N'golo Kante sifa zimemzidi hadi kiburi kinamnyemelea

Arsene Wenger;
"Kwa mtazamo nafikiri N'Golo Kante ndiye kiungo bora zaidi kwasasa kwa bara zima la Ulaya. Kuna kitu amekiongeza kwenye soka lake."

"Hapo kabla alikuwa ananyang'anya mipira vizuri na anatoa pasi nzuri, alikuwa ni mchezaji bora sana kwenye kupora mipira. Nasema ni mchezaji bora kwenye kunyang'anya mipira sababu anaweza kuunasa mpira bila kucheza madhambi."

"Lakini kwasasa ana uwezo pia wa kuunasa mpira kisha akakimbia na kwenda kutoa pasi nzuri kwenye eneo la timu pinzani. Na ndiyo maana nasema kwasasa yeye ndiye kiungo aliyekamilika kwenye bara zima la Ulaya."
#d1905_updates
 
Thierry Henry;
"Ni nadra sana kuona mchezaji anafika kabla ya mpira kufika. Kama ambavyo (Kante) amekuwa anafanya, anajua kabisa kwamba mpira utaenda kutua pale."

"Kuna wakati anafika eneo ambalo mpira baadae unafika, huwa nabaki kujiuliza, kwani alijuaje?"

"Ana uwezo wa kuusoma mchezo na kunyang'anya mpira bila kucheza madhambi, na ana uwezo wa kukata mashambulizi yanayosababishwa na timu pinzani."

"Ana uwezo wa kubadilisha shambulizi la hatari linalosababishwa na timu pinzani na kulifanya liwe shambulizi la kushtukiza kwenda kwa timu pinzani."

"Unaweza kutengeneza shambulizi kuwashambulia, lakini anaupora mpira na kusababisha hatari kubws tena dhidi yako.
 
Wacha afaidi matunda ya jasho lake. Unateseka ukiwa kidimbwi gani wewe?
 
Ngolo Kante ni mtu mzuri tu, wnaomuharibu ni hawa mashabiki wake mandazi mpaka wamefikia kumuaminisha kuwa anakwenda kubeba balloon d'or
Kwani mwenyewe anasemaje kuhusu ballon d'or
 
Na hiki ndio alichowafanyia madrid nje ndani na city
 
Uchambuzi mzuri sana
 
Kipimo cha rough ni red card sasa kantetele mnyama anakadi ngapi..?
 
Hahahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…