Wakuu, leo nataka tuongee kuhusu DNA (vinasaba)
Kuna mambo kadhaa ambayo ningependa tuyajadili na kujifunza kutoka kwa wataalamu na wenye uelewa wa masuala haya
1. DNA na mapenzi/Sexual Compatibility😊
Je, kuna namna ya kupima vinasaba vya watu wawili na kugundua kama wanaendana kibaiolojia?
I mean, kuna uwezekano DNA za watu wawili kuwa na uhusiano fulani unaoweza kufanya wanaposhiriki tendo la ndoa wakapata msisimko au raha zaidi kuliko kawaida?
2. DNA na uzazi
Je, kuna umuhimu wa wenza kupima vinasaba vyao kabla ya kupata mtoto?
Kwa mfano, mkiwa wawili mkapima DNA zenu je, inawezekana kutabiri baadhi ya sifa za mtoto mtakayempata kama vile mwonekano, urefu, rangi, uwezo fulani au uwezekano wa kurithi magonjwa ya kinasaba?
Ex: Wanandoa au wapenzi wakaamua tu kupima vinasaba ili kujua uwezekano wa wao kupata mtoto wa aina fulani.
Labda mtoto genius, n.k.
3. DNA na utamaduni wetu wa Kiafrika
Kwa utamaduni wetu wa Afrika, kwa nini inaonekana kuwa jambo gumu kufanya vipimo vya DNA tofauti na mataifa mengine?
Watu wengi wanalalamika sana wakisema mchakato ni mgumu na usio na uwazi.
4. DNA na tabia za binadamu
Lakini pia kuna jambo lingine
Unaweza kukuta mtoto ana tabia fulani ambazo wazazi wake wote wawili hawana, mpaka wazazi wenyewe wanajiuliza, huyu mtoto amerithi kwa nani?(Au ndio kitanda hakizai halamu😊)
Kwa mfano, uchoyo, majivuno au ubinafsi.
Naomba tuelewane ndugu wana jukwaa sizungumzii tabia ambazo mtoto anaweza kujifunza shuleni, kwa marafiki au kwenye mazingira anayokulia bali zile zinazoonekana mapema kabisa hata akiwa bado hajaweza kuchangamana
Je, tabia nazo ni sehemu ya DNA? Kama ndiyo inawezekanaje mtoto akawa na tabia ambazo hata wazazi wake hawana?
Au ni combination ya tabia za wazazi ndiyo huzaliwa kwa mtoto?
Karibuni tujifunze
Karibu Tujadili
Chombezo : Wanaume pimeni vinasaba kuliko kukaataa uja uzito kwa mashaka ya kua mtoto sio wako
Chombezo no2 : Wanaume pimeni vinasaba hakuna mama fake ila baba fake
ShesRise_1 ✋️