Hapana, wakenya wameanza kugundua kwamba Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi katika maeneo mengi Sana, hasa baada ya hili janga la Corona, wachache sana, hasa waliopo hapa JF wanapata ugumu kukubali hadharani, hiyo ni hali ya kawaida kwa binadamu yeyote kukubali kushindwa kiurahisi, hasa kwa sisi waafrica.
Kuthibitisha hilo, chaguzi zote za Africa ni chache sana aliyeshindwa kukubali ameshindwa pamoja na kila kitu kuwa hadharani, mfano mzuri ni hapa Tanzania, ni wazi kwamba CCM ina nguvu za kupitiliza lakini bado upinzani unahisi kuibiwa kura. Pamoja na tafiti zote duniani kukipa ushindi CCM zaidi ya 80%, bado upinzani utapinga matokeo baada ya kutangazwa.