Ngorongoro hatarini kupoteza uhai na umaarufu wake kutokana na kukithiri kwa shughuli za binadamu

Nimeshuhudia ng’ombe wa kifa, watoto wamechakaa kwa lishe duni huku uchafu ukiwa ni jambo la kawaida! Hifadhi hiyo ina wasomi wengi, ila sioni faida yoyote kutoka kwao kuifanya jamii yao ionekane bora! Ufugaji bora na uliorafiki kwa uhufadhi haupo mpango huo!
Huduma za bure ambazo hutengewa fungu kubwa ni rutuba ya maisha ya anasa kwa viongozi wachache wa kimila na wasomi wachache wa jamii hiyo ambao wengi mkiwachunguza sidhani kama wanampango na wajukuu zao kuendelea kuishi Ngorongoro, kwani huwezi kuwa msomi au kiongozi ukaacha jamii yako iingie mtegoni kwa kukiuka taratibu ili waadhibiwe!
TUNAAMBIWA KITUNZE KIKUTUNZE!
Ningeshauri kuwe na mpango wa sensa ya kila mwaka kwa binadamu! Kuzaliana sio dhambi, ila utaratibu wa kuwapanga wanajamii hawa uwepo wa kuwapa maeneo nje ya hifadhi! Wale wanaotaka kuishi kimagharibi basi wapewe eneo nje ya hifazi wajenge majumba yao waishi! Litengwe eneo katika one of the Maasai steppes wanajamii wapangiwe huko, wale walioamua kuishi kimila wabaki hii itaondoa visingizio!

Jamii hii ielimishwe kuhusu kujitegemea pia! Hifadhi zoote ni kwa ajili ya Watanzania wote! Hii dhama ya huduma bure ndio ina itesa Hifadhi!
Haihitajiki diploma au certificate ya darasa lasaba ku negotiate na wanajamii unless kuna mgongano wa kimaslahi! Ni aibu tulizoea kuona fisi au duma wakikimbiza ndama wa nyumbu pale golini lakini tulistaajabu kuona ni mbwa wa nyumbani wanafanya hiyo kazi!

Priority’s za ajira na Huduma nyingine nazo ziwe kipaumbele kwa watoto wa wazazi watakao kubali kuipa hifadhi pumzi! Kwa kufanya hivyo serikali mtajikuta mna miji yenye majina ya Ngorongoro nje ya hifadhi na mtapata kodi pia!
Ni mtazamo tu
 
Ungeisoma sheria ya hifadhi na General Management Plan ya Ngorongoro bila shaka ungejua kinacholalamikiwa hapa.
Please kabla ya kupost jiridhishe kwanza. Na kama kitu wewe ni bila bila bora ukae kimya usije kuwa jingalao!!
 
Hatari sana... Yanayoendelea Ngorongoro yamepitiliza na yanavuruga misingi ya uhifadhi.
Bahati mbaya ni kuwa tatizo limeanza kuinyemelea Serengeti.
 
Ungeisoma sheria ya hifadhi na General Management Plan ya Ngorongoro bila shaka ungejua kinacholalamikiwa hapa.
Please kabla ya kupost jiridhishe kwanza. Na kama kitu wewe ni bila bila bora ukae kimya usije kuwa jingalao!!
Sisi hatutaki mtuone tuna akili. Tunapambania urithi wetu wa karne na karne.
Mkapambanie urithi wenu huko walikochagua babu zenu.
Ya nini kuja kupambania urithi wa watu wengine?
Si mkapambanie gesi, dhahabu, almasi na theluji juu ya mlima Kilimanjaro?
Kwanini Ngorongoro iwaume sana?
 
Ukiwa sober utujulishe!!
 
Pwenti tupu yaani
 
Nyumba nyingi sana ziko maeneo mengi ya Hifadhi
Acha urongo wa kijinga labda unaongelea ngorongoro ya wapi?tuanzie kimba pale kuna nyumba chache za mbao kma lodge...nyumba ziko wilayani tu....hotel zimejengwa kufuata uhifadhi na ziko chache hazifiki 6,nyingi ni tented camps,acha kuongopea
 
Eeeeehhhh Hadi serengeti kumbe nako taa nyekundu
Kule nako kuna ujenzi holela wa hoteli.
Sites zinagawiwa kama njugu za kuonja.
Usiku ni mitaa tu inatambulisha mitaa.
Holela sana yaani...
 
Alipotajwa Habib mchange tu,hapo ndipo kila kitu kiliharibika.
 
Acha urongo wa kijinga labda unaongelea ngorongoro ya wapi?tuanzie kimba pale kuna nyumba chache za mbao kma lodge...nyumba ziko wilayani tu....hotel zimejengwa kufuata uhifadhi na ziko chache hazifiki 6,nyingi ni tented camps,acha kuongopea
Unazungumzia Kimba ya wapi?
 
Ndio nini sasa?..kwa hiyo nasisi tuibe?
Acha kupewa pesa ili uandike vibaya wananchi wanachungia mifugo yao hapo na wakati kuna maovu watwala wanafanya lakini upo kimya, mwarabu wa Loliondo mbona hujawahi kumwandika au kakutoa chochote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…