Nguvu ya Job Ndugai ilivyowasambaratisha Prof. Assad, Makonda, Tundu Lissu, Mbowe na Mpina!

Nguvu ya Job Ndugai ilivyowasambaratisha Prof. Assad, Makonda, Tundu Lissu, Mbowe na Mpina!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hao niliowataja ni wachache miongoni mwa wengi waliojaribu kupimana ubavu na mh Job Ndugai na kuangukia pua.

Wengi hawaijui nguvu ya Ndugai ndani ya CCM lakini kiukweli huyu jamaa ni very powerful.

Wako wapi leo akina Makonda, Prof Assad, Mbowe na yule aliyepima samaki kwa rula kwenye mgahawa wa bunge?
Nawashauri akina Halima Mdee na wenzake waweke imani yao kwa Spika Ndugai watavuka salama.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mtoa mada kamtaja Job kama job lakini lazima tutambue kiti cha spika ndo chenye nguvu yoyote akikalia kiti cha spika lazima awe vile.
 
Unachosema ni kama mtu kufyatua risasi ikamlenga adui/target moja kwa moja kwenye paji la uso/bull's eye halafu ukaisifia bunduki kwa jinsi inavyoweza kulenga shabaha.
 
Nchi kwa sasa inapita kwenye tanuru lamoto, baada ya hapo kila mtu atakuwa ameiva hamtataka utoto tena, unaikumbuka ile sheria ya majuzi inayoongeza watu wataolindwa na katiba hata kama wakiivunja? ni akina nani waliipitisha? unawakumbuka walioikataa katiba ya warioba? kwa nini waliikataa?

Historia ya nchi yetu inaandikwa upya na safari hii haitambeba mtu! ulishawahi kusikia mtu furani mkubwa anaitwa MANGUNGO tunakoenda kina mangungowatakuwa wengi subirini mtaona.
 
Hao niliowataja ni wachache miongoni mwa wengi waliojaribu kupimana ubavu na mh Job Ndugai na kuangukia pua...
Huyo Spika Ndugai nguvu yake inatokana na Jiwe ambaye ndivyo anavyotaka serikali yake iendeshwe kwa kutozingatia hata Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama, ambayo hao viongozi wote waliapa kuitii na kuiheshimu kabla hawajakabidhiwa majukumu waliyo nayo.
 
Hao niliowataja ni wachache miongoni mwa wengi waliojaribu kupimana ubavu na mh Job Ndugai na kuangukia pua.
Hivi huwa unalipwa kiasi gani kila siku kupost issues ambazo hazina faida yoyote kwa taifa na kwako mwenyewe? Hata unao watetea hawakujali yani.
 
Back
Top Bottom