Ng'ombe mwenye thamani ya IST

Ng'ombe mwenye thamani ya IST

Nimeona mkuu, ila sijui kama niliyoiona ndiyo uliyoizungumzia😀

Kulingana na "Jarida" la African Farming Report la mwezi August 2023, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alilinunua dume la ng'ombe (Boran) kwa Randi 3.5m sawa na zaidi ya Tsh 400,000,000/=.

Dume hilo la ng'ombe lililojulikana kwa jina la Jester, lilikuwa likiuzws kwenye mnada wa Mpamalanga.

Taarifa pia zinaonesha kuwa Ramaphosa alimwuza mg'ombe wake wa Kiankole kwa Rand 2.65m, sawa na zaidi ya Tsh 200,000,000/=.

Kwa ufupi, ng'ombe waliotunzwa vizuri wana faida sana.
Mkuu pana mfugaji wa Arusha alinunua ng'ombe bei ya ajabu sana na anapandisha alinunua huko huko SA kwa kipindi alichonunua na gharama wanayomlipa kupandisha Jike atakua asharudisha hela unajua sisi hatuna exposure mtu akiniambia kitu cha Panama Canal ntabisha kweli kwa sababu muda wote tupo na habari za hovyo hovyo tu...hao Ng'ombe walitoka Rwanda wakaenda kutunzwa Uganda na kupandikiza na aina ingine ya ng'ombe ili watoke hao Ankole ya SA maana hao wa Rwanda walikua wakipelekwa moja kwa moja SA walikua wanakufa sasa unadhani wakitaka kuuzwa watauzwa bei gani?
 
Samahani mkuu! Kwa nini watu waliandamana?
ANC toka Zuma awekwe ndani imegawanyika wale wafuasi wa Zuma wakisikia kashfa yeyote ya Ramaphosa kama hii walizusha kuwa anatumia fedha za Serikali kununulia ng'ombe wake mpaka huko Bungeni kuliwaka moto..
 
Huyo jamaa yuko vizuri nimejifunza mengi sana na nitaenda siku moja UG kumtembelea
Mkuu, unalikumbuka jina la huyo mkulima?

Naona Value Farm ni channel yenye wakulima mbalimbali.

Nimevutiwa sana na mfugaji wa kike wa Uganda aliyeacha kazi ya ulecturer wa Vyuo Vikuu vitatu akaamua kuwa mfugaji. "Anatengeneza" hela nzuri kuliko aliyokuwa akiipata kwenye ufundishaji Vyuo Vikuu.
 
Mkuu mwaka huu kauzwa rand 3m zidisha mara Tsh 160 upate hela za kitanzania unaweza kudhani unadanganywa hata mtandaoni yupo...
Ingawa nafahamu kuwa ulishawahi kuishi South Africa, au pengine hata upo huko kwa sasa hivyo ni rahisi zaidi kuwa na taarifa sahihi kutuzido tuliopo nyumbani, ingawa kupitia nyuzi zako ninefahamu kuwa wewe si mtu wa longo longo, lakini kama isingelikiwa
google, inawezekana nisingeamini. Sana sana ningekuwa neutral, nisingekubali wala kukataa.

Lakini sasa sina mashaka tena! Nimeshafahamu kuwa kuna ng'ombe wanaouzwa ghali kuzidi bei ya V8 mpya "zero kilometre"
 
Mkuu, unalikumbuka jina la huyo mkulima?

Naona Value Farm ni channel yenye wakulima mbalimbali.

Nimevutiwa sana na mfugaji wa kike wa Uganda aliyeacha kazi ya ulecturer wa Vyuo Vikuu vitatu akaamua kuwa mfugaji. "Anatengeneza" hela nzuri kuliko aliyokuwa akiipata kwenye ufundishaji Vyuo Vikuu.
Ni huyu hapa bonge la mtu wa katikati, alikuwa Amerika miaka 15 kaamua kurudi kwao ndio kaanzisha mradi huo naona sasa yuko mbali sana alianza na kufyeka pori, akapeleka vijana baadae kaweka mabanda ya mbuzi wakawa wengi akaongeza kondoo, akalima nyasi kwa ajili ya malisho hapo hapo, akaongeza kondoo

Halafu kila akipata hela anawekeza kwenye mifugo
Kwa sasa ana nguruwe, kuku, na pia akaanza kuleta na ng'ombe wa Boran
Anauza mbegu bora kabisa Tena na vyeti anakuonyesha alikowanunua mpaka kuingia UG
Ni jamaa smart sana na huyo partner wake wa biashara ni mdada huyo kwenye picha
Valuefarm ni moja tu hiyo hiyo na sio wengi ni huyo Bonge na mdada
Screenshot_20231224_072048_Google~2.png
 
Ng'ombe wa kutoa Lita hizo wapo Ila ukiwaleta huku kutokana na.mazingira watatoa Lita chache
Kama ni mazingira mabaya hawatastahimili watakufa
Ukiona yupo yupo tu na hatoi maziwa mengi hivyo basi ujue lishe duni
Wanataka gharama haswa na pia uangalizi kwa madawa na usafi wa hali ya juu, maji Safi lazima

Kwa kina sisi wengi wanafikikiria ufugaji wa mifugo ni rahisi sana
Sawa kama umewekeza mamilioni na sio kama watu wanavyofikiri
Kama ng'ombe mmoja ni kuanzia 3m na mbuzi wa Boer au Kalahari ni laki 7 bado utahitaji labda na Mubende kadhaa na kondoo aina ya dorper
Hapo najipanga na 50m kwa kuanza na huo mradi yaani kila kitu
Bila hela utahangaika na mmoja tu ila mradi huu unalipa kama utawekeza kisawasawa
 
Sasa kama anakupa Lita 20 Tu x 2000= 40,000 Kwa siku x 30= 1,200,000 x mwaka= 14,000,000 toa 2,000,000 za kumtunza unarejesha pesa yote ...hapo ndama na mbolea sijaweka.Kuanzia mwaka wa 2 ni faida tu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mbona kama unajipigia upatu , umeleta Uzi kwa id nyingine unajipigia upatu kwa id. NYingine
 
Mkuu pana mfugaji wa Arusha alinunua ng'ombe bei ya ajabu sana na anapandisha alinunua huko huko SA kwa kipindi alichonunua na gharama wanayomlipa kupandisha Jike atakua asharudisha hela unajua sisi hatuna exposure mtu akiniambia kitu cha Panama Canal ntabisha kweli kwa sababu muda wote tupo na habari za hovyo hovyo tu...hao Ng'ombe walitoka Rwanda wakaenda kutunzwa Uganda na kupandikiza na aina ingine ya ng'ombe ili watoke hao Ankole ya SA maana hao wa Rwanda walikua wakipelekwa moja kwa moja SA walikua wanakufa sasa unadhani wakitaka kuuzwa watauzwa bei gani?
Ni kweli mkuu! Exposure bado ni changamoto kubwa sana kwetu. Ndiyo maana ninatamani sana niweze kuzitembelea nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
 
ANC toka Zuma awekwe ndani imegawanyika wale wafuasi wa Zuma wakisikia kashfa yeyote ya Ramaphosa kama hii walizusha kuwa anatumia fedha za Serikali kununulia ng'ombe wake mpaka huko Bungeni kuliwaka moto..
Inawezekana Waafrika ndiyo wanaoongoza kwa roho ya "kwa nini!"
 
Tumeshawazoea, anaweza kukwambia ukilima matikiti maji unakua bilionea unamzidi Moo na Baresa
Kwa nini motivational speakers wanadharaulika sana Tanzania? Mbona ni watu wa muhimu sana kwenye Jamii hasa kwa mazingira ya sasa yaliyojaa changamoto lukuki?
 
Ni huyu hapa bonge la mtu wa katikati, alikuwa Amerika miaka 15 kaamua kurudi kwao ndio kaanzisha mradi huo naona sasa yuko mbali sana alianza na kufyeka pori, akapeleka vijana baadae kaweka mabanda ya mbuzi wakawa wengi akaongeza kondoo, akalima nyasi kwa ajili ya malisho hapo hapo, akaongeza kondoo

Halafu kila akipata hela anawekeza kwenye mifugo
Kwa sasa ana nguruwe, kuku, na pia akaanza kuleta na ng'ombe wa Boran
Anauza mbegu bora kabisa Tena na vyeti anakuonyesha alikowanunua mpaka kuingia UG
Ni jamaa smart sana na huyo partner wake wa biashara ni mdada huyo kwenye picha
Valuefarm ni moja tu hiyo hiyo na sio wengi ni huyo Bonge na mdada View attachment 2851391
👏👏👏🙏
 
Kama ni mazingira mabaya hawatastahimili watakufa
Ukiona yupo yupo tu na hatoi maziwa mengi hivyo basi ujue lishe duni
Wanataka gharama haswa na pia uangalizi kwa madawa na usafi wa hali ya juu, maji Safi lazima

Kwa kina sisi wengi wanafikikiria ufugaji wa mifugo ni rahisi sana
Sawa kama umewekeza mamilioni na sio kama watu wanavyofikiri
Kama ng'ombe mmoja ni kuanzia 3m na mbuzi wa Boer au Kalahari ni laki 7 bado utahitaji labda na Mubende kadhaa na kondoo aina ya dorper
Hapo najipanga na 50m kwa kuanza na huo mradi yaani kila kitu
Bila hela utahangaika na mmoja tu ila mradi huu unalipa kama utawekeza kisawasawa
Kwa kifupi, hakuna kizuri kilicho rahisi! Lazima ugharamike ama muda, fedha, nguvu, akili, au vyote kwa pamoja.
 
Hapo ndio utajiamulia sasa ununue IST au ununue ngombe ukanywe maziwa maana vyote vinatembea na miguu minne
Bora ng'ombe. Kama ni usafiri, hata ng'ombe anaweza kutumika ikilazimu🤣
 
Ni kweli mkuu! Exposure bado ni changamoto kubwa sana kwetu. Ndiyo maana ninatamani sana niweze kuzitembelea nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
Kutembea ni mtaji mkubwa sana wenzetu Wazungu wametushinda hapo niliwahi kutana na mtoto wa miaka 14 Addis Ababa katokea Canada anaizunguka Afrika alinitajia kuwa alikua Songea na Shinyanga kipindi hicho mimi sijawahi kufika niliumia sana na hapo anataka kwenda Senegal harafu ana ratiba ya Egypt mtoto yupo peke yake ana ramani zake za kutosha na anajiamini mno anasema kila rikizo ana kazi ya kwenda Nchi kadhaa na kila akitembelea anaandika kama report hivi ya vitu tofauti alivyoviona nikasema wanaposema Nchi zimeendelea hata Bongo zao pia zipo tofauti na Nchi masikini aisee...
 
Brian Tracy, akiwa na miaka kumi na nane, alisafiri kwa gari binafsi kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Afrika Kusini. Lengo lilikuwa kusafiri kwa baiskeli kutokea Ulaya hadi Kusini mwa Afrika kuanzia Kaskazini mwa Afrika. Lakini alilazika kutumia usafiri wa gari baada ya kufahamu kuwa asingeweza kukatiza jangwa la Sahara kwa baiskeli. Anayahusisha mafanikio yake na ziara aliyoifanaya akiwa na miaka kumi na nane.

Kuna faida kubwa sana "kutembea"
 
Kwa nini motivational speakers wanadharaulika sana Tanzania? Mbona ni watu wa muhimu sana kwenye Jamii hasa kwa mazingira ya sasa yaliyojaa changamoto lukuki?
Nadhani ni kwa sababu huwa wanazungumz mengi yasiyo na uhalisia
 
Back
Top Bottom