Ngorongoro hali mbaya: Maulid Kitenge ataka hatua za dharura zichukuliwe kuwanusuru Wamasai

Ngorongoro hali mbaya: Maulid Kitenge ataka hatua za dharura zichukuliwe kuwanusuru Wamasai

Kwani mbuga ni hiyo moja tu? Wahamishiwe Serengeti
Serengeti walikuwepo wakurya na waikoma wote hao waliondoshwa na wakakubali bila sinema kama hizi.

Hawa wamasai and his company wana jivunia kuwepo kwa social media kiwa free na dunia kuwa kijiji ila wale waliokuwa Serengeti hakukuwa na tweeter na jamii forum nk.
 
Sifa ya Ngorongoro ni mchanganyiko wa wanyama na binadamu hiyo ndio brand yake.

Sasa kama wanataka kuiua branda wawaondoe wamasai ili ngoro ngoro iwe mbuga sawa na nyingine.

The good things would have been to put the proper ways of how to conserve the area and not to permanently barn Maasai population in the area.
Hatuna budi kudhibiti uongezekaji wa idadi ya binadamu na viumbe wengine wafugwao na wasiofugwa ndani ya eneo la Mamlaka-Unique Eco System for Ngorongoro as a World Heritage Site.
Ninahisi utaalam wa kuweka mizania rafiki kwa vyote unahitajika na hilo ni jukumu la jamii husika,nchi na dunia kwa ujumla.
Ngorongoro Must Stay Alive for Us.Let's think big.
 
Binaadamu wana hali mbaya sana kuliko wanyama....wanaotakiwa Kuokolewa sasa ni wamasai si wanyama

Jenga Hoja
Wamasai nao ni lm wanyama tu waishi humohumo pamoja na wenzao simba na chui.
Hao watu wameishi hivyo miaka na miaka hawana habari na wala huduma za kijamii hawataki waachieni maisha yao waliyozoea.
 
Mbona Loliondo kwa Mwarabu huzungumzii umekomaa na Ngorongoro?

..idadi ya wamaasai na mifugo wakati Ngorongoro inaanzishwa ilikuwa ndogo sana ukilinganisha na sasa hivi.

..wakati tunapata uhuru Tanganyika ilikuwa na watu milioni 9 kama sijakosea. Jiulize sasa hivi tuko wangapi na eneo la ardhi halijaongezeka.

..kwa kifupi serikali imekosa mbinu na mikakati ya kushughulikia tatizo la ongezeko na watu na mifugo ktk maeneo ya karibu na mbuga za wanyama.

..Wamaasai wanatakiwa watafutiwe maeneo mazuri yenye miundombinu rafiki kwa ufugaji. Pia wafundishwe ufugaji wa kisasa ili wasishawishike kuingia mbugani kutafuta malisho.

..kuhusu eneo la Loliondo ni kweli kulikuwa na UFISADI. Lakini ni ukweli vilevile kwamba ukiruhusu mifugo iingie kwa idadi kubwa huko madhara yake kwa uhifadhi yatakuwa makubwa.

..Labda tuulize; kwani Muarabu ana ng'ombe, mbuzi, na kondoo, wangapi? Je, anaathiri mazingira kwa namna gani? Na njia za kumdhibiti ni ngumu kiasi gani?

..Ukweli mchungu ni kwamba Wamaasai wanaharibu mazingira kuliko Muarabu wa Loliondo.
 
Serengeti walikuwepo wakulya na waikoma wote hao waliondoshwa na wakakubali bila sinema kama hizi.

Hawa wamasai and his company wana jivunia kuwepo kwa social media kiwa free na dunia kuwa kijiji ila wale waliokuwa Serengeti hakukuwa na tweeter na jamii forum nk.
Tuna mbuga ngapi? acheni wamasai wachungie humo?
 
Wamasai wahamishwe kutoka Ngorongoro kwa nguvu, watolewe nje ya hifadhi, sbb hao wabishi sana, watafutiwe maeneo nje ya Ngorongoro kwa nguvu, hao huwezi ongea nao, nguvu itumike, kuongea ni kupoteza muda na hifadhi itakufa miaka si mingi ijayo.
 
Tuache siasa uchwara, Ngorongoro lazima iwe salama.

Lakini itumike njia sahihi kuwaondoa Maasai.

Tuzingatie haki za binadamu, Serikali iweke bajeti kubwa ili wasipate athari.

Ngorongoro must survive.
 
Wao wanasema wamefika, na wanapigana wasiondoke,hata sie watanzania wenzako tuko nao bega KWa bega ,Kitenge anawashwawashwa nini?masai tribe SIO watu wa anasa hata walioko mjini huwezi jua wanalalaga wapi,na ndo maana kabila hili limebaki kuwa la kipekee

Waachwe nao ni watanzania, tunazo hifadhi ngapi tz? Lakini pia mbona wemeshiriki kutunza wanyama,

Ngorongoro iwe aridhi ya wanasai period, na mbunga wakabidhiwe moja KWa moja

Yaan umeandika upupu pori kabisa.. Mbuga inayoliingizia taifa fedha za kigeni leo hii wapewe binadamu wachache kwa sababu zipi za msingi?

Kila kitu kikizidi kiasi hua ni shiida, hao wafugaji kama mifugo yao inazidi eneo husika wahamishwe kutoka humo.. hao wanyama pori pia wana haki zao

Wanyama pori wakianza kupotea bila shaka utarudi hapa kuja kuilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia Vizuri. Yaan sijui ni nani alieturoga watanzania. Hovyo sana
 
Unamsaidia mtu tajiri kuliko wewe??
Mtu ana ng'ombe elfu 3... fanya 700,000 × 3000=2,100,000,000Tshs na anapata maziwa kila siku... wewe unakuja na kapero yako na mic unataka kumsaidia.

Maasai wana namna yao ya maisha ambayo kama unataka kusuggest chochote kwao lazima uijifunze!
Unafikiri mjini kwenye lami hawapaoni?

Haya yakusema Tembo wamepungua au Simba wamepungua yanahitaji utafiti! Kwanza kama kweli wamepungua? Na je, wamasai wamechangia kiasi gani kupungua?
Usikute mtu amefika Ngorongoro hajaona tembo basi ana conclude kuwa hamna tembo.

Hiyo co-existence ya watu na wanyama pori na yenyewe ni scenario inayohitaji utafiti kwenye faida na hasara..haya maswala ya wahamiaji..haya ni purely administrative...wewe bwana hapa sio kwako, hapa umevamia, sepa! Ngoma mbona inaisha..
"Ndugu zetu wamasai wanaoishi humu wanahitaji kusaidiwa"- Kitenge
 
Kituo cha Wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa (MECIRA) kimeitaka serikali kuchukua hatua madhubuti za haraka na dharura ili kunusuru maisha ya wananchi jamii ya kimasai wanaoishi katika tarafa ya Ngorongoro iliyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na kunusuru mazingira na uhifadhi wa eneo hilo unaoonekana kuathiriwa kutokana na muingiliano wa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza.

Makamu mwenyekiti wa kituo hicho mwanahabari mkongwe Maulid Kitenge ameyasema hayo kwa niaba MECIRA muda mfupi baada ya kamati tendaji ya taasisi hiyo kutembelea hifadhi hiyo kujionea utalii na maisha ya wananchi husika kuzingatia ukweli kuwa hifadhi ya Ngorongoro ndio hifadhi pekee nchini inayohusisha maisha ya binaadamu, mifugo na wanyama

Miongoni mwa mambo yaliyomsikitisha Kitenge ni jinsi wakazi wa maeneo hayo wanavyoishi kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maji, barabara, Hospital n.k

Kitenge ameishauri Serikali kuwatafutia mahali salama pakuishi kwakazi waliopo hifadhini ili wapate huduma umuhimu za kijamii na waweze kuendelea kama binadamu wengine.

Nae Mjumbe MECIRA Oscar Oscar ameshangazwa baada ya kutembea umbali zaidi ya Km 45 lakini hajaona Wanyama zaidi ya pundamila kuchanganyika na mbuzi, ng’ombe kitendo ambacho kinahatarisha afya za wanyapori na usalama wao,

Pia ameogopeshwa na kasi ya ongezeko la wanyama wa kufugwa ng’ombr mbuzi kitu kinachosababisha Wanyamapori kukimbia, na kugombania malisho

Inasikitisha saana, hawa jamaa kabla ya uhru walikuwa wanaishi na hao wanyama sasa leo wanaonekana ni kero anyway....i wish government ingekuwa inatumia takwimu na kuona ongeeko la watu kulinganisha na limited resources Nchi inamiliki.....Mamlaka ya ngorongoro ilivyoanzishwa hawa jamaa walikuwa elfu sita tu...leo wapo zaidi ya laki na ishirini anyway hili lilitakiwa lionekane siku nyingi,,,hawaruhusiwi kulima ndio umaskini ni mkubwa ila itumike njia ambazo ni sahihi mfano wanaweza anzishiwa wilaya yao na kuhudumiwa kwa mika kadhaa kabla hawajaanza jitegemea...na sio hizi ropaganda za akina kitenge
 
Kitenge umeongea mambo ya msingi sana ila kwa jinsi ninavyowafahamu ndugu zangu wamasai watakuchukulia negatively na kupinga kwa nguvu zote kutaka kuendelea kuishi ngorongoro kuendelea kupokea kibaba cha mahindi ya bure na kuona kama kitu cha maana sana badala ya kukubali kuondoka na kujitanua kwa uhuru nje ya eneo bila kubanwa
 
Inasikitisha saana, hawa jamaa kabla ya uhru walikuwa wanaishi na hao wanyama sasa leo wanaonekana ni kero anyway....i wish government ingekuwa inatumia takwimu na kuona ongeeko la watu kulinganisha na limited resources Nchi inamiliki.....Mamlaka ya ngorongoro ilivyoanzishwa hawa jamaa walikuwa elfu sita tu...leo wapo zaidi ya laki na ishirini anyway hili lilitakiwa lionekane siku nyingi,,,hawaruhusiwi kulima ndio umaskini ni mkubwa ila itumike njia ambazo ni sahihi mfano wanaweza anzishiwa wilaya yao na kuhudumiwa kwa mika kadhaa kabla hawajaanza jitegemea...na sio hizi ropaganda za akina kitenge

..ni kwasababu wamekuwa wengi kupita kiasi.

..na mifugo pia imekuwa mingi kiasi cha kuathiri shughuli za uhifadhi.

..serikali iangalie uwezekano wa KUWAMOTISHA ili wahamie maeneo mengine Ngorongoro wabaki watu wachache.
 
Tunataka tusikie upande wa wamasai, wao wanasemaje..........maana mtu anajipa cheo kuwa semaji la wamasai.
 
Yaan umeandika upupu pori kabisa.. Mbuga inayoliingizia taifa fedha za kigeni leo hii wapewe binadamu wachache kwa sababu zipi za msingi?

Kila kitu kikizidi kiasi hua ni shiida, hao wafugaji kama mifugo yao inazidi eneo husika wahamishwe kutoka humo.. hao wanyama pori pia wana haki zao

Wanyama pori wakianza kupotea bila shaka utarudi hapa kuja kuilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia Vizuri. Yaan sijui ni nani alieturoga watanzania. Hovyo sana
Wewe ni mmoja wapo wa mipango ya kishetani, kwenda bwana nitolee takataka zako hapa aliekwambia Ngorongoro isipokuepo basi nchi itasimama nani, nyie wasomi uchwara ndo mnaliua taifa Hili period, ujuaji mwingi kumbe fisadi mkubwa,
Nakupa onyo ukiendelea utapata zawadi YAKO hapa live pitia jf,kwenda zako huko
 
Back
Top Bottom