Nguruwe mmoja anaweza kukupa hadi zaidi ya TSh. Milioni 1 ndani ya muda huu tu!

Alafu wewe jamaa upo seriously kabisa
πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ni kweli changamoto hazikosekani, ila hakuna kisicho an changamoto
Kama utakuwa na uhakika wa chakula, mradi wa nguruwe unalipa sana kama utawekeza kwa ukubwa.
Kama utafanikiwa kuwakuza 500+, wewe utakuwa ni mtu mwingine ila mifuko lazima itoboke sana katika kuhudumia, vinginevyo uwe umelima mashamba kwa ajili ya chakula cha nguruwe.​
 
Kwa constext ya TANZANIA, kama huna mtaji mkubwa, kama wewe unajitafuta,, hii KITU hapana,,,kilimo cha kwenye makaratasi ni kweli kinalipa na faida unaweza iona lakini in reality hakuna kitu kama HICHO,

Kuna swala la chakula + unaweza anza fuga mfano pumba bei yake ni 20, 000, ikapanda mpaka uifikishe shambani kwa 43,000,, wakati wa kuuza hiyo factor dalali hatokuelewa

Kilimo + UFUGAJI Tanzania BORA uwe dalali, ndio utaiona pesa...mkulima au mfugaji hana direct access na mlaji mpaka upite kwa dalali,,,yeye anazo option anapokea mzigo sehemu mbalimbali wakwako ukimringia anaconider option nyingine....hapo bado hujauziwa DAWA na chanjo FEKI,,,, bado unasafirirsha USHURU na vibali,,,mara mlipuko wa magonjwa ;;;;unaweza likimbia shamba lako

Siku tukiweza adopt option kama ya South Africa tu kuna kuwa na ile minada angalau unaweza toboa ila mifumo tulionayo tuendelee tu kufuga kwa kujaribu si kutoboa kimaisha
 
Anaitwa Noah au Mbuzi wa ParokianiπŸ˜‚πŸ«’πŸ«’πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Pigo zanguhizi. Mwezi May nimeingiza 2m kwa kuuza vibwagala tu. Na sasa nimepandikiza tena. Naamini Novemba nitapata tena 2m
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…