Ngoma mpya ya King Kiba (So Hot) ni hot kweli kweli

Alikiba niliyemzoea sio huyu wa sasa hivi. Alikiba aliyekuwa akitoa jiwe moja tu linasumbua mwaka mzima, akina Diamond and the like watahangaika kutoa nyimbo kama kumi but ngoma moja tu ya Alikiba ilikuwa inasumbua sana.

Alikiba umekuwaje tena, mbona unatuaibisha mashabiki zako tuliokuwa tukijisifia uwezo wako mkubwa wa kutoa nyimbo moja inasumbua mwaka na sehemu. Unaanza kuwa kama hasimu wako domo anayetoaga nyimbo kila siku, ndo kusema kipaji kinaanza kuisha au mashairi na melody kali zimeisha kichwani.

Basi tafuta hata mtu awe anakutungia basi nyimbo wewe unaingiza tu sauti kuliko huu utaratibu wako wa kuachia wimbo kila muda unatuaibisha sana sisi mashabiki tutawaambia nini watu?
 
Aisee ukiwasikiliza binadamu unaweza kuchanganyikiwa na ukafail sana. Akitoawimbo mmoja mwaka mzima mnasema anawaangusha hayuko serious kushindana, wasanii siku hizi ni ngoma baada ya ngoma. Basi naye kaamua kuanza fanya hivyo sasa bado mnamponda. Aisee kweli dunia ina maajabu hadi jogoo anaweza taga kama alivyoimba Roma
 


Kiba kaishiwa....jamaa hana kitu. Mpira hawezi, muziki uko ICU, arudi tu Kigoma kuvua dagaa.
 
Yaani hauwezi kumridhisha kila mmoja kwakweli
 
Hizi nguvu unazo wekeza kumfatilia Alikiba unge fatilia maisha yako ungefika mbali
 
Halafu hamjaona ile beat inavyofanana na hii ya kriz beat aliyemshirikisha Diamond??????
Angekuwa mondi kafanya hivyo zisingeisha nyuzi za kuponda humu ndani
 
Halafu hamjaona ile beat inavyofanana na hii ya kriz beat aliyemshirikisha Diamond??????
Angekuwa mondi kafanya hivyo zisingeisha nyuzi za kuponda humu ndani
Unakomaa kuaminisha watu upuuzi ambao hauna ukweli wowote
 
Umemaliza mkuu.

Humu kuna watu wazuri wa kusema nyuma ya key board ila ukienda kwenye fani zao ni failure wakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…