Mpo salama waungwana?
Swali hili ningependa haswa kulipeleka katika pande mbili (2) kwenye sayansi na wanaoamini uwepo wa Mungu.
Katika sayansi ningependa kuhoji hivi je, ni kivipi nguvu inaweza kutengeneza/kutokeza object?
Katika upande wa Waumini wa Mungu naomba kuhoji hivi
kama ilivyoandika na vitabu vyake kwamba kwa kutumia uweza wake ama nguvu zake Mungu aliumba kila kitu. Swali hapa ni je, ni kivipi nguvu hiyo ya Mungu iliweza kuumba/kutokeza/kuunda objects kama dunia,nyota n.k?
Ni hivyo tu
Kisayansi,
Nguvu au force hutumika kushikilia elements ndogo ndogo kwa pamoja ili kutengeneza vitu.Kwa mfano, kupitia hesabu Ya sayari Ya Sir.Isaaac Newton Tunajua kwamba, sayari zilitengenezwa kwa kuvutwa kwa vipande vidogo vidogo vya gas, katika nguvu kubwa Ya presha na kugeuka Kuwa maada yabisi (solid) kutoka kwenye gesi. Nguvu kama Ya gravity, hutumika kushikilia hivi vitu kwa ziada, mfano ni mifumo yetu Ya sayari na mzunguko wake wa jua.
Mfano rahisi ni wa maji, maji hutengenezwa na matone madogo kwa pamoja, ndani ya Kila tone kuna molecule za maji mambazo hutengenezwa kwa nguvu inayoishikilia element Ya Oksijeni na Haidrojeni kwa pamoja, ndani ya haidrojeni (au Oksijeni) kuna nguvu inayoshikilia element Nyingine ndogo zaidi (protons, neutrons na electron) Hivyo hivyo mpaka chembe Ya mwisho. Ndio maana kila element hapa duniani inaweza kuvunjwa vunjwa Kisayansi na kuwa kitu kingine kwa sababu wanasayansi simply hutoa ile nguvu hapo katikati. Mfano mwingine ni kama utengenezaji wa Almasi kupitia bila kuchimba (kupitia maabara).
Mfano mwingine ni mvuke wa maji (ambao ni gesi) unaweza kubadilishwa kuna yabisi (solid) au barafu moja kwa moja bila kua kimiminika (liquid) kwanza kama tulivyozoea. Njia ambayo hutumika ni kuweka nguvu Ya mgandamizo (pressure) kubwa.
Rejea Hapa:
How much pressure is needed to force a gas into a solid? - Quora
NB: kwa Mungu ni kwa kupitia Imani. yakubidi uamini kwanza kwamba yupo yule aliyekua mkuu juu yetu, alafu kisha ukubali kwamba mpango mzima wa maisha na vitu vyake vimetengenezwa na huyo mwenye akili zaidi yetu mwanzo na mwisho wa kila kitu ameumba yeye...., uthibitisho ni mgumu kwa sababu ni suala la Imani sio vitu vinavyoonekana. Lakini labda jiulize, nguvu (force) ilizaliwaje hapo mwanzo?