Bwana Mkaruka unapoteza muda kushindana na jamii ya vijana wenye uwezo finyu wa kuelewa na kupembua mambo,
Mtu yoyote ambaye ameelimika na muungwana hawezi shabikia Public Nudity ambazo hufanywa na wasanii wetu,
Ifike mahali tutambue kwamba wasanii ni kioo cha jamii hivyo ni lazima wawe na adamu ili kulinda jamii nzima.
Wajinga wajinga wote ambao wanashangilia hivi vitendo vya ngono kwanza nikuhakikishie kwamba wanatokea kwenye jamii za hovyo hovyo kabisa na hata mahakamani hawajawahi kufika. Ukishafika mahakamani na yakakukuta nadhani kuna kiwango fulani cha adabu utakuwa nacho.
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa nikiletewa kesi za namna hii au zile za ubakaji nilikuwa sioneshi hata chembe ya huruma kama waendesha mashitaka wengine. Utageuzwa mfano na utafungwa tu tena mvua nyingi labda uonewe huruma na hakimu au jaji. Ifike mahali ni lazima tutumie mitandao vizuri ili kulinda watoto wetu.
Ukifuatilia kesi ya Lulu utatambua kwamba alisema yeye yuko juu ya miaka 18, lakini baada ya Kanumba akasema yeye ni mtoto hivyo apelekwe Juvenile Court (Mahakama ya watoto). Lakini kwenye gazeti aliwahi kuweka cheti cha miaka 18 akisema "Nimetimiza miaka 18 sasa mabaunsa wa Club watanikoma". Waendesha mashitaka walitafuta yale magazeti na kuyapeleka mahakamani kuthibitisha kwamba Lulu siyo Minor.
Sasa nasema hivi "Ikithibitika huyo Paul ni mtoto wa chini ya miaka 18" basi imekula kwa huyo Rayvanny.
Lakini mpaka sasa kuvujisha video zao za namna hiyo ni sababu tosha kabisa ya kuwashikisha ababu wasanii kama yeye.