N'golo Kante sifa zimemzidi hadi kiburi kinamnyemelea

N'golo Kante sifa zimemzidi hadi kiburi kinamnyemelea

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka wanajamvi!

Nyodo, ngebe, dharau, majigambo, majivuno vinaweza kumpata asipojiangalia.

Ngolo Kante mchezaji wa mpira mstaarabu na muungwana kuliko wote inaonekana sifa zimemjaa hadi utanashati wake uliotukuka kwa mbali unaanza kuingia na doa. Hii ni kutokana na mtazamo wangu.

Siku hizi anacheza rafu sana. Anatembeza ngwala bila huruma hii siyo sawa kwa mchezaji wa kaliba yake.

43609391-9633331-image-a-67_1622331369025.jpg
.​

Pia matanuzi na kujionesha sana mali zake mitandaoni. Asiende kasi sana. Tulimzoea na magari ya kawaida sasa hivi anapiga picha na magari ya ghali na ya ajabu ajabu.

Screenshot_20210603_073011.jpg

Ajiangalie sana asipoteze focus kwa sifa kedekede anazopata sasa hivi na huenda akawa mchezaji bora wa mwaka duniani na hadhi yake iliyotukuka kushuka.

Licha ya yote namtakia mafanikio mema na tunasuport sana na tunamkubali.

Senior JF Local and International sports analyst and correspondent

Masters
 
Wewe upo nyuma ya wakati. Hiyo picha tangu mwaka juzi naiona mitandaoni.

Halafu uchezaji wa rafu nao pia kwa position anayocheza rafu za hapa na pale hazikosekani. Lakini katika hili pia sijaona mabadiliko yoyote.

N'Golo Kante ni yuleyule jana, leo na kesho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muacheni kijana hata kama atajipnyesha lakini anapambana na jitihada zake zinaonekana
 
Kama ushabiki wa Man city au Real Kwanza pole mana huyo kiumbe mnajua alichokuwa anakifanya uwanjani mlipokutana nae.

Kwenye hizo rafu unazosema wewe, jee anakadi nyekundu ngapi?

Hizo picha pia nizamiaka mingi .
naona kweli umeanza mjua kante alipowafanya kitu kibaya kipindi hichi.
Ila huyo ndo kante wa kila kipindi
 
Sawa sijakataa. Lakini zamani hizi rafu hazikuwepo. Yani kante sasa hivi anatandaza rafu sana. Ni Hulka ya mwanadamu akisifiwa sana
Kante yupi hakuwahi kucheza rafu? Au unamaanisha Dante???
 
Kwa nafasi yake kucheza rafu siyo stories,hayo mengine ni maisha binafsi kuyajadili ni kupoteza muda tu
 
Back
Top Bottom