Askari Polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa mshale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa zoezi la uwekaji mpaka katika eneo la pori tengefu kwenye Tarafa ya Loliondo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema kwamba kifo hicho kilitokea Juni 10 alasiri, na kusisitiza kwamba kama serikali wanatambua uzalendo wa askari huyo.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.
Wananchi wanatakiwa na Serikali kuhama katika eneo la Ngorongoro na kwenda kuishi Handeni, Tanga ambapo Serikali itawasaidia katika kuhama. Nia ikiwa ni kuhakikisha uhifadhi endelevu katika Hifadhi ya Ngorongoro.
Baadhi ya Wananchi wa Ngorongoro hawataki kuhama katika ardhi yao ya asili kwani Wanaishi hapo kisheria na Wanatambulika.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha JOHN MONGELLA akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kuuawa kwa Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Loliondo jana Juni 10, 2022.

Hili Taifa tumerogwa. Nilisema jana huyu waziri mkuu atoke tu lakini wakaja juu Sasa ona mambo yote hadharani. Siku zote njia ya mwongo nifupi. Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema askari wao kafa kwa mshale chanzo ni vita inayoendelea Kati ya wamasai na polisi. Jana waziri mkuu alikanusha na kusema loliondo ni shwari.
Mwekezaji yoyote kitu Cha kwanza ni kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wanaomzunguka, unawekezaje katika sehemu ya mgogoro?
Hapewe hifadhi ya bugiri period,