Binaadamu wana hali mbaya sana kuliko wanyama....wanaotakiwa Kuokolewa sasa ni wamasai si wanyama
Jenga Hoja
Una hoja nzuri, lakini badilisha 'angle' unayotumia.
Usiseme wanaotakiwa kuokolewa ni Wamasai, badala yake sema wanaotakiwa kuokolewa ni Binadamu na mifugo yao.
Ngorongoro ni ya Watanzania wote, siyo ya Wamasai pekee.
Kuidumisha Ngorongoro, kinachotakiwa ni 'Ecological Balance'.
Ngorongoro ni 'unique' duniani, kwa maana ya Binadamu kuishi na Wanyamapori.
Hoja hapa ni kuiokoa Ngorongoro na siyo kuokoa Binadamu.
Hoja ni kuiboresha Ngorongoro ili Binadamu na Wanyamapori waendelee kuishi pamoja.
Viongozi wa MECIRA, Maulidi Kitenge na Oscar Oscar wamefanya kazi nzuri sana ya kutuhabarisha Watanzania ili tupaze sauti zetu kwa lengo la kuitunza Ngorongoro.
Uwekezaji wa Wageni usikubaliwe, lakini pia uwekezaji wa Wakazi wa Ngorongoro udhibitiwe.
Kama ujenzi katika maeneo yaliyopimwa Mijini yanahitaji kupata Kibali cha Ujenzi cha Halmashauri husika, vivyo hivyo, Ujenzi katika Hifadhi ya Ngorongoro unatakiwa udhibitiwe kwa Vibali vya Mamlaka husika.
Ngorongoro ni World Heritage na Watanzania tunalo jukumu kuitunza.