N'golo Kante sifa zimemzidi hadi kiburi kinamnyemelea

N'golo Kante sifa zimemzidi hadi kiburi kinamnyemelea

Haya, nyingine hiyo. Wewe pambana na hali yako
A6CC0EDB-041F-4010-8599-331F1FEE3CFC.jpeg
 
Kwa nafasi kupata kadi kwa kucheza rafu ni kawaida labda uwe mgeni au mamluki katika mchezo huu pendwa...
Kuhusu kuonyesha Magari yake na vitu vya thamani muache afanye hivyo maana ni jasho lake ndilo linaloleta vyote hivyo,
Hakuna timu ulaya isiyotaka kua na mchezaji kama Ngolo Kante
 
Sawa sijakataa. Lakini zamani hizi rafu hazikuwepo. Yani kante sasa hivi anatandaza rafu sana. Ni Hulka ya mwanadamu akisifiwa sana
Ndiyo sababu CHELSEA FC ni mabingwa wa Ulaya na domestic cup (FA)..

Bila ya hizo "technical tackling" zake ambazo wewe unaziita "rafu" usingeona Chelsea wakiweka kabatini makombe maarufu mawili...!

Unamkumbuka Roy Kean aliyekuwa kiungo mkabaji hatari wa Man Utd au Steven Gerrad wa Liverpool FC...?

Hawa wote walikuwa viungo wakabaji wa sampuli ya Ng'holo Kante. Bila tacklings za aina ya Kante, Roy Keane, Steven Gerrard au Paul Scholes timu yako haiwezi kutoboa...

Hayo ya nje ya soka umetia chumvi tu kwa kuokoteza vihabari vya kutengeneza ktk mitandao na kudhani Kante ndivyo alivyo...!
 
Uchambuzi mzuri sana mkuu.

Masahihisho:
Chelsea hatujachukua kombe la FA. Tulipigwa na Leicester City fainali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha aliyosimama na gari ni ya kutengeneza

Jamaa mpaka sasa anadrive mini cooper yake....
 
Sawa sijakataa. Lakini zamani hizi rafu hazikuwepo. Yani kante sasa hivi anatandaza rafu sana. Ni Hulka ya mwanadamu akisifiwa sana
Yaan zama zipi hizo ambazo hakukuwa na rafu??? Zama za akina Patrick Viera ama Jean Claude Makelele??? Kante bado sana rafu zake hazijafikia miamba hao wawili kwahiyo hana mwenendo mbaya.
 
Humjui Ngolo Kante tulia

Ngolo Kante aliamua kuiacha Mini Copper yake nyumbani akaamua kuchukua treni wakati akiripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya EURO juzi.

Kwa bahati mbaya treni ilichelewa kwasababu ya hitilafu iliyotokea katika kituo kimoja. Ngolo Kante akachelewa kuripoti kambini.

Alipofika kambini, kikao kilishakwisha na wachezaji walikuwa wanaendelea na mambo mengine.

Alifika kwa kocha Didier Deschamps na kumpa tabasamu kama kawaida yake kisha akamuambia nimecheleweshwa na treni.

Didier Deschamps hakuwa mkali kwake. 'Anajua tu huyu ni Ngolo Kante na hawezi kuchelewa nje ya taratibu kwasababu za kihuni'.

Didier Deschamps alimpa tabasamu na kumuambia, "Lakini Ngolo Kante upo fasta kuliko treni kwanini hukuiacha kisha ukaja mwenyewe??" 🤠. Walicheka wote kisha kesi iliishia hapo.

NGOLO KANTE ALISAMEHEWA KWASABABU NI NGOLO KANTE.
 
Back
Top Bottom