida kabisa kwenye maisha yangu.

Hata michepuko wangu huwa nawafanyia ujasusi kabla ya kuwapa " zawadi" ya kuwa nao kimapenzi. Kila mwanamke ana file na dawati lake. Mfano " Fatuma's desk" ( Dawati la Fatuma: dawati maalumu la ku dili na masuala yote yanayo muhusu Fatuma. Humo kuna mafaili yenye taarifa zote kuhusu Fatuma plus what when and how to act when dealing with Fatuma). The same to my children. Kila mtoto ana dawati lake.

BACK to my topic . Wazazi wengi wa miaka hii ya elfu 2 ambao ndio kina sisi tulio zaliwa miaka ya themanini katikati na mwishoni ( themanini mwanzoni na 70 mwishoni) plus miaka ya tisini mwanzoni, kwenye mindset zetu hatunaga image ya mtoto ambae yupo kwenye adolescent age ( teen age / foolish age) When it comes to children, wengi wetu huwaga tuna picha ya yule mtoto wa mwaka 0 mpaka 9 au 12 n.a. 13 hapo. Mtoto ambae bado ni mtiifu kwa almost kila kitu. Mtoto anaeweza kudhibitiwa hata kwa fimbo etc.

Wengi wetu huwaga hatujiandai kisaikojia kukabiliana na changamoto za mtoto alie balehe. Huwaga tunadhani mtoto ataendelea kuwa " Mtoto " hivyo hivyo maisha yake yote..

Utamsikia mtu anasema " namlipia mamilioni mtoto wangu shule hii ya English Medium kwa sababu hapa wanafaulisha vizuri. So nataka afaulu vizuri hapa then aende O level then A level then Chuo the apate kazi yake nzuri"

Mawazo kama hayo 👆 anasema Robert Kiyosaki kwenye kitabu " Poor Dad Rich Dad " yalikuwa valid kuanzia mwaka 1985 kushuka chini and not after that. Sasa hivi dunia imebadilika ( kumbuka hiyo ilikuwa mwaka 97 mzee ) Sasa hivi ni 2023 dunia imebadilika zaidi. Mfumo wa maisha ya dunia ya sasa umebadilika juu chini kama ulivyo badilika pale Eden baada ya Adam na Hawa Kula tunda la mti ule ulio katazwa...

Wakati wewe mzazi unahangaika kulipa mamilioni ili mtoto wako awe injinia, mwanasheria au daktari kumbe mwenzako anawaza kufanya kitu tofauti kabisa na wewe. Anataka kuwa kama Mzize, Zuchu au Gigy Money

Ndo maana nasema no matter how much money u put on ur children when they are young, when they grow up they will branch out.

Kwa wewe mzazi ambae una watoto wadogo ambao ni watiifu kwako at this moment fanya yote unayo fanya lakini jua kwamba wakifika adolescent age wata branch out. Watakuwa tofauti kabisa na unavyo tarajia..

Mimi namshukuru Mungu nimeujua huu ukweli tangu nikiwa mdogo kwa sababu Nimepata watoto nikiwa mtoto.

Nimesex ( kikubwa kubwa achilia zile za utotoni za kufanya kinguo nguo au kichupi chupi) kwa mara ya kwanza tareje 18 November 2000 nikiwa kidato cha pili najiandaa kuingia form three. I was 15 years old and she was 15 years old too. Tuliendelea na kamchezo Ketu mpaka demu akapata ujauzito nikapata mtoto wa kwanza wa kike nikiwa nna miaka.16 ( 2001) ( kumbuka jambo hili ni kinyume kabisa na maadili ya familia yetu Nimetoka kwenye familia inayo swali)

Mwaka 2003 nikiwa nna miaka 18 nikapata mtoto mwingine wa kike kwa mwanamke mwingine.

Hawa wote walisoma Kayumba.

Mwaka 2007 nikapata mtoto mwingine wa kike kwa mwanamke mwingine. Huyu alinikuta tayari nna vihela hela nikampeleka English Medium kuanzia la kwanza hadi la saba. N.a. private school kuanzia form one hadi form four.

2015 n.a. 17 nikapata watoto wawili wa kiume kwa mwanamke mmoja.

Huyu wa 2001 now yupo chuo mwaka wa mwisho ( she is very smart and very disciplined. )

Huyu wa 2003 yupo Chuo mwaka wa kwanza. She is very smart and very disciplined ( wote hawa wamesoma kayumba kuanzia la kwanza hadi form six )

Huyu wa 2007 yupo form four. Amesoma private kuanzia chekechea hadi form four. She is very smart darasani but kuhusu discipline nisiseme uongo. Ana leta uzungu mwingi. ( anajionaga kama.yupo na kina Ticha Thomas muda wote ) Kwake yeye uzungu ndio ujanja. I was so much dis appointed with her nilipomuuliza anataka kuja kuwa nani akaniambia she want to be a soldier. Duh yani Mimi nahangaika kulipa mamilioni ya hela halafu unakuja kuniambia unataka kuwa mwanajeshi? Hiyo hela si bora ningeenda kutoa single kwa .master Jay nikakusomesha Kayumba? ( ningejua ange kuja kuwa na wazo kama.hili aisee Kayumba ingemfaa sana kuanzia std 1 . Ila nashukuru Mungu huyu dogo amenisanua)

Hawa wawili niliwarudisha Kayumba mmoja akiwa la tatu na mwenzake akiwa la kwanza now mmoja yupo la nne na mwenzake la pili ( I am so much pleased na namna walivyo na discipline )

Namshukuru Mungu nimestuka mapema.

Mimi Nina afadhali, kuna jamaa zangu ambao wamekuwa dis appointed big time.

1. Kuna huyu brother ( was born in early 80s) a very smart dude . Darasani alikuwa anafanya vizuri sana. Mtoto wake wa kwanza wa kiume kamlipia private kuanzia chekechea hadi form four. He was paying almost 4 million per year ( hiyo ada 2 ukijumlisha na makorokoro mengine inafika almost 7 million)( hiyo chekechea na Primary)
Secondary kampeleka Alpha. Dogo kamaliza form four kapata one Kali. Ila kagoma kwenda form six. Anataka kwenda chuo. Now anasoma CBE. Kozi anayo isoma sasa? Procurement ina nafuu.

Baba mtu amechanganyikiwa amekuwa dis appointed watoto wake wengine wote kawarudisha Kayumba ( mmoja class 5, mwingine glass 2) na.mwingine form 3. Hataki tena kusikia habari za kulipa mamilioni kusomesha mtoto.

Huyu ana ahueni kuna dada mmoja mlokole best yangu, ni single mother , kamsomesha mtoto wake wa kiume shule za private kuanzia chekechea hadi form four . Dogo kapata one form form four ila anataka kusoma chuo. Kozi anayoitaka sasa!!! Anataka driving.

Mama kamshauri Mwanae hadi kachoka kaita wachungaji na walimu wamshauri ila dogo msimamo wake uko palepale.

Mwisho wa siku kanitafuta nimpe ushauri Mwanae asome chuo gani nikashauri asome Veta akisha pata leseni ya udereva aende pale NIT asome Defensive Driving plus other driving courses. ( nilishauri hivi ili at least mama mtu apate faraja aone mwanae anasoma kitu cha kueleweka) Now dogo yupo Veta, mama.mtu anasema mtoto wake amerogwa...

Kama.uwezo wako ni mdogo usijibane kumsomesha mtoto wako English Medium kwa matarajio kwamba eti atakuja kuwa vile unavyo tarajia wewe nope. English Medium waachie wenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao kwao hiyo milioni 7 kwa mwaka sio pesa ya mawazo.

Wewe mwenye pesa ya mawazo bora umsomeshe Kayumba mwanao halafu pesa itumike kufanya mambo mengine ya maana.

Zile zama za eti kulala chini ili mtoto asome hazipo tena.Gone are those days!!
Usije kuishia kumpa mwanao radhi bure. Wewe unataka awe injinia kama Hersi kumbe mwenzako anataka kuwa kama Konde Boy.

Ni Mimi Likud wa JF..

Rais wa,
BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN

motto : MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN CAMPAIGN

Stupidity in a making.....
 
Kasoma english medium mda wote,
Mamaake alikataa asiende kayumba anajutia mpk leo.
Mtoto alifaulu vizuri tu akapangiwa seminari nzuri tu mama kakataa.
Tukapeleka private ni hela baada ya hela.
Kamaliza nikambeba mazima
Aje tupambane.
Connection kapata mahali pazuri tu.
Katosa.
Nikamuacha apambane na hali yake na Malengo yake
Kwa hiyo unahisi angeenda Kayumba asingekuwa kama alivyo Kwa sasa ?
 
Back
Top Bottom