Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wanachama Wawili wa Chama cha Wananchi CUF wa Kijiji cha Mabama Wilayani Uyui mkoa wa Tabora Husseni Hammis Kwabi Aliyekuwa Mjumbe mkutano mkuu CUF Wilaya Uyui na Mashaka Said Lintu Aliyekuwa Mjumbe kamati tendaji, Mkurugenzi wa Fedha na Meneja Kampeni wa Chama cha CUF Wilayani Uyui wametimkia Chama cha Mapinduzi CCM.
Wakizungumza katika mkutano wa kuwashukuru Wananchi wa Kijiji cha Mabama kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kijiji wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wanachama hao wamesema kuwa hawaoni haja ya kuendelea kubaki Chama Pinzani huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Rais Samia ikifanya vizuri.
Wawili hao wamekabidhi kadi za Chama cha CUF tarehe 29 Disemba, 2024 kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi CCM Wilaya ya Uyui, Shaffin Ahmedal Sumar.