Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Siku ya mwanzo Marekani na Uiengereza walipoanza kushambulia Houth kule Yemen maeneo karibu 85 ya Houth tuliambiwa yamepigwa na picha za moshi ukifuka tukarushiwa.
Kuna watu walijua Houth imeisha lakini siku iliyofuata Yahya Sarea akatoa tangazo kulenga meli nyengine na watu hawakuamini.
Baada ya hapo Marekani kipekee na wakati mwengine Uiengereza anajiunga wameshambulia mara nyingi sana.Rada zote za Houth tuliambiwa zimevunjwa vunjwa.Zaidi ya hivyo droni na makombora ya Houth tukaambiwaa sasa yanawindwa na kuwahiwa kuangamizwa kabla hata hayajarushwa hewani.
Meli na majahazi yanayopeleka silaha kwa Houth kutoka Iran mara kadhaa zimeshikwa na meli hizo kuzamishwa na shehena zake japo mara moja askari wawili wa US walisukumwa majini.
Yote hayo yaliyotokea kumbe si chochote.Houth kila siku wanarusha makombora kwa meli zenye mafungamano na Israel,Marekani na Uiengereza.Matangazo ya Houth hayabaki kuwa ni kampeni na propaganda tu bali yamekuwa yakithibitishwa na mataifa hayo bila kutaja hasara wanazozipata.
Hapo juzi na jana mfululizo meli za Uiengereza za mizigo ya nafaka na mafuta zimerushiwa makombora na kukoswa koswa.Hali hiyo haiyapi mashirika ya meli furaha na uhuru wa kutumia bahari ya red sea.
Mashirika makubwa ya usafirishaji mizigo baharini kama Maersk wamesalimu amri na kusema hawawezi kubahatisha kupita maeneo hayo ya Houth kwa kuamini ulinzi wa Marekani na Uiengereza ambao meli zao zenyewe zikiwemo za kivita haziko salama.